34,030 Euro kwa mtandao wa kuanika wala rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

34,030 Euro kwa mtandao wa kuanika wala rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, May 27, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,508
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  Mafisadi waumbuka, sasa kuanikwa kwenye mtandao

  Wednesday, May 27, 2009 11:20 AM

  MBINU mpya imegundulika ya kuwataja mafisadi ili waweze kujulikana na na wataanikwa kwenye mtandao wa mawasiliano duniani kote.

  Utekelezaji wa kuwaanika mafisadi hao wanaotuhumiwa ama kushitakiwa ulizinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

  Katika kutekeleza mradi huo tayari nchi mbili za Bara Ulaya ambazo ni Finland na Switzerland zimeshatoa mabilioni kiasi cha Euro 34,030 ili kuweza kutekeleza adhma hiyo.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [Takukuru] Dk. Edward Hoseah amethibitisha kutolewa kwa mabilioni hayo kwa ajili ya kufadhili mradi huo.

  Fedha hizo zilitolewa na asasi ya Agenda Participation 2000 [AP2000] itakayoratibu na kusimamia mradi huo.

  Mtandao huo wa kisasa utatoa taarifa kwa Umma zinazohusu mashauri yanayodaiwa na yaliyothibitishwa kuhusu rushwa ili kuongeza uwajibikaji katika vita dhidi ya rushwa nchini.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo zilisema kuwa lengo kuu la mradi huo wa kuwaanika mafisadi ni kuweka kumbukumbu za watuhumiwa na wahusika wa tuhuma hizo.

  Pia kuongeza kiasi cha uwazi katika mashauri hayo ili raia waweze kutambua na kuwekwa wazi kuhusu ufisadi wa wahusika.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wakitajwa katika mtandao what next? Wametajwa magazetini, redioni, kwenye luninga lakini no action talk only ( NATO ). Nani ni muwajibikaji mkubwa katika vita ya rushwa PCCB au wananchi nadhani ni PCCB, in which case kama hawajibiki sawasawa hatuhitaji foreign donors kutoa fedha kwa ajili ya hilo bali ni wao kuwajibishwa.
   
 3. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  why the long route......watanzania wangapi wana access na mitandao??? wanataka tu kulefusha zoezi hili mpaka hapo watakaporudi tena madarkani.
  la maana ni kutafuta mkakati wa ku-speed up kesi zote za ufisadi na kuongeza uwazi katika vita ya ufisadi...hao PCCB na DPP wamekuwa hawatoi ushirikiano na public media katika hili, haiwezekani file la kagoda asitokee mtu wa kulizungumzia na kutoa hatima yake....wasitucheze shere....
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,508
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280


  Katika kutekeleza mradi huo tayari nchi mbili za Bara Ulaya ambazo ni Finland na Switzerland zimeshatoa mabilioni kiasi cha Euro 34,030 ili kuweza kutekeleza adhma hiyo.

  mabilioni kiasi cha Euro 34,030 --HAPO NDIPO SHUGULI INAPOAANZA
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kimeo kingine hicho!!!!! Eti kuwataja mtandaoni!!! ambapo si watu wote wenye access ya mtandao.

  Tuliwataja kwenye TV na magazeti at least audience ni kubwa hakuna impact katika utekelezaji. Unajua wanataka kuongea politics ili mataifa waone kuwa Tz wako serious kupambana na Rushwa na ufisadi kumbe ni usanii na fix tu.

  Jana niliangalia TV yule mkurugenzi wa Kupambana na Ruswa (Idara) alipotamka kupambana na ufisadi alisita kidogo kutaja ufisadi, yaani kama anajitafuna vile!!!!

  Tunataka mtu kama Mengi ambaye anataja na kutamka ufisadi bila kumumunya na kupata kigugumizi za maneno. Hakuna kitu hapo, hela ya Donors inapotea bure. Leteni hizo hela zihudumie kuboresha shule zetu (hasa msingi na sekondari).

  Aliyeangalia ripoti maalum ITV jana atakubaliana na mimi kuwa shule hazina madarasa ya kutosha, yaliyopo ni mabovu nyufa kibao, waalimu ni wawili kwa say wanafunzi 300 na nyingine ina 700.

  Tatizo hatuongozwi na priority, ni usanii na kutaka fuata upepo.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kichwa cha bandiko kinatasfirika "Mengi anaweza kumchunguza RA na wenzake"
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Asante moods mmesaidia kuweka heading sawa. Maana heading ya awali ilikuwa inapoteza mwelekea kidogo. Kudos.
   
 8. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mbona mtandao wa kuanika wala rushwa upo? JF so to say, ndio kusema hawajauona huu mtandao au hawaujui?
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mbona tushawataja humu??? ina maana hawaoni siku hizi??
  najua huo mtandao ambao unadhaminiwa kwa nia njema na wahisani ila wakubwa wetu watautumia kwa nia nyingine yaani kuwa na data yakinifu za vimbelembele woote watakaothubutu kupost humo.

  Ila shime wadau tuendeleze mapambano dhidi ya Rushwa.
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Maxence Melo,
  Labda na sisi JF tuombe EU msaada wa hizo pesa na JF ianze kutangazwa kama chombo cha kupigana na UFISADI. JF pia inaweza kuchukua lengo la kutangaza habari kwa Watanzania katika maeneo tofauti kwa kuweka computers walau wilaya zote ambazo hazina computer/internet. Hii kama ikiandikwa vizuri, inaweza kabisa kukubalika ndani ya EU na huo msaada ukaja na mwisho wa siku JF ikaanza kupanua makucha yake.

  Mwaka jana kuna jamaa fulani walijaribu kufanya kitu kama hicho na lengo lilikuwa baadaye waje washirikiane na JF kama itawezekana. Sema tu walikwama kupewa hizo hela. Mwakani wanataka wajaribu waingie kwenye EU moja kwa moja.

  Nafikiri uongozi wa JF unaweza kujaribu hili (kama haujahi kufanya) na kama ulifanya na ukakataliwa, basi kila mwaka ikumbukwe kuna bajeti mpya na mnaweza tena kutuma maombi. Sijui katika sheria zenu kipesa zikoje, ila kama inawezekana kuomba basi msisite kufanya hivyo na hii hata ikibidi kwenye foundation kama za akina Billy Gates nk. Kama JF itafikishwa hadi walau kwenye tarafa au kata kwa Tanzania nzima, itakuwa vizuri sana. Na uongo mbaya, ili zifike huko inabidi mtandao na computers ambazo inabidi ziwe nyingi na ghalama pia kubwa. Ila kufungua watu macho siku zote ni aghali sana.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Nyie wekeni mnaviwekea vifisadi dagaa vile hizo pesa then viwewe papa.
  Hapa bongo bana kila kitu dili waache watangaze dau watu watachangamkia dili hilo.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hii post yako ipo kuntu sana naamini akina Max wanasoma na wataifanyia mwendelezo.
  JF idumu
   
 13. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #13
  May 27, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Hili wazo si geni... niliwahi kulitoa kule eThinkTank-TZ. Wakasema ni baya.
   
 14. Z

  Zahir Salim Member

  #14
  May 27, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa Wazungu ndio Mafisadi iko haja sasa Tuwafukuze Nchini Mwetu, hawana msaada wa aina yeyote, hawa ni Wahuni waliokuja kwa mlango wa Nyuma kupora rasilimali zetu na huku kulea Serikali ya CCM iliodhaifu na kandamizaji ijikite zaidi katika Madaraka. Mafisadi wanajulikana na wanatajwa kila siku ya Mungu hakuna hatuwa wanayochukuliwa sasa wao kutowa Fedha kwa kudhamini kufunguwa mtandao wa kuwataja mafisadi huko si Kutubereuza sisi Watanzania? wasimae na sisi kutupa KATIBA Mpya na Chaguzi Huru na za Haki na waone kama mafisadi watabakia, hili hawalifanyi walifanyalo ni Ubaradhuli mtupu tuwakomeshe kwa kuwafukuza hjapa petu watokomee kwao huko Ulaya wakahanisiane wenyewe kwa wenyewe.
   
Loading...