45yrs, Mapinduzi ya Zanzibar

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844

...tukiwa tunaelekea tarehe 12.January, si vibaya tukijikumbusha ilikuwaje miaka 45 ilopita siku ya mapinduzi ya Zanzibar kwa picha.
View attachment 3250
...serikali ya Zanzibar huru chini ya utawala wa Sultani Jamshid, ilokuwa ikiongozwa na Shamte.

...wananchi walochoshwa na ubwana na utwana wakichapana mikwaju, mawe, mashoka na mapanga kuelekea mapinduzi yaliyodumu masaa tisa.

...mass grave kuonyesha umati wa watu waliofariki katika mapinduzi hayo.

...Field Marshall Okelo, kiongozi wa mapinduzi hayo akiwa na wafuasi wake

...picha kwa hisani ya www.zanzibarhistory.org
 
Last edited:
Huyu Fieldmashiall Okelo mbona huwa angolewei katika kukumbuka siku hi?i. Uwa tunasikia habari za hayati Karume zikiongelewa na viongozi wengine. Au kwa kuwa hakuwa raia wa Tanzania ndio maana habari zake hazitiwili kipau mbele?
 
...swali zuri, fuatilia picha zifuatazo,

..."inasemekana" Abdulrahman Babu alitumia ngalawa kwenda Unguja baada ya mapinduzi, kama alivyotumia ngalawa baada ya kuuwawa Karume
...baada ya Mapinduzi, Okello na Karume...washkaji!?
View attachment 3258
...Okello mbaroni!...baada ya hapo? wengine watatusaidia 'kuutafuta undani'...
 
Last edited:
...Mzee Abeid Amaan Karume alishawishi wananchi moyo wa ujamaa na kujitegemea mfano ujenzi wa majumba ya maendeleo ya michenzani, kilimani, makunduchi nk...
 
na hii leo wananchi wanaonja machungu ya mapinduzi maana ukienda zanzibar weyeji kazi hawana na njaa kali wanakimbilia Tanzania Bara hiyo ndio faida sasa Wazanzibari wanatawaliwa na watangayika baada ya kujikomboa kwa Sultani waswahili wamesema (ukiruka mkoyo utakanyaga mavi) ndio haya sasa cha kukila wanakitafuta stahili yao na serekali ya mapinduzi na hao waarabu walakula kuku OMAN.
 
Yakhe, hebu tulia na uandike vizuri.... Ulichoandika hapo juu hakifahamiki...!
 
na hii leo wananchi wanaonja machungu ya mapinduzi maana ukienda zanzibar weyeji kazi hawana na njaa kali wanakimbilia Tanzania Bara hiyo ndio faida sasa Wazanzibari wanatawaliwa na watangayika baada ya kujikomboa kwa Sultani waswahili wamesema (ukiruka mkoyo utakanyaga mavi) ndio haya sasa cha kukila wanakitafuta stahili yao na serekali ya mapinduzi na hao waarabu walakula kuku OMAN.

...yakhe uloyasema wala hayahusu. Zanzibar na Pemba karne na karne inaendeshwa kwa mfumo wa kibiashara, kinachoikwamisha Zanzibar wala si serikali ya Tanganyika, bali ni fitna baina ya wazanzibari na wapemba wenyewe.

Ardhi ya Pemba imejaa rutba tosha, na kule ni mahodari wa kilimo, siasa chafu za kukomoana ndio zinazosababisha njaa na kudidimia uchumi visiwani humo. Iwapo kila Mpemba na Mzanzibari duniani kote wangewekeza 10% tu ya mapato yao kwa mwaka visiwani, wallahi leo hii visiwani humo ingekuwa kama Seychelles au Mauritius.

BTW leo ni mkesha, usiku kama leo miaka 45 iliyopita...
 
Back
Top Bottom