31 october vijana tukafanye maamuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

31 october vijana tukafanye maamuzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by lewas, Sep 17, 2010.

 1. l

  lewas New Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi wana jimii kwa mara ya kwanza najitokeza kwenye jukwaa la uchaguzi 2010 nimeona nianze kwa kuwakumbusha vijana wenzangu zile kadi siyo za kufungulia account za benki tu lakini 31 october zitumike kufanya maamuzi makubwa kwa nchi yetu.
   
 2. P

  Paul S.S Verified User

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Vijana watambue kwamba masuala ya msingi yanayohusu ustawi na maendeleo yao binafsi na ya nchi yanategema sana ushiriki wao katika siasa za nchi, na hasa katika kuchagua viiongozi watakaoweza kutimiza haja zao.

  Zipo changamoto nyingi zinazowakabili vijana wa leo, ambazo kama hazitozingatiwa na viongozi, basi maisha ya mbeleni ya vijana yapo mashakani. Tukiangalia kwa karibu, suala la ajira kwa vijana limekuwa ni kero, dunia nzima, lakini kwa Afrika limekuwa ni kero zaidi.

  Pamoja na kwamba vijana wenyewe na jamii kwa ujumla ina jukumu kubwa katika kuhakikisha serikali ina mikakati endelevu na inayofaa katika kupatia vijana ajira, serikali ina jukumu la kwanza katika kutengeneza mazingira yanayoweza kuleta ajira.

  Katika kipindi hiki cha kuchagua viongozi, suala la ajira lipewe kipaombele na vijana wanapohudhuria kampeni hawana budi kuwauliza wagombea maswali magumu kuhusu hatima ya ajira, tena ajira yenye ujira mzuri unaoweza kukidhi mahitaji ya lazima ya binadamu.

  Leo hii ni zaidi ya asilimia 47 ya vijana ambao hawana ajira dunia nzima na zaidi ya asilimia 80 ya vijana duniani wanaishi katika nchi zinazoendelea ambako ukosekanaji wa ajira ni mara tatu zaidi ya nchi zilizoendelea. Tatizo ni kubwa na halijapata ufumbuzi ata hapa Tanzania.

  Mikakati mizuri ya kuondoa umaskini itazidi kuwa ndoto kama idadi kubwa ya vijana wataendelea kukosa ajira, hawa ni kundi la maskini wa leo na kesho. Je vijana wenyewe wana mawazo gani kuhusu changamoto hii? Je wanafuatilia kwa karibu ajenda za vyama vya siasa kuhusu ajira kwa vijana na je wanauliza ahadi za ajira kwa vijana zimefikia wapi? Na ikumbukwa kwamba hili sio tu suala la chama kimoja, bali kila chama kina wajibu wa kuhusika katika mchakato wa kutengeneza fursa za ajira kwa vijana, aidha kwa kushiriki kikamilifu katika michakato mbalimbali, kwa kuhamasisha vijana au kwa kuhamasisha serikali kwa kuiwajibisha vya kutosha kutekeleza ahadi.

  Ili vijana wasivutwe katika siasa za rushwa na kudanganywa kwa zawadi za muda mfupi, hawana budi kuuliza maswali magumu yanayohusu upatikanaji wa ajira endelevu, itakayostawisha maisha yao binafsi, ya familia zao na taifa kwa ujumla. Leo hii, ni aidi ya vijana milioni 238 wanaoshi kwa chini ya dola moja kwa siku. Viajana wanaitafakari hali hii kwa namna ipi?

  Kama vile ukosekanaji wa ajira hautoshi, wapo baadhi ya vijana ambao wameweza kijiajiri, wengine wameajiriwa, lakini je ni ajira ya aina gani? Suala sio tu kuwa na ajira, bali ni kuwa na ajira inayostahi utu wa binadamu na kuweza kukidhi mahitaji ya lazima. Sasa, kutokana na takwimu za Shirika la Kazi duniani, vijana walio katika ajira mbovu ni zaidi ya million 130, hawa ni maskini, pamoja na kwamba wana ajira.

  Hawa ni kundi la vijana, wakiungana na wengine wengi ambao wamevuka ujana ambao wanapata ujira ambao kamwe hautawatoa katika dimbwi la umaskini. Kwa maana ya kwamba, ujira wanaopata hautoshi kukidhi mahitaji yao ya msingi na mbaya zaidi, hauwapi ata nafasi ya kujikwamua katika hali duni, aidha kwa kuwekeza, kujiendeleza au kujiwezesha kupanuka kimawazo na kiuchumi.

  Ukosekanaji wa ajira kwa vijana ni tatizo kubwa ambalo linahitaji uchambuzi yakinifu, unaoongozwa na vijana wenyewe. Na kipindi hiki cha uchaguzi ni fursa nyingine kwa vijana kulijadili zaidi na kutafuta ufumbuzi wa kudumu. Vijana waongee na wagombea na mwisho wamwapigie kura wale wanaoonekana kuwa na dira na mikakati yenye tija kwa vijana.

  Chanzo: Mwananchi
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  lewas
  [​IMG] Junior Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] Join DateFri Sep 2010Posts2 Thanks : 0
  Thanked 0 Times in 0 Posts
  Karibu sana, naamini na wewe ni kijana pia........kukumbusha huku kusiishie hapa tu! kama mwanaharakati, usisite kuanzisha mijadala ya kuhamasisha vijana kupiga kura popote utakapokuwepo.
   
 4. MAWANI

  MAWANI Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Do not SAY NO TO KIKWETE; SAY YES TO DR. SLAA. BECAUSE IF YOU SAY NO TO KIKWETE, AND YES TO SLAA, THEN YOUR VOTE WILL BE COUNTED AS SPOILT.

  SAY YES TO DR. SLAA
  :glasses-nerdy:
   
 5. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii yaweza kuwa a vry gud point, AISEEE!
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ipende Chadema ,ipende CCM ,penda na chama kingine chochote kile ila hakikisha kura yako ya Ndio unaipeleka CUF.
   
Loading...