4000 waambukizwa Ukimwi Kinondoni ndani ya miezi mitatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

4000 waambukizwa Ukimwi Kinondoni ndani ya miezi mitatu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Dec 28, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  IMEDAIWA kuwa ndani ya miezi mitatu kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu watu wapatao 4072 wameambukizwa virusi vya ukimwi katika Manispaa ya Kionodnoni jijini Dar es Salaam

  Hayo yalijulikana baada ya kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Manispaa hiyo kutoa takwimu hiyo.

  Kati ya watu hao, 1,165 ni wanaume na 2,911 ni wanawake ambapo wote walipewa rufaa kwenda katika vituo vya kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU nchini.

  Katika taarifa iliyotolea na kamati hiyo imesema watu hao wataanza tiba ya huduma ya kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU na katika Manispaa hiyo kuna jumla ya vituo 17 vya kupata vidonge hivyo.

  Imesema kwa sasa katika vituo hivyo wameshafikia wagonjwa 12,829 ambao wamejiandikisha.

  Pia taarifa hiyo ilidai kuwa kwa sasa wagonjwa wanaotumia dawa hizo ARVs ni 7,033 huku wengine wakiendelea na huduma za uchunguzi na ufuatiliaji na endapo CD4 zitashuka chini ya 200 wataanzishiwa dawa.

  Source: www.Nifahamishe.com
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280
  Dahh.
  Lijigoma latisha..
  Sasa hizo takwimu za watu gani?
   
 3. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  takwimu za uongo hizo.....wamejuaje km hao watu wameupta ndani ya miezi hiyo

  au kipimo kinaonyesha upeupata lini?
   
Loading...