5 Acres Plot for Sale at Iyumbu Estate Center, Dodoma

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
2,000
Kiwanja chenye ukubwa wa ekari 5.2 kinauzwa Dodoma mkabala na NHC Iyumbu Estate Centre ambapo rais alizindua mradi wa Iyumbu Estate Center na kununua nyumba 60. Mradi wa NHC ni nyumba 300. Eneo liko kilometer 2 kutoka UDom Administration block.

Kiwanja kina hati ya miaka 33 iliyotolewa na CDA na limetengwa kwa ajili ya shule ya sekondari ingawa sheria inaruhusu mabadiliko. Bei ni 500m na mazungumzo yapo.

Call or Sms 0787377511
 
Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,416
2,000
hivi unaijua mil 500 au unaweza tu kuiandika hizo tarakimu zake?
Mkuu sio nyingi sana kwa mwekezaji anayehitaji eneo kubwa mjini. Hivi nyumba moja ya gharama nafuu ya NHC inauzwa kiasi gani? Ukijua hilo ndipo useme kama 500m kwa ekari 5 ndani ya manispaa kama ni kubwa sana au ni wastani.

Vv
 
Mdhamini

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
218
250

Mkuu kwani hiki kiwanja umekipataje? Ulinunua sh ngapi na mwaka gani?
 
Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
2,000
Mkuu kwani hiki kiwanja umekipataje? Ulinunua sh ngapi na mwaka gani?
Awali ilikuwa shamba, nilikwepa vihunzi vingi kutoka NHC waliotaka wanilipe fidia ili wachukue na CDA. Hatimaye nilifanikiwa kupima na kupata hati.
 
Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
2,000
500m? Jaribu kunielewesha vizuri kwanza kwanini hiyo bei.
Utapata wapi ekari 5 za pamoja na utazifanyia nini? Waonahitaji kuwekeza hilo eneo ni zuri, sio kwa ajili ya makazi. Hata hivyo mazungumzo yapo.
 
Mdhamini

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
218
250
Awali ilikuwa shamba, nilikwepa vihunzi vingi kutoka NHC waliotaka wanilipe fidia ili wachukue na CDA. Hatimaye nilifanikiwa kupima na kupata hati.
Hongera kwa kupambana. Hauwezi ukapunguza punguza bei ili watu waweze kumudu kununua.
 
Thesis

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,611
2,000
Nyumba moja ya NHC Iyumbu estate inauzwaje?
Mkuu, thamani ya nyumba za Iyumbu haitokani na thamani ya kiwanja bali inatokana na ukweli kwamba nyumba zile NHC wamejenga kwa mkopo, kama tujuavyo mikopo ina riba inayotozwa kila mwaka, hivyo hiyo riba ime inflate bei ya nyumba zile.

Pili, NHC ndio waliopeleka maji pale na umeme na wamevuta toka mbali, hivyo gharama hii imeongezwa kwenye gharama ya nyumba.

Tatu, NHC wanatengeneza barabara wenyewe ambazo zinachongwa kwa motorgrader, yote hiyo imeongezwa kwenye gharama za nyumba.

nne, ni kuwa nyumba za NHC ile bei imekuwa inflated sana kwasababu hazina thamani ya ile bei tuliotajiwa, nyumba ya 76M mtu unaweza kujenga kwa 30-40M. Infact kwa mtu mchumi na anaeweza kusimamia ujenzi wa nyumba yake hawezi nunua nyumba za NHC kwa bei ile. Naamini, bei ya nyumba za NHC iyumbu kwa asilimia zaidi ya themanini haitokani na thamani ya ardhi pale bali ni factors nyingine.

Je, wewe viwanja vyako umeshakita nguzo za umeme? umeshaweka maji? Umeshachonga barabara ya kutoka na kuongia ambayo ina water drainage system?
Jifunze biashara vizuri mkuu, pia jifunze kufanya valuation. Eka moja Dodoma maeneo mengi ambayo bado haijapimwa ni 3M, Maeneo ambayo imepimwa ni 12-20M. Pole mkuu. Limbukeni ndio anaweza nunua hilo plot lako kwa 500M. Tambua tu kuwa thamani ya ardhi ya Dodoma mjini iliyopimwa ni 1SQM haizidi 6,500. This is a fact.
 
Hizo factors ndizo zinazo-dermine bei ya soko hapo Iyumbu, ,kuwa karibu na UDom ni factor nyingine, barabara ya kutoka Dar inachepukishwa kule.

Plot iko opposite na NHC Iyumbu estate, mmiliki atatumia barabara inayoingia NHC Iyumbu estate, maji atachukua bomba linaloingia NHC na hata umeme atachukua huo unaoingia NHC Estate. Mmiliki anaweza kupanga fremu pale na wateja wanakuwa wakazi wa NHC Iyumbu estate maana wanatenganishwa na barabara, akijenga shule tayari pale NHC Iyumbu estate kuna familia 300!

Kumbuka pia wakazi wa NHC Iyumbu estate hawafanani na wale wa Chang'ombe au Kizota, hadhi yao sio ya kupeleka watoto wao St. Kayumba

Sasa utahamisha mtaa kule mmoja pale Majengo, Kizota au Chang'ombe, ukiwajengea English Medium school watawaleta watoto wao wasome hapo? Ukiweka shopping mall au Supernarkets Chang'ombe au Majengo hao wakazi wa maeneo hayo ndio wanunuzi wakuu wenye hadhi za kufanya shopping kwenye hizo supermarket na shopping malls utakazowawekea wakazi wa NHC Iyumbu?

Hata hivyo maongezi kwa aliye serious yapo. Unakaribishwa.
 
ukiuza 500M utatutaarifu mkuu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom