3D bongo muvie

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,043
21,517
hivi wakuu mnadhani ni lini na hapa kwetu tutaanza kuangalia muvi za 3d zilitongenezwa hapa hapa kwe2? halaf pia kuhusu muvi za animation. hapa kuna magwiji wa 3d modelling, watu wanajua lightwave na ma 3ds max yakutosha but stil ha2apply knowledge zetu. mnaonaje wakuu?
 
Mbona una taka kutembea bila kutambaa kwanza?, eti 3D movie , unafurahisha, uliza kwanz aje lini tutaanz akushot ovies kwnye Film, na sio hizi home made video za kina Kanumba?
 
Mtoto wa Kishua umeniwahi, ila ukweli ndio huo. Bado Wabongo hatujaanza kutengenza filamu (movie in that sense), zilizopo ni 'video'.

Kwa hiyo tukianza kufanya filamu then 3D films pia zitakuja.

Kitu kingine muhimu cha kufahamu ni kuwa, animation ya kwenye movies nyingi za wenzetu hazifanya kwa kutumia off-the-self programs kama ulizotaja. Kila filamu ina mahitaji yake, kwa hiyo watu wanafanya custom programs ili kutimiza malengo yao (script whatever).
 
wakuu ni mtazamo tu ila nimefurahishwa na michango yenu. mi nafkiri kinachokwamisha ni budget. utaskia m2 ana tumilion tutano kashatoa muvi
 
Mtoto wa Kishua na Gurta..kilichopo Tanzania ni michezo ya kuigiza nafikiri hata kuitwa video bado...maana angalia hizo mnazoita ''video'' za kibongo eti unaweza kukuta inaishia mtu anakunywa chai au anacheka...no lesson etc
 
Hii inastahili kuwekwa kule kwenye jokes,it serves the purpose of making one laugh.
 
hivi wakuu mnadhani ni lini na hapa kwetu tutaanza kuangalia muvi za 3d zilitongenezwa hapa hapa kwe2? halaf pia kuhusu muvi za animation. hapa kuna magwiji wa 3d modelling, watu wanajua lightwave na ma 3ds max yakutosha but stil ha2apply knowledge zetu. mnaonaje wakuu?

Wewe na wataalam wengine wa graphics naomba niwaulize sababu siku za karibuni nimekuwa nina interest na mambo ya graphic. na ubaya au uzuri napenda kujaribukwa vitendo

Maswali

  1. Je nikitaka kuiweka hiyo avatar yako hapo kwenye 3D nitahitaji nyenzo gani na itanichukua muda gani na hatua gani zitaniwezesha kufikia malengo yangu ?
  2. Kutengeza carton movie ya kiswhaili ama ya zile hadithi za kiswahili tulizosoma zamani kama ya sungura eg sizitaki mbichi hizi inahitaji shilingi ngapi?
 
Mimi ni mpenzi wa 3D, ingawa najaribu tu kujifunza mwenyewe kwa kusoma tutorials na kutumia sources zingine. nashauri badala ya kukatishana tamaa tuangalie uwezekano wa kushirikiana ili kufikia lengo la kupiga hatua katika fani hii. Ningefurahi sana kama ningeweza kukutana na hao magwiji wa 3d ili nipate niweze kuvuna maujuzi yao. Cha msingi ni kwamba tushieikiane tusinyimane ujuzi, maana tatizo lingimne la wabong ni kwamba mtu akishajua kitu basi hataki wengine wajue ili awe peke yake, wanasahu kwamba hata project hazifanywi na mtu mmoja ni teamwork. Sikatishi tamaa na ninamshukuru mzeewaloliondo kwa kuleta mada hii.
 
u0u0g.jpg


Bajeti $150 million

LCV7m.jpg

Bajeti: $200 million

Bajeti ya elimu Tanzania $400 million.
So hakuna economic sense ya kutengeneza movie kwa kiwango hiki Bongo kwa sasa, hauwezi ukarudisha hela, labda tufanye short story ambazo ni za kujifurahisha na kukuza jina kama hizi zimetengenezwa Zimbabwe na Korea ila sijui wazim wanahusika kiasi gani.
Jungle Beat from [url]www.junglebeat.tv - YouTube[/URL]
 
naomba niulize....hivi ukitaka kuona hizo 3D moviez si lazima uwe na TV inayosupport.......na je hapa bongo itakuwa inauzwa sh ngapi?.....nimeuliza tu....
 
<font color="#800080"><font size="4"><span style="font-family: comic sans ms">naomba niulize....hivi ukitaka kuona hizo 3D moviez si lazima uwe na TV inayosupport.......na je hapa bongo itakuwa inauzwa sh ngapi?.....nimeuliza tu....</span></font></font>

Usisahau na miwani yake
 
naomba niulize....hivi ukitaka kuona hizo 3D moviez si lazima uwe na TV inayosupport.......na je hapa bongo itakuwa inauzwa sh ngapi?.....nimeuliza tu....

Kuiona 3D movie in 3D lazima uwe na TV inayosupport na movie yenyewe inabidi iwe imetengenezwa ionekane in 3D ila kuiona movi ya 3D Animation in 2D hauhitaji kitu chochote special kama hiyo youtube clip hapo juu ni 3D animation lakini iko kwenye 2D format, kwa hiyo hapa tunaongelea zaidi 3D kama technique ya animation kuliko kuona kitu in 3D.
 
Kama unataka kuangalia video za 3D nunua HTC EVO 3D,LG OPTIMUS 3D,shoot ur own videos na utaenjoy! I dnt evn want to get started with us making 3D Movies....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom