40 days 2022/2023 road trip adventure around Tanzania

We nn yan 40 days 1.5M nitoke hivi hivi mkuu tumalizie kidimbwi
1.5m ilikuwa makadirio kwa route yote ya moja kwa moja kwa siku 40.

Baada ya kuonekana kuwa si wengi wenye fursa ya kuwa free kwa siku 40 ndipo wazo wa kugawa route likafuatia.

Kwa sababu sasa route zimegawanywa inakadiriwa kwa route inaweza kuwa laki 3 kama nyongeza basi ni kwa matumizi ya ziada kwa mhusika.

Lakini, bajeti halisi itajulikana wakati wa kupanga bajeti kwa route husika.
 
Check update post #1 or post #163
Nimeangalia updates
Lkn mbona kama unaifanya tour iwe ngumu, kwa nini unarudi rudi Dar ?
Naona kama kuna stress za kutaka kutembelea maeneo mengi kwa mpigo, nashauri labda hii tour iwe endelevu ili mwakani labda kuwe na lengo la kutembelea sehemu nyinginezo, nashauri labda uweke plan ya round trip kutokea Dar na hadi ukirudi Dar tour iwe inaishia .

Lets say Dar, lindi, Mtwara ,newala ,masasi mtambaswala ,Tunduru ,songea ,mbinga , mbamba bay , songea ,njombe ,makete kitulo , Tukuyu, kasumulu ,kyela , tukuyu mbeya, Tunduma, Sumbawanga, mpamda .....hapo mnapandisha hadi nyakanazi then kabanga boarder mnarudi rusumo boader then mnapandisha karagwe , kyaka hadi mutukula , then mkitoka mutukula ,mnarudia bukoba , muleba hadi kyamirorwa chato ,mwanza bunda ,musoma , Tarime ,sirari, mnarudi tena bunda na kukatisha Serengeti hadi Arusha , Arusha, Mombo, lushoto, Tanga mjini , Pangani , saadani hadi bagamoyo then Dar .

Utaona kuwa hii trip lengo liwe ni kuzunnguka pembezoni mwa Tamzania , then unaeza arrange trip nyingine mwakani ikiwa na lengo la kutembea Tanzania kati kati .
Tanzania ni nchi kubwa sana , huwezi kuitembea yote kwa mara moja utachoka sana , uzuri nchi nzima siku hizi ipo well connected na barabara za uhakika

Nashauri trips kama hizi mkitoka dar mmetoka !! Mkirudi na tour imekwisha .
 
Lengo la kuizunguka Tz ili wadau wapate kuijua Tz yao, angalau kwa kuanzia, kisha trip nyingine tuvuke mipaka
Wazo zuri, kwa wapenda Adventure tumekuelewa sana.

Ila mkuu roadtrip ikiwa ndefu sana inachosha balaa.

Nimewahi kufanya kitu kama hiyo ilikuwa siku 10 tu ila wadau walikuwa hoi hoi...maybe kwa msimu huu ambapo barabara zimeboreshwa.
 
40 Days 2022/2023 adventure around Tanzania main land.

1. Gari ipo, Land Rover Defender 110 / 2016 Station Wagon kama hiyo hapo chini ila rangi tofauti.

2. Wanao hitajika ni wadau watano (5), wanawake watatu (3) na wanaume wawili (2) na mimi mwenyewe jumla tuwe watu sita (6).

3. Wakijitokeza watu wengi zaidi utaratibu wa kupata (ma)gari (me)ngine utafanyika.

4. Tutatembea zaidi ya kilomita 6,000 kwa siku 32, siku 8 zitapotelea katikati kadri tutakavyo amua.

5. Makadirio ya gharama ya mafuta ni 1.8M hadi 2m.

6. Mchango kwa kila mdau itahitajika 1.5m ambayo itagharamia mafuta, chakula, malazi na utalii.

7. Mchango haukusanywi bali kila mmoja ajiwekee akiba benki au popote pale kuanzia sasa hadi mwezi October 2022 panapo majaaliwa ambapo tutafanya kikao na kupanga safari yetu, lengo liwe hadi kufikia 5 Disemba 2022 tuwe tumemaliza mzunguko wetu.

Mawazo chanya, yanakaribishwa, kuhusu Route, gharama, usahihi wa umbali, usalama, nk.

8. Mapendekezo yangu ya route iwe ni kuzunguka pembezoni mwa Tanzania kama ifuatavyo:-

Day 1
Dar - Lindi - Mtwara, almost 600km.

Day 2
Mtwara - Masasi - Mtambaswala, almost 320km.

Day 3
Mtambaswala - Masasi - Songea, almost 500km.

Day 4
Songea - Mbinga - Mbamba bay, almost 180km.

Day 5
Mbamba bay - Songea - Njombe, almost 420km.

Day 6
Njombe - Makete (via Kitulo) - Mbeya, almost 170km.

Day 7
Mbeya - Kasumulu, almost 120km.

Day 8
Kasumulu - Mbeya Tunduma, almost 230km

Day 9
Tunduma - Sumbawanga - Kasanga, almost 350km

Day 10
Kasanga - Sumbawanga - Muze - Lake Rukwa, almost 180k.

Day 11
Lake Rukwa - Muze - Namanyele - Kibaoni - Majimoto, almost 180km.

Day 12
Majimoto - Kibaoni - Stalike - Mpanda, almost 150km

Day 13
Mpanda - Uvinza - Kigoma town, almost 320km.

Day 14
Kigoma - Kasulu - Nyakanazi, almost 350km

Day 15
Nyakanazi - Lusahunga - Nyakahura - Kobero border, almost 150km.

Day 16
Kobero border - Nyamiyaga - Rusumo border, almost 70km.

Day 17
Rusuma - Nyakasanza - Mtukula, almost 250km.

Day 18
Mtukula - Bukoba town, almost 90km.

Day 19
Bukoba - Biharamuro - Geita - Mwanza, almost 450km.

Day 20
Mwanza - Bunda - Musoma - Migori, almost 300km.

Day 21, 22, 23, 24
Migori - Tarime - Serengeti, almost 200km + other 200km.

Day 25, 26
Serengeti - Ngorongoro, almost 70km + 200km.

Day 27, 28
Ngorongoro - Karatu - Arusha, almost 200km.

Day 29
Arusha - Segera - Tanga - Horohoro, almost 550km

Day 30
Horohoro - Tanga town, almost 70km + 50km.

Day 31
Tanga - Pangani - Sadani, almost 200km.

Day 32
Sadani - Bagamoyo - Dar es Salaam, almost 180k.

Karibuni kwa mawazo chanya.

___________


Updated

(a) Safari zitagawanywa kwa “5days to 8days trip” kwa kuzingatia "route" yenyewe.

(b) Idadi ya wadau watakao jitokeza itaamua gari gani na gari ngapi zitumike.

(c) Wenye gari binafsi wanakaribishwa kwenye msafara, wakipenda kuchukuwa baadhi ya wadau kwa kuchangia mafuta pia itaruhusiwa, gari ziwe zenye uwezo wa kupita njia zenye changamoto (rough roads, mud roads, sandy roads) – itazingatiwa kwenye route husika.

(d) Familia zinaruhusia kushiriki, ili mradi kila mshiriki awe ametimiza miaka 18 na kuendelea

(e) Panapo majaaliwa tarehe 15 Feb 2022 tutaanza kujiorodhesha kwa wale walioazimia kisha kupanga bajeti kwa kila route itakavyo kubaliwa.

(f) Matarajio ya safari ni July 2022 au Nov 2022 kadri wadau watakavyo amua wenyewe.

(g) Makadirio ya kilomita yamezingatia pia "idling time", mizunguko ya mchepuko, na michepuko ya kitalii, Lakini kama kuna sehemu kilomita zimekosewa sana turekebishe kwa maana ndizo zitakazo tuongoza kwenye bajeti ya mafuta.

(h) Katika mapendekezo ya "route' inawezekana kukawa na route muhimu imesahaulika, basi TUPENDEKEZE, Mapendekezo ya awali ya mgawanyo wa "route" ni kama ifuatavyo:-

1st route.
Dar – Lindi – Mtwara (day 1 = 600km)

Mtwara – Masasi – Mtambaswala – Masasi (day 2 = 450km)

Masasi – Songea (day 3 = 400km)
Songea – Mbinga – Mbamba bay (day 4 = 180km)

Mbamba bay – Songea – Makambako (day 5 = 500km)

Makambako – Iringa – Morogoro – Dar (day 6 = 650km)

{Makadirio jumla ni kilomita 2,800}

2nd route.
Dar – Makambako –Tunduma (day 1 = 950km)

Tunduma – Ileje – Kasumulu (day 2 = 250km)

Kasumulu – Tukuyu – Makete (day 2 & day 3 = 170km + 50km)

Makete – Njombe - Iringa – Dar (day 4 = 830km)

{Makadirio jumla ni kilomita 2,250}

3rd route.
Dar – Mikumi (day 1 = 300km + 100km)

Mikumi – Mbeya (day 2 = 550km)

Mbeya – Tunduma – Sumbawanga (day 3 = 350km)

Sumbawanga – Kasanga – Namanyele – Kibaoni – Majimoto (day 4 = 350km)

Majimoto – Lake Rukwa – Muze – Sumbawanga (day 5 = 160km)

Sumbawanga – Mbeya – Morogoro (day 6 = 960km)

Morogoro – Dar (day 7 = 200km)

{Makadirio jumla ni kilomita 3,000}

4th route.
Dar – Dodoma – Manyoni – Itigi – Tabora (day 1 = 850km)

Tabora – Sikonge – Ipole – Makongolosi – Chunya (day 2 = 550km)

Chunya – Mbeya – Mlowo (day 3 = 140km)

Mlowo – Mtowisa –Muze (day 4 = 280km)

Muze – Ntendo – Chala – Mashete – Kisi – Mpanda (day 5 = 300km)

Mpanda – Inyonga – Ipole – Tabora (day 6 = 300km)

Tabora – Nzega – Singida – Dodoma (day 7 = 580km)

Dodoma – Dar (day 8 = 450km

{Makadirio jumla ni kilomita 3,200}

5th route.
Dar – Dodoma – Iringa (day 1 = 750km)

Iringa – Mbeya – Chunya (day 2 = 420km)

Chunya – Rungwa – Itigi (day 3 = 450km)

Itigi – Tabora – Ipole – Inyonga – Mpanda (day 4 = 450km)

Mpanda – Uvinza – Kigoma town (day 5 = 320km)

Kigoma – Tabora – Itigi – Manyoni (day 6 = 700km)

Manyoni – Dodoma – Dar (day 7 = 600km)

{Makadirio jumla ni kilomita 3,700}

6th route.
Dar – Singida (day 1 = 700km)

Singida – Kahama (day 2 = 300km)

Kahama – Nyakanazi – Kibondo – Kasulu – Kigoma (day 3 = 550km)

Kigoma – Kobero border – Rusumo border (day 4 = 520km)

Rusumo – Singida (day 5 = 600km)

Singida – Babati – Kondoa – Dodoma (day 6 = 240km)

Dodoma – Dar (day 7 = 450km)

{Makadirio jumla ni kilomita 3,400}

7th route.
Dar – Sadani (day 1 = 180km + 50km)

Sadani – Pangani – Tanga (day 2 = 200km )

Tanga – Horohoro – Tanga –Korogwe (day 3 = 250km)

Korogwe – Arusha – Karatu (day 4 = 490km)

Karatu – Ngorongoro – Karatu - Arusha (day 5, day 6 = 340km)

Arusha – Segera – Msata – Bagamoyo – Dar (day 7 = 650km)

{Makadirio jumla ni kilomita 2,200}

8th route.
Dar – Kahama (day 1 = 900km)

Kahama – Bukoba – Mtukula (day 2 = 480km)

Mtukula - Bukoba – Biharamula – Geita – Mwanza (day 3 = 510km )

Mwanza – Musoma – Sirari (day 4 = 300km )

Sirari - Tarime – Serengeti (day 5, day 6 = 120km + 100km)

Serengeti – Karatu – Arusha (day 7 = 400km)

Arusha – Chalinze – Dar (day 8 = 650km)
{Makadirio jumla ni kilomita 3,500}

#Tuhakiki umbali (kilomita)
#Tuanishe route muhimu zilizo sahaulika
#Tupeane maangalizo ama mambo ya kuzingatia kwa ajili ya usalama
#Mengineyo

Karibuni.

___________
JBourne59
Una familia? Je unalipa school fees za watoto kama unao?
 
sijaona budget ya matairi ya gari husika, kwa kuongezea siku 40 nyingi na umeweka hizo kilometers none stop yaani day 1,2,3,4 mpaka mwisho....hampumziki?! kama sio mzoefu wa safari lazima mtu azime hapo..

mwisho kwanini opposite sex safarini tena kwa idadi ya kuwiana..
 
Gari siyo yangu ila ya jamaa yangu ambaye hana shida nami, nimemuumiza amesema ni Defender ya 2016, startech sixty eight.

Siyo lazima iwe siku 40 mfululizo

Na kuhusu bajeti siyo kihivyo kama ukianza kuchanga kuanzia Jan

Kila mtu atatumia hela zake, bajeti iliyotajwa na makadirio tu hiyo labda kwenye kuchangia mafuta ambapo napo tutachanga kila tunapojaza full tank labda au kadri wadau watakavyo amua
Huyo jamaa yako kama sio utoto basi hajielewi au huenda bado wote ni wageni kwenye vyombo vya moto. Hiyo kitu ya kwamba mtatumia gari yake na hana tatizo inaashiria bado hamjielewi (wenyeji wa magari watanielewa,wageni wa magari kama wewe hawatanielewa).
Nasisitiza kama mnaplan kweli tafuteni gari ya kukodi na muiwekee bajeti
 
Siyo lazima kila mdau atumie siku zote hizo...

Suala la mimba nimecheka sana, lakini kimsingi watu watakuwa na maamuzi yao wenyewe juu ya miili yao.

Route zimegawanyika, maximum days per route ni 8days

Check update post #1 ama post #163
Good idea, haswa kwa wale wanaotumia 356 days sehemu moja. Kuna madhali nzuri sanaaaa!! outside your comfort zone.
 
Huyo jamaa yako kama sio utoto basi hajielewi au huenda bado wote ni wageni kwenye vyombo vya moto. Hiyo kitu ya kwamba mtatumia gari yake na hana tatizo inaashiria bado hamjielewi (wenyeji wa magari watanielewa,wageni wa magari kama wewe hawatanielewa).
Nasisitiza kama mnaplan kweli tafuteni gari ya kukodi na muiwekee bajeti
Siyo utoto,
Its just a matter of adventure!,

Na siyo wageni kwenye vyombo vya moto, binafsi nilinunua gari yangu ya kwanza peugeot 504 GL pickup miaka ya 1980's jamaa yangu yeye alitangulia kabla yangu na kipisi cha 108 Landrover.

Sadaka hutolewa kwa namna mbalimbali moja wapo ni kama hivyo...

Jamaa yangu ni mkongwe kwenye magari kuliko mimi, yeye ni "teja" wa magari ya UK.

Sisi wote ni wastaafu (mie na jamaa yangu), so tunajielewa vizuri tu, tunafurahia maisha baada ya kutumikia nchi kwa muda mrefu na uliotukuka.

Get 60yrs old and you will understand the meaning ya kufurahia maisha.

Hata hivyo tumepewa ushauri kwa kutumia off-road cars za kijapani.

Na ushauri wako wa kukodi gari utazingatiwa, hata toyota coaster ikibidi ili mradi kuwe na vibe la pamoja bila kujali rika ingawaje above 18yrs itazingawa.
 
Siyo utoto,
Its just a matter of adventure!,

Na siyo wageni kwenye vyombo vya moto, binafsi nilinunua gari yangu ya kwanza peugeot 504 GL pickup miaka ya 1980's jamaa yangu yeye alitangulia kabla yangu na kipisi cha 108 Landrover.

Sadaka hutolewa kwa namna mbalimbali moja wapo ni kama hivyo...

Jamaa yangu ni mkongwe kwenye magari kuliko mimi, yeye ni "teja" wa magari ya UK.

Sisi wote ni wastaafu (mie na ama yangu), so tunajielewa vizuri tu, tunafurahia maisha baada ya kutumikia nchi kwa muda mrefu na uliotukuka.

Get 60yrs old and you will understand the meaning ya kufurahia maisha.

Hata hivyo tumepewa ushauri kwa kutumia off-road cars za kijapani.

Na ushauri wako wa kukodi gari utazingatiwa, hata toyota coaster ikibidi ili mradi kuwe na vibe la pamoja bila kujali rika ingawaje above 18yrs itazingawa.
Ok mkuu kwa umri huo inawezekana kwakua tayari mmeshapitia mengi na hamna jipya. Nilidhani ni rika letu hili la kati ambapo urafiki kwa kiasi kikubwa si urafiki wa kweli bali ushkaji tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom