4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,100
18,333
Kuna hoja nimekuta watu wanaongea, ni kuhusu kile ambacho mama amesema waziri wa fedha akakae na mwenzake wajadili na kusuluhisha katika kero za muungano. Ninaupenda sana Muungano,ninauunga mkono. lakini, nilijiuliza kitu kimoja, mimi kama mtu wa bara sitaki tupigwe pia kama wazenji wasivyopenda kupigwa.

1. hivi Zanzibar inachangia kitu gani kwenye kwa Tz bara kinachowastahilisha tuwagawie hiyo asilimia? Bara inafaidika nini toka Zanzibar?

2. Mgao unaoongelewa ni wa misaada toka nje, au ni mapato ya nchi (pato la madini bara, TRA, navitu vyote vya bara)?

3. kama ni mapato ya nchi, kwani TRA haipo Zanzibar ya kikwaokwao?

4. proportion ya wingi wa watu + ukubwa wa eneo vinazingatiwaje wakati wa kugawa pato ya muungano?

5. kwanini marais waliopita walikuwa hawashughulikii hilo jambo, kulikuwa na kitu gani walichokiona? including one of them who was Zanzibari.

6. kwa anayeelewa, naomba anieleweshe hili jambo kwasababu kama vile tu zanji wasivyopenda kupigwa, mimi kama mtu wa bara pia sipendi na sikubali.

Naongea hivi kwasababu watu wanavyoongea mtaani wanaongea kama vile kwasababu mama ni mzanzibar basi wanaona wazanzibar wanaweza kupitisha vitu vingi sana ambavo vilikuwa havipiti kwa awamu za nyuma ambazo nyingi hazikushikwa na rais wa zanzibar.

MWISHO: siongei kwa ubaya, wala kwa unafiki, ila ninaongea kinachoongelewa mitaani. Ninamwamini mama atafanya makubwa. Ila naamini tunatakiwa kuwa na busara ya hali ya juu kwasababu kuna mambo tunaweza kufanya tukifikiri tunajenga muungano kumbe ndio tunauweka kwenye mazingira ya kubomoka kabisa.
 
Kwani Pwani inapata mgao kiasi gani? bila kusahau Chato
watu tunataka kujua, hicho kinachotakiwa kugawanywa ni kitu gani kilichokuwa kimeshikilia muungano miaka yote hiyo hakifanywi? kikifanywa kwa uwazi kitadumu, kisipofanywa kwa uwazi ni bomu litakalolipuka siku moja litusumbue tena.

bara wanafaidikaje na zenji kimapato, na zenji wanafaidikaje na bara kimapato? what are our common interest zinazotuunganisha (zaidi ya undugu ambao weusi wengi wa zenji wametoka huku na wao wapo wengi sana bara wanamiliki biashara, ardhi na maisha). kama hujui acha kujibu hii mada.
 
Halafu huyu mama sometimes naona amekuja kutuchanganya tu, hii huruma anayoiweka mbele badala ya kutumia akili atatuumiza, hao wazanzibar wenzake wana bunge, mahakama, serikali, jeshi, kuonesha kwamba wana mamlaka wanajitegemea, sasa hii kuwabeba beba mara umeme, bado tuwagawie 4% maana yake nini?
 
Halafu huyu mama naona amekuja kutuchanganya
Hajaja kutuchanganya, anaonyesha matumaini makubwa sana. hoja hapa ni wasije kuja watu wakutake advantage upole wake, wakaingiza vitu vya ajabu kwenye muungano. kama kuna hoja ya msingi binafsi mimi sina shida, ila napenda mwenye kuelewa zaidi atuambie, ni mapato yepi?

Yanainclude na mapato ya migodi ya bunzwagi geita na bulli? na ya TRA ya bara? au ni pesa za misaada pekee? na je, zanzibar wana TRA yao au hawana? wanaendesha nchi kwa pesa ipi? si wanajitegemea? au? sasa sisi tuwachangie kwa ajili gani?
 
Wazanzibari walishaturahisishia Watanganyika baada ya kugunduliwa kuwa wanayo hazina kubwa ya mafuta baharini. Hapo ndipo na wapenda Wazanzibari kwa kusimamia maslahi yao kwa ukweli. Walisema, utafiti wa mafuta na mafuta yenyewe haya husu Muungano wetu" Watanganyika wao ni copy and paste tu ya huu msimamo wa ndugu zetu.

Itakuwaje pato la dhahabu au Tanzanite liwe la muungano? Mh Mpango usituangushe katika hili. Hii 4% ni kero ya Muungano tena kubwa iondolewe.

Kuwe na kuchangia gharama za Muungano kwa uwiano unaoeleweka. Ikitokea mbia mmoja anashindwa kutimiza wajibu wake mahisabu ya wekwe na kutuzwa kama yale ya Tanesco na Zesco ila kusitokee kusamehewa. Bali kuchukuliwe fidia kama China walivyo miliki uwanja wa ndege Zambia na bandari Sirilanka.
 
Kwenye Katiba kumeainisha vitu ambavyo ni vya muungano na vingine sio vya muungano, mfano mafuta na gesi au madini, wazanzibari wanadeka sana na huyu mwenzao kaja naona ndio ameamua kuwabeba muda sio mrefu atatuletea habari za Chato nyingine.

Huu muungano sio koti alisema Karume, kuendelea nao ni kujiumiza vichwa bure, hao marais wenyewe wanatoka Zanzibar kuja kututawala bara, kwanini siku nyingine asitoke Rais bara akatawale Zanzibar?
 
Wazanzibari walishaturahisishia Watanganyika baada ya kugunduliwa kuwa wanayo hazina kubwa ya mafuta baharini. Hapo ndipo na wapenda Wazanzibari kwa kusimamia maslahi yao kwa ukweli. Walisema, utafiti wa mafuta na mafuta yenyewe haya husu Muungano wetu" Watanganyika wao ni copy and paste ya huu msimamo wa ndugu zetu.

Itakuwaje pato la dhahabu au Tanzanite liwe la muungano? Mh Mpango usituangushe katika hili.
unfortunately, amini usiamini, mafuta zenji hakuna. na kama yapo, yapo kidogo sana, na kama yakiwepo zenji basi na bara yapo. hata gesi tu hawajagundua. binafsi, ninaamini kama tunataka muungano, tuungane kabisa kabisa tuwe nchi moja, hata hoja ya kuwa na marais wawili kwenye nchi moja hii huwa naona ni ukakasi.

ila kama kweli kuna mafuta zanzibar, ni haki wayatumie wao tu, na sisi gas na mafuta na helium etc zitumike huku tu. Zanzibar kama wakipata mafuta kweli wataendelea sana, kama wakipata kitu cha kuwaingizia hela wataendelea sana kwasababu nchi yao ni ndogo kuiendeleza ni rahisi. hata hivyo.

wamejaa sana bara na ninapenda wajae zaidi ndio maana ya muungano, ila sisi sasa kwenda kwao tunaonekana wageni fulani hivi. tukija ndani ya hoja, ni kitu gani hiki kinachotakiwa kugawanywa? isije kuwa wana hoja ya msingi halafu inafunikwa.
 
Hajaja kutuchanganya, anaonyesha matumaini makubwa sana. hoja hapa ni wasije kuja watu wakutake advantage upole wake, wakaingiza vitu vya ajabu kwenye muungano. kama kuna hoja ya msingi binafsi mimi sina shida, ila napenda mwenye kuelewa zaidi atuambie, ni mapato yepi? yanainclude na mapato ya migodi ya bunzwagi geita na bulli? na ya TRA ya bara? au ni pesa za misaada pekee? na je, zanzibar wana TRA yao au hawana? wanaendesha nchi kwa pesa ipi? si wanajitegemea? au? sasa sisi tuwachangie kwa ajili gani?
Sio suala la upole hapa inatakiwa itumike akili kuamua mambo sio mahaba kwa sababu unatokea huko, hao watu wata take advantage kwasababu yeye mwenyewe ameamua kuacha watu wamsaidie kufikiri, serikali yake tayari imeshaamua baadhi ya mambo lakini utekelezaji wake bado umekuwa mgumu, mfano suala la vifurushi vya simu, kwa anaejielewa ataona huyu Rais bado haja-fit hiyo position ipasavyo, na wala msimtetee hakupata nafasi ya kujiandaa.
 
Kabla ya Muungano kulikuwa na nchi mbili huru, Znz na Tanganyika. Ishu ya mgao sijaelewa mantiki yake naomba maelezo.
China wana 'One country, two systems', sheria za Hongkong na China mainland ni tofauti KABISA! hii ingetufaa sana sisi pia. nawasilisha wazo
 
unfortunately, amini usiamini, mafuta zenji hakuna. na kama yapo, yapo kidogo sana, na kama yakiwepo zenji basi na bara yapo. hata gesi tu hawajagundua. binafsi, ninaamini kama tunataka muungano...
Kwa namna ulivyouelezea muungano vyema kabisa, ni wazi kabisa mfumo huu uliopo unainufaisha chama tawala zaidi ya nchi na raia wake.

Ile hoja ya CHADEMA aliyokuwa akiipigia debe Lissu kwenye chaguzi ya mwisho ilikuwa safi sana yenye afya kwa maendeleo ya nchi na raia wake.

Tatizo ni uwezo mdogo wa kufikiri walionao asilimia kubwa ya raia wetu, wanadanganywa eti 'itavuruga amani' sijui na upuuzi gani mwingine
 
Hajaja kutuchanganya, anaonyesha matumaini makubwa sana. hoja hapa ni wasije kuja watu wakutake advantage upole wake, wakaingiza vitu vya ajabu kwenye muungano. kama kuna hoja ya msingi binafsi mimi sina shida, ila napenda mwenye kuelewa zaidi atuambie, ni mapato yepi? yanainclude na mapato ya migodi ya bunzwagi geita na bulli? na ya TRA ya bara? au ni pesa za misaada pekee? na je, zanzibar wana TRA yao au hawana? wanaendesha nchi kwa pesa ipi? si wanajitegemea? au? sasa sisi tuwachangie kwa ajili gani?
Binafsi sina shida kama hiyo 4% itahusisha mapato na madeni. Kama ni mapato tu, hapo kuna tatizo.
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom