50 kwa 50 ni bomu linalosubiri kulipuka.

pierre buyoya

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
476
163
Hamsini kwa Hamsini ni kauli mbiu yenye lengo la kuleta usawa wa kijinsia baina ya Wanawake na wanaume katika jamii, Kauli mbiu ina lengo zuri sana na imeegemea zaid katika kumsaidia mwanamke afikie malengo yake na apate haki sawa na mwanaume . . .

Ni kweli kabsa kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na kitu kinaitwa mfumo dume ambacho kilikuwa kinamnyima mwanamke nafasi ya kuonesha uwezo wake katika maamuzi katika jamii, Hivyo ilikuwa ni lazima kupiga vota mfumo huo ili mtoto wa kike apate nafasi . . .

Ila kaulimbiu hii imeenda na inapoelekea inafika pabaya na inapoelekea itakuwa inaleta chuki kwenye jamii, Naomba niseme ukweli tu kama anavyosema Mhe. Rais Magufuli "Msema kwel ni mpenzi wa Mungu" kuna mambo ambayo tuliyapiga vita sana na ndio lengo kuu la kaulimbiu hii, Maswala kama Ndoa za utotoni, ukeketaji na mila nyingine potofu ambazo zilikuwa zinamnyima nafasi mtoto wa kike kupata elimu. Ila siungi Mkono hata kidogo 50/50 kwenye nafasi za uongozi bila kuangalia vigezo na uzoefu . . .

Baada ya Rais kutoa majina ya Wakuu wapya wa mikoa baadhi ya wanaharakati wamekuja juu na kusema kuwa Rais hajaitendea haki Kaulimbiu ya 50/50, Hili swala halina mantik kabisa kama Rais amekaa akaona hao ndio watu wanaofaa kumsaidia na katoa nafasi kwa wanawake na wanaume kwann mng'ang'anie kaulimbiu hyo ambayo lengo lake mwanzo kabisa haikua kupewa tu ili itimie 50/50. . .

Nichukulie mfano wa mataifa yalioendeleka kama Marekani, Marekani ina miaka kibao na imefanya chaguzi kuu nyingi sana ila ukiangalia mpaka sasa kuna mgombea urais Mmoja tu wa kike. Ukiangalia Maseneta marekani wanawake ni asilimia 20 tu, hatakwenye serikali kuu pia wanawake wako wachache. Si kwamba hawastahili hapana ila watu wote wanapaswa kupewa haki sawa kila mmoja atajua ni namna gan atatumia uhuru aliopewa ili awe na manufaa kwa taifa lake na apewe nafasi ya maamuzi . . .

Kenya kule sasa hivi kuna vyama vya Wanaume wanaodai haki zao sijui kama sababu ni kama zitakazotokea huku ila Kama tukiendelea na hamsini kwa hamsini ya namna hii si ajabu ikawa bomu kubwa linalosubiri kulipuka muda wowote. . .

d41b2f402f4de985af2be0c5502616aa.jpg
 
Back
Top Bottom