40 days 2022/2023 road trip adventure around Tanzania

Mie pia ni generation landrover,. Nilianza na the by then icon 109, nimecheza nazo sana enzi hizo na kwa wakati huo niliamini kabisa hakukuwa na 4x4 ya uhakika kama landrover, i was wrong. Landrover zina matatizo madogo madogo mengi sana ,hasa leakages na suspension, bushes , ukitumia on personal issues huwezi jua , Ila nenda porini with a loaded landrover, halafu kule inyeshe kimvua ka cha buku hivi !!! on your return you'll face eye watering expensive repair bill.

Safari kama hizo mwenzie toyota , if it is a landcruiser , that will be a bonus .
Sawa mkuu nafikiri hili la gari tuwaachie waandaaji tuone watapendekeza lipimaana tutawfisha moyo na hili wazo nilizuri sana kwa watukufanya utalii wandani,kwa mimi usafiri kwabarabara kwangu ni zaidi yautalii.
 
Niwekee nafasi yangu mimi na pisi yoyote kali,iwe kali kweli kweli humu jf,nitamlipia huyo pisi nitakayempata
 
Mkuu Tz kubwa hii Iringa jimbo la Isimani ukivuka bwawa la Mtera kutokea Dodoma kwa mbele kama 40km kuna Migori pia na samak wa kutosha kutoka bwawani Mtera wazima unachagua wanakukaangia kitoga,kambale na perege
Mkuu umenigusa 😂😂😂
 
Mkuu watu wa Dodoma huwa wanaenda hapo wikend kula samak, mbuzi choma na vinywaji ni ka mji tu kapo road ya kwenda Iringa na lodge zipo so sometime mjini kuna boa unaibuka tu hapo
Napajua mkuu nilishiriki kujenga hilo bwawa ndio maana nikasema umenigusa nimekumbukambali sana aisee
 
Mkuu, jitolee V8 yako, tukishapanga route utaleta bajet ya mafuta, watakaoweza kuchangia kwenye V8 utawapata, ila njiani tutatembea convoy kwa speed 80, 50, 30kph.

Au tutakubaliana kusubiriana kwenye points tutakazo chaguwa, ili wenye V8 wa enjoy thrilling ya power with luxury.
nafikia muweke category wa 180, 150, 100, na 220.. wengine humu ndio raha yetu.. 80, 50 safari inakuwa ndefu sana
 
Muda wa safari umependekezwa kupunguzwa mkuu

Kwa kuanzia safari haitozidi wiki moja.

Na minimum bajet ya wiki moja ni laki 3 hivi

Tuendelee kupendwkeza route na kwa ajili ya kujuwa bajet

Karibu sana
Kama laki tatu, wadada 10 warembo wa jf najitolea kuwalipia.. asee 😊😊
 
Mkuu Tz kubwa hii Iringa jimbo la Isimani ukivuka bwawa la Mtera kutokea Dodoma kwa mbele kama 40km kuna Migori pia na samak wa kutosha kutoka bwawani Mtera wazima unachagua wanakukaangia kitoga,kambale na perege
Lakini mbona migori iliyoongelewa hapo kama sio ya mtera
Naifahamu kuna izazi migori na mtera though
 
Lakini mbona migori iliyoongelewa hapo kama sio ya mtera
Naifahamu kuna izazi migori na mtera though
Soma vizur kuna jamaa kasema Migor ipo Kenya nami nikamjibu kuna Migor nyingine ipo Iringa - Isiman kama inaitwa izazi sijui but jina maarufu pale ni Migori
 
Utaratibu wa kuchangia utakuwa wazi, maana bajeti ya mafuta itajulikana kabla ya safari, na hela itakayobaki ama kuzidi titaona waziwazi.

Kwenye matumizi binafsi hapa ndipo kila mtu atatumia kwa uwezo aliojipangia kwa safari hiyo.

Kwa mfan route hii:-

Dar - Lindi - Mtwara - Masasi - Mtambaswala - Masasi - Songea - Mbinga - Mbamba bay -Songea - Njombe - Iringa - Moro - Dar ni almost 2,800km

Kwa gari inayotumia lita moja kwenda km 8 maana yake zitahitajika lita 350 hivi ambazo kwa bei ya 2600 ni sawa na Shilingi laki 9.

Kwa gari moja ambalo limechukuwa watu sita ina maana kila mdau atachangia 150,000/- kwa ajili ya mafuta tu.

Route hiyo ili muifaidi inabidi kulala sehemu zifuatazo:-

Mtwara, Masasi baada ya kutoka Mtabaswala, Songea mjini, Mbamba bay, Njombe.

Hapo ni sehemu 5 za kulala ambazo kwa wastani wa lodge 15,000/- ni sawa na 75,000/-

Chakula kila siku ni wastani wa elfu 10, route ni siku 6 sawa na 60,000/-

Sasa chukuwa 150,000 + 75,000 + 60,000 = 285,000/-

Hivyo utaona angalau kila mtu asipungukiwe laki 3 kwa siku hizo sita.

Matumizi ya ziada kila mmoja anajuwa bajeti yake.

Kuitafuta laki 3 kwa miezi 6 inawezekana.


Tuendelee kuchaguwa ROUTE, IDADI YA SIKU kwa route hizo ili tufanye makadirio ya bajeti.
Sijaona ukielezea gaharama za matengenezo ya gari hapo.
 
Soma vizur kuna jamaa kasema Migor ipo Kenya nami nikamjibu kuna Migor nyingine ipo Iringa - Isiman kama inaitwa izazi sijui but jina maarufu pale ni Migori
Nimesoma vizuri mkuu , ninkweli kuna migori Tanzania , km 95 kabla ya kufika iringa mjini ukitokea dodoma , lakiji migori inayoongelewa na mtoa mada sio ya mtera , ni migori ya kenya , 30 km kutoka isebania na 30 km kabla ya kufika Rongo.

Ndo maana kasema mwanza musoma migori na kurudi watapitia Tarime ni exactly 300 km trip kama alivyoainisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom