5 bila za Dr Slaa, CHADEMA kwa serikali na jeshi la polisi

Wana JF nimefurahia sana majibu ya Dr. Slaa kwa polisi

1. Chadema hawana imani na jeshi ya police

2. Polisi waseme kwa nini mara zote wapinzani wanapolalamika polisi hawapatiwi majibu i.ekupigwa kwa polisi mwanza, mauaji ya raia arusha, mauaji ya igunga, mauaji arumeru nk.

3. viko wapi vinasa sauti walivyochukua hotelini kwa dr slaa dodoma

3. Kama wanaweza kuzuia mikutano ya chadema kwa kupata taarifa za kiitelijensia basi watumie vyanzo hivyohivyo kupata taarifa za mpango wa kuwadhuru dr. slaa, mnyika na lema.

4. Dr. Slaa na wenzake hawatajipeleka polisi kuhojiwa

5. Kama polisi wanataka basi waende wakawakamate

Kwa kweli hizi point zote ziko hot na kama polisi na nchimbi hawatazitafakari wakaamua kutumia mabavu na udhaifu kujibu basi wanaweza kuiweka serikali na jeshi la polisi pabaya.

Nasema hivi kwa sababu it is naked fact kwamba mambo yasiyokuwa ya msingi sana kama kuuawa kwa mwekezaji, kuawa kwa faru nk tumeona polisi wakichukua hatua kwa haraka sana tofauti na wawekezaji kuua raia, wizi wa nyara za serikali ikiwepo kusafirishwa nje kwa wanyama ikiwepo nembo ya taifa (twiga) nk.

Mchimbi elewa tanzania ya jana si ya leo,...... mwema cheo ni dhamana.....ccm nao wajue mwisho wa ubaya ni aibu.
NAWASILISHA
Vita mbaya katika nchi hii nabashiri itaanzishwa na ukandamizaji wa Polisi
 
Slaa kama anatakakuwa rais wa TZ halafu anadharau vyombo vyo ulinzi na usalama, je ikitokea 2015 akashinda inamaana ataanzisha jeshi, polisi na TISS yake? anaweza kufanya hivyo kwa kipindi kifupi? kwa nini anajisahau kama yeye ni states man hivyo awe muungwana na aache kuropoka ropoka? and by the way yeye ni mtu mzima busara anazitumiaga saa ngapi hasa anapotoa matamshi ya hear say tu maana anadai ana watu very reliable ndani ya TISS sasa anaogopa nini? si watamwambia siku na saa ya kuuwawa?

Slaa acha kudharau kazi za askari maana ni hao hao watakupigia saluti ukiwa rais najua huna washauri wazuri maana kila mtu anajaribu kukusifu na kukutukuza kwa kila unachosema yaani hata ukikohoa wanakusifu lakini hawakusaidii kitu, fahamu hata Gaddafi alikua anaabudiwa hivyo hivyo lakini mwishowe sote tuna fahamu kilicho mtokea so acha kuruhusu hizi sifa za kijinga!

I AM OUT!

hahahahahahaha! umenichekesha kweli kumfananisha Dr Slaa na Gaddafi! any way na wewe ndiyo mawazo yako hayo!
 
hapa ndo tunamis lema bungeni angelikuwepo tena mwaka huu tungelisikia mengi kutoka kwake kama alivyosemaga mwaka jana akisoma hotuba ya kambi ya upinzani
 
Slaa kama anatakakuwa rais wa TZ halafu anadharau vyombo vyo ulinzi na usalama, je ikitokea 2015 akashinda inamaana ataanzisha jeshi, polisi na TISS yake? anaweza kufanya hivyo kwa kipindi kifupi? kwa nini anajisahau kama yeye ni states man hivyo awe muungwana na aache kuropoka ropoka? and by the way yeye ni mtu mzima busara anazitumiaga saa ngapi hasa anapotoa matamshi ya hear say tu maana anadai ana watu very reliable ndani ya TISS sasa anaogopa nini? si watamwambia siku na saa ya kuuwawa?

Slaa acha kudharau kazi za askari maana ni hao hao watakupigia saluti ukiwa rais najua huna washauri wazuri maana kila mtu anajaribu kukusifu na kukutukuza kwa kila unachosema yaani hata ukikohoa wanakusifu lakini hawakusaidii kitu, fahamu hata Gaddafi alikua anaabudiwa hivyo hivyo lakini mwishowe sote tuna fahamu kilicho mtokea so acha kuruhusu hizi sifa za kijinga!

I AM OUT!

Tatizo hapa sio mbwa bali ni mfuga mbwa mwenyew alivyowafunza mbwa wake. kawaida watumishi wa ngazi za chini wakiboronga, waziri ndiye anayetakiwa kuwajibika. Kwa hiyo slaa hajadharau jeshi la polisi, bali amedharau jeshi la polisi linavyotumiwa vibaya na viongozi wao kiasi cha kukosa imani kwa jamii.

Kuna baadhi ya mawaziri wachache wanaosimamia haki katika wizara zao kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kujenga imani na serikali kwa sababu yao, vile vile wapo waliolala kiasi cha kuwafanya wananchi kutamani mabadiliko ya uongozi haraka, kwa hiyo kama kiongozi wa juu atawaamsha walio chini yake hata kauli kama hizo za akina slaa hazitasikika kwani kabla ya kuzisema hadharani atazipeleka panapohusika na akipatiwa majibu mwafaka atatulia.

Wewe Nyantella ndugu yangu, watu wakikosa imani na jeshi la polisi pia ishara zake zinaonekana, hivi majuzi nadhani umesikia wananchi wamewapora watuhumiwa kutoka mikononi mwa polisi wakawahukumu kwa sheria zao za mikononi. Ukiona hivyi ujue viongozi wa jeshi hilo wamepumzika.
 
Back
Top Bottom