40% ya wateja wa Shirika la Ndege ( ATCL) ni wakazi wa Jiji la Mwanza

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
31,188
2,000
Hii taarifa inaonyesha jinsi jiji la Mwanza lilivyo na mchango mkubwa sana katika uchumi wa taifa.

Ni wakati sasa wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa zaidi katika jiji la Mwanza kwa faida kubwa ya taifa letu.

Ni hayo machache.

Maendeleo hayana vyama!
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
4,161
2,000
johnthebaptist,
Haiwezekani ndugu takwimu hizo kuwa kweli. Hii ilisemwa tu kumfurahisha mkuu. Huwezi kusema 40% ya abiria ni Mwanza je unataka kusema Dar ina abiria wachache kuliko mwanza? Dar peke yake ni zaidi ya 60%. Kilimanjaro haipungi 20%, Dodoma, Mbeya, Zanzibar, Bukoba, etc zipo wapi?
tuwe makini na wanaofanya kila kitu kumfurahisha rais.
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,325
2,000
Hii taarifa inaonyesha jinsi jiji la Mwanza lilivyo na mchango mkubwa sana katika uchumi wa taifa.

Ni wakati sasa wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa zaidi katika jiji la Mwanza kwa faida kubwa ya taifa letu.

Ni hayo machache.

Maendeleo hayana vyama!
Ili ATCL ipate soko, wameua Fastjet. Ili uwanja wa Songwe usishindane na huo wa Mwanza, wamegoma kuweka taa ili ndege zitue usiku au wakati wa ukungu. Wamegoma kuhakikisha jengo la abiria linakamilika. Bado kuna banda la muda tu.
Maendeleo hayana kanda!
 
Samson Ngomboli

JF-Expert Member
Oct 30, 2019
479
1,000
Hii taarifa inaonyesha jinsi jiji la Mwanza lilivyo na mchango mkubwa sana katika uchumi wa taifa.

Ni wakati sasa wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa zaidi katika jiji la Mwanza kwa faida kubwa ya taifa letu.

Ni hayo machache.

Maendeleo hayana vyama!
Vitu vingine tuwe tunachanganya za zetu,kwamba 60% pekee kwa mikoa yote ambako ATCL inaenda,Mambo ya awamu hii ni kujitoa ufahamu kumfurahisha mtawala.
 
Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
12,744
2,000
Ili ATCL ipate soko, wameua Fastjet. Ili uwanja wa Songwe usishindane na huo wa Mwanza, wamegoma kuweka taa ili ndege zitue usiku au wakati wa ukungu. Wamegoma kuhakikisha jengo la abiria linakamilika. Bado kuna banda la muda tu.
Maendeleo hayana kanda!
Mkuu kwan jengo la abiria la Mwanza limekamilika tayari?
Halafu kutokuwa na taa ndipo kunafanya abiria wa songwe wabadiri mawazo na kuja Mwanza
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,325
2,000
Mkuu kwan jengo la abiria la Mwanza limekamilika tayari?
Halafu kutokuwa na taa ndipo kunafanya abiria wa songwe wabadiri mawazo na kuja Mwanza
Abiria wengine convience yao ni usiku. Uwanja hauna taa. Ukiwa na taa abiria wataongezeka bila shaka
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,629
2,000
Hamjuamuelewa! Alisema katika route za ATCL hapa nchini 40% ya wateja wake wanatumia route ya Mwanza Airport. Na ni kweli kama ATCL wanaroute tatu kila siku kwenda na kurudi Mwanza na zinajaa na anasema wanataka waongeze route moja zaidi.
Amekosea kuelezea ndiyo maana watu wanashindwa kuelewa. Angesema hivi: Route ya Dar-Mwanza-Dar ndiyo yenye abiria wengi! Lakini yeye kasema ni wakazi wa Mwanza! Kwa nini asiseme ''route ya Dar-Mwanza, which make sense kwa sababu ndiyo majiji makubwa Tanzania ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom