50.000/= kuhudhuria maonyesho ya kwaya kumsifu Mungu ni dhuluma

chapachapa

Member
Jan 14, 2013
93
21
Nasema si haki wala halali kwa wanaofanya biashara kupitia neno la Mungu.

Kuna kampuni inatangaza kwamba kutakuwa na kwaya mbalimbali zitakazotumbuiza wakati wa xmas lakini kiingilio kwa high table ni 50,000/= Jamani kwa Mungu kuna high table? Kumtukuza Mungu mpaka niwe na pesa zote hizo? Mbona mmepata bure lakini hamtaki kutoa bure?

Itafika wakati watu watakata tamaa kuwa miongoni mwa wanaomtukuza Mungu. Kwa kweli kupiga dili kali kama hili kupitia Mungu ni noma na sio ucha Mungu.
 
Leo ndio mnaamka? Makanisa kama uyoga kule mitaani na sadaka ni lazima tena kwa kiwango kilichowekwa, hutaki hupati kiti cha kukalia au usije kabisa, kama ulikuwa unajua bado dini ni ibada Pole sana, dini ni biashara kama zingine, swali dogo tu Makanisa yote yana mabango na matangazo yakuelekeza yalipo kama vile Hotel, guest house na biashara zingine, upo au bado usingizi?
 
I see.....
 
Biblia inasema na watu wale madhabauni.
Na pia waishi kwa kupitia injili.
Hilo ni Onyesho, waimbaji wanamsifu Mungu na kupata pesa hapo hapo. Kama huna Pesa, tulia nyumbani na msifu Mungu wako kivyako vyako kwa Tenzi za Rohoni na Mapambio.
 
Makanisa haya yanayojitangaza vipindi kupitia luninga(kulipia airtime)hii ni biashara 100% haya nayo ni majipu...kenya walikua na mpango wa kuanza kuyapunguza
 
Hapo kwa red panatosha kujua kuwa hii ni biashara tena kubwa sana.
 
Umelazimishwa kwenda? Kwani ukienda ama usipoenda ndo utaenda mbinguni? Baki nyumbani, waache wanaoweza kutoa hiyo Elfu 50 waende.
 
Makanisa haya yanayojitangaza vipindi kupitia luninga(kulipia airtime)hii ni biashara 100% haya nayo ni majipu...kenya walikua na mpango wa kuanza kuyapunguza

Cie tusiyapunguze Bali yaanze kulipa kodi kamailivyo kwa maduka,bar,hotel n.k
 
Siku hizi hakuna dini bali ni watoza ushuru,dawa ni kuwapotezea kama ninavyofanya mimi,nikienda kanisani sitowi sadaka hata sh.hamsini ni kimyakimya,
 
Biblia inasema na watu wale madhabauni.
Na pia waishi kwa kupitia injili.
Hilo ni Onyesho, waimbaji wanamsifu Mungu na kupata pesa hapo hapo. Kama huna Pesa, tulia nyumbani na msifu Mungu wako kivyako vyako kwa Tenzi za Rohoni na Mapambio.

Wito wangu ni kwamba haina haja ya kulipa mapesa yote hayo badala yake nunua kanda na cd maana baraka za Mungu hazinunuliwi
 
Wakuu;

ni kweli kabisa kwamba haingii akilini kutoza fedha hasa nyingi kiasi hicho kwa ajili ya kongamano kama hili. lakini vitu vingine pembeni, huu ni ujasiriamali kama ujasiriamali mwingine, yaani ni eneo la burudani. na hawa waimbaji watalipwa pia, na ukumbi utalipiwa, na vitu vingine kadha wa kadha. badala ya imani yako kwa Mungu kutetereka kwa sababu ya kitu kama hiki, we endelea kutazama wapi ulijifunza habari za Mungu na usimamie msimamo wako. Kipimo chako kisiwe binadamu gani kafanya nini maan utafika wakati utakata tamaa maana binadamu wana mengi sana. linapofika suala la imani ni wewe na Mungu wako ilimradi unao uwezo wa kufanya maamuzi sahihi
misahafu iko wazi kabisa kuhusu dini ama imani iliyo bora, jisomee upate maarifa ili usiyumbishwe
 
Ndiyo maana hata wageni wasio kuwa na nia njema na nchi hii wanawezatumia njia ya dini kuingia kirahisi na kutekeleza azma yao mbaya. Hapo kale serikali ilikuwa na njia ya kuthibiti. Sasa hivi wameaachia
 
Msama ni mwizi wa karne..... Anaishi hapa mjini kwa matamasha ya injili huku akiwaibia wananchi...... Jamaa ni mwizi vibaya sana
 
Nasema si haki wala halali kwa wanaofanya biashara kupitia neno la Mungu.

Kuna kampuni inatangaza kwamba kutakuwa na kwaya mbalimbali zitakazotumbuiza wakati wa xmas lakini kiingilio kwa high table ni 50,000/= Jamani kwa Mungu kuna high table? Kumtukuza Mungu mpaka niwe na pesa zote hizo? Mbona mmepata bure lakini hamtaki kutoa bure?

Itafika wakati watu watakata tamaa kuwa miongoni mwa wanaomtukuza Mungu. Kwa kweli kupiga dili kali kama hili kupitia Mungu ni noma na sio ucha Mungu.

Umeona? Hao ni wachumia tumbo hakuna kusifu wala nini ni biashara tu
 
Mtume Paulo anasema 'Yeye hakumuelemea mtu' alitangaza neno la Mungu na bado alifanya kazi nyingine ya kumuingizia kipato. Kamwe hakuwafanya wafuasi wake kama chanzo cha mapato yake. Hata Yesu Kristu aliwafundisha wanafunzi wake, aliwaponya wagonjwa lakini hakuwatoza chochote ali neno la anayetumikia hekaluni ale vya hekaluni. Yesu pia alichukia walifanya hekalu la bwana kama pango la biashara. Sijajua, ni biblia ipi inayosema pigeni zeze na vinumbi mkisubiri ujira wa pesa. Ni ukanja njaaa umeingia makanisani.Tukubali siku hizi kila kitu ni biashara hata mavi ya kuku yanauzwa.

Back
Top Bottom