50,000/= TZS note coming soon?

Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,686
0
nimesikia tetesi ya kwamba kuna noti ya elfu tano, can anyone proove this?

Nadhani ulitaka kuandika 50,000/- rekebisha....

Inawezekana maana mwekundu hana thamani tena ukinywa chai restaurant tu kwishney
 
Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,557
2,000
ngoja JK aanze kazi, maana nchi haina pesa n amafuta na umeme unapandishwa na kodi hakusanyi anawaonea aibu, ngoja mkuu mziki mkubwa unakuja sasa hivi, tutafika mpaka noti ya 1000000 kam Zim
 
pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
4,122
2,000
Tusipoangalia rate ya kuanguka shilingi yetu itawapita hata hao majirani anakotawala yule king'ang'anizi mkuu. Inatisha. Siwashangai wanaodai malipo ya dola!

Wachumi wetu - ipeni serikali (kama itawasikiliza) mikakati mathubuti ya kupambana na hali hii.
 
Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Kama kwa muda huu aliokuwepo madarakani, shilingi imeporomoka kwa zaidi ya asilimia hamsini, ina maana miaka mingine mitano atafikisha asilimia 200. US dollar 1 itakuwa ni sawa na sh 3000 ya tz. Hapo atalazimika kuchapisha hata noti ya sh 100,000/=. Kwa hali ilivyo nchini hivi sasa, ni kila mtu anatakiwa kubeba mzigo wake mwenyewe.
 
pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
4,122
2,000
Biashara ya pochi za fedha imebidi ife - pochi hazina ubavu wa kubeba mabunda!
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,528
2,000
Tusipoangalia rate ya kuanguka shilingi yetu itawapita hata hao majirani anakotawala yule king'ang'anizi mkuu. Inatisha. Siwashangai wanaodai malipo ya dola!

Wachumi wetu - ipeni serikali (kama itawasikiliza) mikakati mathubuti ya kupambana na hali hii.

sirikali yetu inaambilika?. CUF wamempa ilani yetu ya uchaguzi nadhani itamsaidia
 
Makame

JF-Expert Member
Jan 3, 2008
512
0
Wadau, being critical is acceptable, but not over critical.

Siku zote mnapaswa kutumia vielelezo kujenga hoja, na sio kubwabwaja tu; na iwe vielelezo makini; sio UCHAKACHUZI.

mwaka 2005 JK alipoingia Madarakani Exchange rate ya Tshs against USD ilikue Tshs 1235 - 1260/ USD; sasa exchange rate ni Tshs 1475 - 1505/USD.

Hio devaluation ya Tshs against the USD haijaawahi kufikia hio ASILIMIA HAMSINI. Jamani, jamani, msichakachue data zisizokuwa zenyewe.

Likewise, kuna sababu kadhaa zinazoweza kupelekea Tsh kushuka thamani kulinganishwa na USD za kiuchumi ambazo sio viashiria vya Uchumi kuzorota. Ningewashauri huu uwanja musiuingie kwani utahitaji Darasa refu kidogo.

All in all, Economy ya Tanzania inakua.

Pili, kule Ulaya kuna noti ya Euro 1000, ambapo Euro moja ni Tshs 2000, hivyo kuna noti ya Tshs 2,000,000. Kama Benki kuu itaona umuhimu wa kutoa Currency ya 50,000/= hakuna mushkeli, sema itazunguka zaidi mijini.
 
wakushanga

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
552
225
Makame,
all in all Economy ya Tanzania inakuwa; mhh........!!!!!! :nono:

eti wana JF hii nikweli!!!!?????
 
spartacus

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
428
195
point tupu, congrats kaka, most of diz JF guys hupenda kuongea kwa ushabiki na sio facts, tena sababu ya kuchange 1$ kwa 1505 now no coz of marekani wenyewe, kipind hiki cha vita wanabana dola, na hivyo kununuliwa kwa thamani kubwa, and tatizo sio tz tu, even nchi jirani, wakafanye uchunguz kenya, 2005 walikua wana rate ipi na leo ni ipi.

Wadau, being critical is acceptable, but not over critical.

Siku zote mnapaswa kutumia vielelezo kujenga hoja, na sio kubwabwaja tu; na iwe vielelezo makini; sio UCHAKACHUZI.

mwaka 2005 JK alipoingia Madarakani Exchange rate ya Tshs against USD ilikue Tshs 1235 - 1260/ USD; sasa exchange rate ni Tshs 1475 - 1505/USD.

Hio devaluation ya Tshs against the USD haijaawahi kufikia hio ASILIMIA HAMSINI. Jamani, jamani, msichakachue data zisizokuwa zenyewe.

Likewise, kuna sababu kadhaa zinazoweza kupelekea Tsh kushuka thamani kulinganishwa na USD za kiuchumi ambazo sio viashiria vya Uchumi kuzorota. Ningewashauri huu uwanja musiuingie kwani utahitaji Darasa refu kidogo.

All in all, Economy ya Tanzania inakua.

Pili, kule Ulaya kuna noti ya Euro 1000, ambapo Euro moja ni Tshs 2000, hivyo kuna noti ya Tshs 2,000,000. Kama Benki kuu itaona umuhimu wa kutoa Currency ya 50,000/= hakuna mushkeli, sema itazunguka zaidi mijini.
 
FADHILIEJ

Senior Member
Nov 5, 2010
132
195
Suala la kukua kwa uchumi halina maana yeyote kama hali za maisha yawatu wa kawaida haiimariki,mathalan wakati jk anaingia madrakani sukari ilikuwa tshs 600-800 sasa ni zaidi ya 1600,kiberiti kilikuwa 20tshs sasa 50shs,hapo uchumi kukua una maana gai?
 
Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,523
2,000
Kama ni kweli basi ndo uje thamani ya tsh inavyoshuka. Wenzete Kenya note kubwa ni buku!
 
Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,940
0
Tusipoangalia rate ya kuanguka shilingi yetu itawapita hata hao majirani anakotawala yule king'ang'anizi mkuu. Inatisha. Siwashangai wanaodai malipo ya dola!

Wachumi wetu - ipeni serikali (kama itawasikiliza) mikakati mathubuti ya kupambana na hali hii.

Siwezi kushangaa Mawaziri na maofisa wakubwa wa Tanzania wana account wameweka hela zao kwenye USD.- Hii Ina maaana hata mawaziri na wachumi hawana imani na Noti ya nchi yao. Ni vipi watatunga policy za kuimarisha Tsh????

Nchi kama south africa Kiongozi kuwa na account ya USD ni kashfa kama wanzo ni kwa kificho ficho Nchi kama south africa unaweza kuhangaika kupata huduma kama huna rand lakini si kwa tanzania. Watunga sera na policy maker wametengeza mazingira hata sisi raia na wao tunakosa imani na fedha yetu kwa kisingizo cha soko huria.
 
Makame

JF-Expert Member
Jan 3, 2008
512
0
Hilo ni suala jengine, la INCOME DISTRIBUTION.

Hio kikawaida ni changamoto, tena haipo kwenye Nchi za Ulimwengu wa tatu tu, bali hata huko kwenye maendeleo.

HOJA YA MSINGI.

1. Uchumi unakuwa.
2. Shilingi haijashuka thamani kwa asilimia hamsini tangu 2005; JK alipopata Urais.
3. kushuka kwa thamani ya shilingi sio lazima kiwe ni kiashiria cha kudorora kwa uchumi.
4. Kuwa na Currency Note ya Tshs sio jambo la kubezwa. kwani wangapi wanaenda sehemu mbali mbali na kutakiwa kulipa hela zaidi ya Tshs 50000 kununulia bidhaa au huduma?

Baada ya HOJA hio, tunaweza kufungua mjadala wa Income Distribution, ambao utakuwa mrefu mno.

Nawasilisha

Suala la kukua kwa uchumi halina maana yeyote kama hali za maisha yawatu wa kawaida haiimariki,mathalan wakati jk anaingia madrakani sukari ilikuwa tshs 600-800 sasa ni zaidi ya 1600,kiberiti kilikuwa 20tshs sasa 50shs,hapo uchumi kukua una maana gai?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom