50 Cent atamba kumficha Jay Z mwishoni mwa mwaka na albam mpya

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
50-Cent.jpg

Baada ya kuikosoa vikali albam ya Jay Z ‘4:44’, 50 Cent ametangaza kuonesha mfano kwa vitendo kwa kuachia albam mpya mwishoni mwa mwaka huu akitamba kuwa itaipiku ya Jigga.

Kiongozi huyo wa G-Unit ambaye hajaachia albam rasmi tangu mwaka 2014 alipoachia ‘Animal Ambition’, amedai kuwa albam hiyo itakuwa na ladha bora zaidi na inayowapa shangwe mashabiki tofauti ya 4:44 ambayo alidai ina lugha ya kisomi na kwamba ni muziki wa kwenye uwanja wa golf.

Wakati 50 Cent anaichana 4:44, Jigga ameendelea kuweka rekodi kubwa na albam hiyo akifika mauzo ya ‘Platinum’ ndani ya wiki chache.

“Nina albam ambayo nilikuwa nasubiri kuiachia,” 50 alifunguka kwenye kipindi cha Access Hollywood Live.

“Itatoka mwishoni mwa mwaka huu. Haitakuwa ‘smart’ kama ya Jay Z. Nataka kufanya muziki ambao watu wakiusikiliza wanapata shangwe. Huwezi kuupata haraka hadi ukae chini uchambue,” alitamba.

Ingawa 50 Cent hakuweka wazi jina la albam hiyo, huenda ikawa ni ‘Street Kings Immortal’ (SKI), jina la mradi aliowahi kuupigia debe tangu mwaka 2012.

Mwaka jana Fiddy aliwahi kusema kwenye moja kati ya mahojiano yake kuwa hawezi kufanya mradi mwingine kabla hajaachia SKI.

Kwa Hisani ya Dar24
 
50 Bana, hajaachia ngoma anajinadi itakuwa nzuri anasahau Mashabiki ndo ambao wataikubali au wataona ya kawaida
 
Mzee wa;
If I fell off tomorrow, would you still love me?
If I didn't smell so good, would you still hug me?
If I got locked up and sentenced to a quarter century
Could I count on you to be there to support me mentally?
If I went back to a hoopty from a Benz
Would you poof and disappear like some of my friends?
If I was hit and I was hurt, would you be by my side?
If it was time to put in work, would you be down to ride?

Nimemisi mashairi kama haya. Siku hizi fifty kama twenty, hakuna kitu.
 
Mzee wa;
If I fell off tomorrow, would you still love me?
If I didn't smell so good, would you still hug me?
If I got locked up and sentenced to a quarter century
Could I count on you to be there to support me mentally?
If I went back to a hoopty from a Benz
Would you poof and disappear like some of my friends?
If I was hit and I was hurt, would you be by my side?
If it was time to put in work, would you be down to ride?

Nimemisi mashairi kama haya. Siku hizi fifty kama twenty, hakuna kitu.
Ngoja tu wait tu Anna namna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jay z ni freemason mkubwa zaidi asee 50 cent jipange

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Freemason ni imani na dhehebu wala haimaanishi jay z kuwa kiongozi mkubwa katika jamii ya freemason ( illuminati ) ndio anaweza kila kitu hapana sio sahihi ni cheo tu wamezidiana ila kwenye ufanisi wa kazi kiuhalisia 50 cent anaweza kuwa mzuri au hata jay z mwenyewe,

Mfano mzuri ni huu.
Msanii meek mill ni moja wa wanachama katika jumuiya ya freemason lakini ameshindwa kiuwezo wa pesa na kuimba na msanii pusha T.

Kuwa mwanachama au kiongozi kwenye hii jumuiya haimaanishi ndio kila kitu utaweza, la hasha bidii yako na nguvu yako katika kazi na kutafuta pesa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom