Aug 8, 2013
10
33
1599112353934.png

CHAMA CHA MAPINDUZI

MUHTASARI WA ILANI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020


Imetolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Agosti, 2020


CHAMA CHA MAPINDUZI

MUHTASARI WA ILANI YA UCHAGUZI WA MWAKA 2020-2025

UTANGULIZI

1. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa vyama vya TANU na ASP na baadae CCM, imejengwa katika misingi ya ujamaa na kujitegemea inayozingatia utu, usawa na haki. Misingi hii imeimarishwa na siasa safi na uongozi bora wa CCM na imekuwa ndio nguzo ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa. CCM itaendelea kuzisimamia serikali zake kuhakikisha kuwa zinazingatia, kulinda na kudumisha misingi hii adhimu.

2. CCM itahakikisha kuwa Tanzania inaendelea kulinda Uhuru wake, kudumisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na kuimarisha Muungano wetu wenye mfumo wa serikali mbili ili kuendelea kujenga Taifa imara linalojitegemea kiuchumi na kisiasa, lenye ustawi wa watu wake na linaloenzi na kuthamini mila nzuri, desturi na utamaduni wetu.

3. CCM inaamini kwamba uzalendo kwa nchi ndio msingi wa maendeleo ya kweli ya Tanzania ambayo yataletwa na Watanzania wenyewe. Hivyo basi, CCM itaendelea kuhimiza wananchi kuwa wazalendo kwa nchi yetu kwa kufanya kazi kwa uadilifu, bidii na maarifa kama msingi imara wa maendeleo.

4. CCM inaamini pia kuwa kila mtu ana jukumu la kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujiletea maendeleo yake na Taifa kwa ujumla. Imani hii ndiyo chimbuko la kauli mbiu za Hapa Kazi Tu! na Kuacha Kufanya Kazi kwa Mazoea! Aidha, CCM inatambua kuwa serikali inazoziongoza zina jukumu la msingi la kuhakikisha kuwa walio wanyonge katika jamii wanapata fursa ya kipekee ya kustawisha maisha yao na kuondokana na unyonge wao ili kupunguza tofauti za matabaka.

5. CCM inatambua kuwa nchi yetu ina watu wenye uwezo na rasilimali za kutosha kama vile ardhi, madini, gesi asilia, misitu, wanyama, malikale/mambo ya kale, bahari, maziwa na mito, pamoja na nafasi na fursa nzuri za kijiografia. Rasilimali na fursa hizi zikitumiwa vizuri zitakuwa chachu kubwa kwa maendeleo ya Taifa, kama ambavyo imethibitika katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 na kwamba tukiamua tunaweza. Ni katika muktadha huu CCM inaamini kuwa Tanzania ni nchi tajiri.

6. Katika miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 -2020 chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, mafanikio makubwa yamepatikana katika nyanja na sekta zote za maendeleo kwa ustawi wa wananchi. Mafanikio haya ni pamoja na:-

(a) Kuendelea kulinda na kuimarisha umoja, mshikamano, amani, utulivu, ulinzi na usalama;

(b) Kuendelea kulinda, kuimarisha na kudumisha Uhuru, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania;

(c) Kuendelea kulinda na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi, haki za binadamu, nchi isiyofungamana na dini yoyote, na kupambana na unyanyasaji na udhalilishaji wa aina zote;

(d) Kuendelea kuwa nchi isiyofungamana na upande wowote ili kuweza kutetea na kulinda masilahi ya nchi yetu kwa kuzingatia misingi tunayoiamini;

(e) Kuimarisha utumishi wa umma unaozingatia weledi, nidhamu, uadilifu, bidii na maarifa katika kazi;

(f) Kuimarisha mifumo ya kisera, kitaasisi na kisheria ikiwemo kutungwa kwa sheria inayotaka Serikali za mitaa kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake (4%), vijana (4%) na watu wenye ulemavu (2%);

(g) Kuimarishwa kwa Ofisi ya Msajili wa Hazina kulikowezesha kusimamia na kuboresha utendaji wa mashirika ya umma yaliyoweza kuchangia jumla ya shilingi trilioni 1.052 kama gawio na michango kwa Serikali.

(h) Kuhamishia Serikali Makao Makuu ya Nchi Dodoma;

(i) Kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa, uhujumu wa uchumi na ufisadi na hivyo kuokoa fedha na rasilimali nyingine na kuzielekeza kwenye mipango ya maendeleo ya nchi;

(j) Kuimarisha mapambano dhidi ya uzalishaji, uagizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya, utakatishaji wa fedha haramu na biashara ya kusafirisha binadamu;

(k) Kujitosheleza kwa chakula na kuzalisha ziada kwa ajili ya masoko ya nje;

(l) Kuimarisha uchumi wa viwanda ambapo idadi ya viwanda imeongezeka kutoka viwanda 52,633 mwaka 2015 hadi kufikia viwanda 61,110 mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.1. Kutokana na hatua hii, uzalishaji wa bidhaa na ajira umeendelea kuongezeka;

(m) Kutekeleza miradi ya kimkakati yenye tija kubwa katika uchumi na ustawi wa jamii ikiwemo miradi ifuatayo: Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere; ujenzi wa reli ya kisasa (SGR); kufufuliwa kwa Shirika la Ndege la Taifa kwa kununua ndege mpya 11; kununua meli mbili mpya Zanzibar; na ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume;

(n) Kuimarisha mfumo wa udhibiti, usimamizi na umiliki wa madini na hivyo kuongeza mapato yatokanayo na mazao ya madini kutoka shilingi bilioni 168 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 346 mwaka 2019;

(o) Kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 kwa mwezi mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa shilingi trilioni 1.3 mwaka 2019. Kwa upande wa Zanzibar mapato ya Serikali yameongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 428.5 mwaka 2015/2016 hadi kufikia shilingi bilioni 748.9 mwaka 2018/19. Mafanikio hayo yameongeza uwezo wa Serikali wa kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma za jamii kwa wananchi;

(p) Kuchukua hatua thabiti za kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari za uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuondoa matumizi ya mifuko ya plastiki; na

(q) Kuendelea kupiga hatua za maendeleo katika maeneo mbalimbali kama vile ujenzi wa miundombinu ya kisasa, kukua kwa kasi kwa uchumi na kuimarika kwa ustawi wa jamii. Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika na hivyo kuwezesha kufikia nchi ya uchumi wa kati.

(r) Matokeo ya mafanikio haya kwa maendeleo na ustawi wa wananchi ni pamoja na:-

(i) Kwa upande wa Tanzania Bara:

▪Wastani wa Pato la Mwananchi limekua kutoka shilingi 1,968,965 mwaka 2015 hadi shilingi 2,458,496 mwaka 2018, na Pato la Taifa limeongezeka kwa wastani wa asilimia 6.7 kwa mwaka;

▪Wastani wa umri wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 61 mwaka 2015 hadi miaka 65 mwaka 2020;

▪Kuongezeka kwa upatikanaji wa umeme kutoka megawati (MW) 1,308 mwaka 2015 hadi megawati (MW) 1,602.32 mwaka 2020. Vilevile, usambazaji wa umeme vijijini umeongezeka kutoka asilimia 16.4 mwaka 2015 hadi asilimia 67.1 mwaka 2020;

▪Kuimarika kwa huduma ya umeme nchini na hivyo kuondoa mgao wa umeme uliokuwa kero na kikwazo kikubwa kwa shughuli za kiuchumi na kijamii;

▪Kutoa elimu bila malipo katika ngazi ya shule za msingi na sekondari na hivyo kuongeza udahili wa wanafunzi katika ngazi zote za elimu. Kwa mfano, idadi ya wanafunzi wa sekondari imeongezeka kutoka wanafunzi 1,648,359 mwaka 2015 hadi 2,185,037 mwaka 2019;

▪Kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini kutoka 65,064 mwaka 2015 hadi 87,813 mwaka 2019;

▪Kuongezeka kwa idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama vijijini kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.1 mwaka 2020. Kwa upande wa mijini, idadi ya wananchi wanaopata maji safi na salama imeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 85 mwaka 2020. Kwa ujumla, idadi ya kaya zinazopata maji safi nchini kutoka vyanzo salama imeongezeka hadi kufikia asilimia 77 mwaka 2020;

▪Kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za afya (zahanati, vituo vya afya na hospitali) kutoka 7,014 mwaka 2015 hadi 8,446 mwaka 2020;

▪ Kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji wa

dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoka asilimia 42 ya mahitaji mwaka 2015 hadi asilimia 94.5 mwaka 2020;

▪ Kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kimepungua kufikia asilimia 26.4; na

▪ Kuboresha makazi na nyumba za wananchi, ambapo asilimia ya kaya zinazoishi katika nyumba zenye mapaa ya kisasa imeongezeka kutoka asilimia 68.0 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 84.1 kwa mwaka 2018/19.

(ii) Kwa upande wa Zanzibar

▪Wastani wa Pato la Mwananchi limekua kutoka shilingi 1,666,000 mwaka 2015 hadi shilingi 2,549,000 mwaka 2019, na Pato la Taifa limeongezeka kwa wastani wa asilimia 6.8 kwa mwaka;

▪Wastani wa umri wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 66.6 mwaka 2015 hadi miaka 68.4 mwaka 2020;

▪Usambazaji wa huduma za umeme umeongezeka kutoka asilimia 70 mwaka 2015 hadi asilimia 90 mwaka 2020;

▪Kuendelea kutoa elimu bure hadi ngazi ya sekondari ikiwa ni utekelezaji wa sera ya msingi ya Mapinduzi ya 1964;

▪Kuongezeka kwa idadi ya wananchi wanaopata maji safi na salama vijijini kutoka asilimia 60 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 72 mwaka 2020. Kwa upande wa mijini, idadi ya wananchi wanaopata maji safi na salama imeongezeka kutoka asilimia 80 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 87 mwaka 2020. Kwa ujumla, idadi ya kaya zinazopata maji kutoka vyanzo salama imeongezeka hadi kufikia wastani wa asilimia 83 mwaka 2020;

▪Kuendelea kutoa huduma ya matibabu bure na kuongeza bajeti ya ndani ya ununuzi wa dawa muhimu kutoka shilingi bilioni 0.5 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 12.7 mwaka 2020 na hivyo kuongeza ugharamiaji huo kutoka asilimia 7 ya mahitaji hadi asilimia 97 ya mahitaji yote; na

▪ Kuimarisha na kupanua matumizi ya utafiti katika kufanya maamuzi sahihi ya sekta mbalimbali.

MALENGO YA UCHAGUZI YA MWAKA 2020 – 2025

7. Ilani hii inalenga kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015. Vilevile, maudhui ya Ilani hii yamezingatia Mwelekeo wa Sera za Chama Cha Mapinduzi wa 2020-2030, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020-2050. Aidha, Ilani hii imezingatia fursa na changamoto zinazotokana na mabadiliko mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiteknolojia yanayotokea nchini na duniani, pamoja na madhara ya janga la ugonjwa wa Corona.

8. CCM inatambua kwamba utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo utafikia kikomo chake katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii. Hivyo Chama kitazisimamia serikali zake kuandaa Dira mpya ya Taifa ya Maendeleo kuelekea mwaka 2050, na kuanza utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2020 – 2050. Katika miaka mitano ijayo, lengo la CCM ni kuendelea kustawisha maisha ya kila Mtanzania. Katika kufikia lengo hili vipaumbele vikuu vya serikali za CCM katika miaka mitano ijayo vitakuwa vifuatavyo:-

(a) Kulinda na kuimarisha misingi ya utu, usawa, haki na uongozi bora ili kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu;

(b) Kukuza uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani uliojengwa katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi;

(c) Kuleta mageuzi ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwa na uhakika wa chakula na kujitegemea kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi;

(d) Kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, maji, umeme na makazi vijijini na mijini;

(e) Kuchochea matumizi ya utafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo ya maendeleo ya haraka ya kijamii na kiuchumi; na

(f) Kutengeneza ajira zisizopungua 8,000,000 (milioni nane) katika sekta rasmi na isiyo rasmi kwa ajili ya vijana.

Mambo muhimu yatakayozingatiwa katika kutekeleza vipaumbele vikuu vya Ilani hii ni kama ifuatavyo:-

A. Kulinda na kuimarisha utu, usawa, haki na uongozi bora ili kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu:-

(i) Kuendelea kudumisha na kuimarisha umoja, udugu, mshikamano, amani, utulivu, ulinzi na usalama;

(ii) Kuendelea kuimarisha Muungano wa serikali mbili, kuenzi Uhuru wa nchi yetu na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pamoja na kutumia tunu nyingine za kitaifa ikiwemo falsafa ya Mwenge wa Uhuru katika kujenga moyo wa uzalendo wa kitaifa na uwajibikaji;

(iii) Kuendelea kuimarisha demokrasia, utawala bora na haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, pamoja na udhalilishaji wa aina zote;

(iv) Kuendelea kuimarisha Serikali za Mitaa ili ziweze kutimiza wajibu wao kwa wananchi katika maeneo husika;

(v) Kuendelea kujenga mazingira wezeshi kwa asasi za kiraia, kidini na vyombo vya habari kustawi ili kuchangia katika maendeleo ya Taifa; na

(vi) Kuendelea kuimarisha huduma na kulinda haki kwa makundi maalum wakiwemo wanawake, vijana, wazee, watoto na watu wenye ulemavu.

B. Kukuza uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani uliojengwa katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi:-

(i) Kuendelea kujenga na kukuza uchumi shindani hususan kupitia sekta za viwanda na huduma za kiuchumi utakaowezesha ustawi wa wananchi wote;

(ii) Kuendelea kuimarisha miundombinu ya kimkakati ili kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi na tija;

(iii) Kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kukua na kustawi pamoja na kuvutia wawekezaji ili watoe mchango stahiki katika maendeleo ya nchi yetu;

(iv) Kuendelea kuboresha masilahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi katika sekta zote;

(v) Kuongeza faida ambazo nchi yetu inapata kutokana na maliasili zetu na utajiri wa nchi kwa kuimarisha usimamizi wa mikataba ya uzalishaji na kujenga uwezo wa ndani wa kuvuna na kuchakata/kusarifu rasilimali hizo;

(vi) Kuimarisha usimamizi na uhifadhi wa mazingira na uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi;

(vii) Kutenga maeneo maalum ya akiba ya ardhi na uwekezaji;

(viii) Kuendelea kuimarisha mawasiliano ya simu za mkononi nchini ili yaweze kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa maendeleo ya wananchi; na

(ix) Kuendeleza diplomasia ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ikiwa ni pamoja na kufanya lugha ya Kiswahili kutumika kikamilifu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN).

C. Kuleta mageuzi ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwa na uhakika wa chakula na kujitegemea kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi:-

(i) Kuhakikisha uzalishaji unaongezeka katika mazao ya chakula, ufugaji na uvuvi kwa ajili ya kujitosheleza kwa chakula na lishe bora;

(ii) Kuongeza tija katika kilimo, ufugaji na uvuvi kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya uchumi hasa katika sekta za viwanda na huduma;

(iii) Kuimarisha ushirika ili kuunganisha nguvu za wazalishaji hasa katika kupata pembejeo na kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi;

(iv) Kuimarisha miundombinu na kuongeza maeneo ya umwagiliaji katika kilimo ili kupata mazao mengi zaidi kwa wakati wote wa mwaka; na

(v) Kukamilisha na kutekeleza mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya shughuli za kijamii, uwekezaji na uzalishaji.

D. Kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za Afya, Elimu, Maji, Umeme na Makazi vijijini na mijini:-

(i) Kuongeza kasi ya usambazaji majisafi na salama ili kutosheleza mahitaji kwa zaidi ya asilimia 85 vijijini na zaidi ya asilimia 95 kwa mijini kwa upande wa Tanzania Bara ifikapo mwaka 2025, na zaidi ya asilimia 95 kwa upande wa Zanzibar;

(ii) Kuendelea kuimarisha mfumo wa elimu ili uweze kuzalisha wataalam mahiri zaidi wenye uwezo katika sayansi, teknolojia, ufundi na nyanja nyingine ambao wanaweza kujiajiri na kuajirika ndani ya nchi na mahali popote duniani;

(iii) Kusambaza umeme kwenye mitaa na vijiji vyote ifikapo mwaka 2025;

(iv) Kutoa huduma za afya kwa wote;

(v) Kuhamasisha na kuweka mazingira wezeshi ili wananchi katika maeneo yote nchini wawe na makazi bora (“Nyumba bora kwa wananchi wote inawezekana”).

E. Kuchochea matumizi ya utafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo ya maendeleo ya haraka ya kijamii na kiuchumi:-

(i) Kuimarisha na kuhuisha taasisi za utafiti, sayansi, teknolojia na ufundi ili ziweze kubuni nyenzo za kuongeza tija katika sekta za uzalishaji na huduma;

(ii) Kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na kompyuta na huduma za intaneti;

(iii) Kusomesha Watanzania nje ya nchi katika vyuo bora na maalum duniani kwenye masuala ya sayansi, tiba,

teknolojia na maeneo mengine yenye umuhimu ili kupata maarifa bora na ya kisasa na ujuzi ili kuchochea maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini; na

(iv) Kuchochea na kuendeleza ubunifu, uvumbuzi na ugunduzi nchini kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

F. Kutengeneza ajira zisizopungua 8,000,000 (milioni nane) katika sekta rasmi na isiyo rasmi kwa ajili ya vijana:-

(i) Kuchochea ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya viwanda vinavyotumia malighafi za kilimo, mifugo, uvuvi, madini, maliasili na sekta ya huduma za kiuchumi ikiwa ni pamoja na utalii;

(ii) Kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za ujasiriamali, ikiwemo kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na taasisi na asasi za utoaji mikopo yenye riba na masharti nafuu;

(iii) Kuwahamasisha na kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika utamaduni, michezo na sanaa kwa ajili ya afya bora na burudani na pia kuongeza fursa za ajira na kipato; na

(iv) Kuhakikisha kuwa miradi mikubwa ya kimkakati inaajiri vijana wengi zaidi wa Kitanzania.

AHADI YETU

9. CCM itahakikisha serikali zake zinatekeleza mambo yote yaliyoahidiwa katika Ilani hii kwa manufaa na ustawi wa Taifa letu. Utekelezaji wa Ilani hii utaongozwa na kauli mbiu ifuatayo: “Tumetekeleza kwa Kishindo, Tunasonga Mbele Pamoja”

10. Ilani hii ni tamko na ahadi maalum ya nia na uwezo wa CCM kuendelea kuongoza nchi, kuleta ustawi wa Watanzania wote na kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, hususan wanawake, vijana, watoto, wazee, pamoja na watu wenye ulemavu. Katika miaka mitano ijayo, CCM itahakikisha matarajio ya wananchi katika nyanja zote yanafikiwa. Chama Cha Mapinduzi kinawaomba Watanzania wote waendelee kukiamini na kukichagua ili kiendelee kuongoza nchi na kuleta maendeleo makubwa na ya haraka kwa faida ya wananchi wote.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
1599111019172.png
1599111127474.png
1599111142699.png
1599111206733.png
1599111219400.png
1599111238014.png
1599111251036.png
1599111264415.png
1599111277151.png
1599111289788.png
1599111304816.png
1599111319595.png
1599111337475.png
1599111353905.png
1599111366648.png
1599111382845.png
1599111398201.png
1599111414102.png
1599111427050.png
 

Attachments

  • ILANI YA CCM 2020.pdf
    5.5 MB · Views: 70
UCHAMBUZI WA ILANI YA CCM 2020-25.

MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA NA UFISADI.

Watanzania walichoka sana kusikia stori za Rushwa na Ufisadi kwenye Ofisi za umma na Watumishi wa umma. Kuingia kwa Serikali ya Awamu ya 5 kulitoa matumaini ya Taifa lao kuanza kupambana kwa dhati dhidi ya Vitendo vya Rushwa na Ufisadi.

Katika kuhakikisha Rushwa na Ufisadi unapingwa kwa vitendo, Ilani ya CCM kwenye Sura ya 6 kuanzia kipengele cha 113 hadi 115 kimeleeza kwa undani mikakati, mipango na mafanikio katika Kupambana na vitendo hivyo ambapo Tayari Serikali ya CCM ilifungua Ofisi mpya 21 katika Wilaya zote ambazo hazikuwa na Ofisi za TAKUKURU na Kuanzisha Mahakama maalum ya kushughulika na Makosa ya Rushwa, Ufisadi na Uhujumu Uchumi ambapo ndani ya Miaka minne tu toka kuazishwa kwake mwaka 2016 tayari kesi 407 za Uhujumu Uchumi zimeripotiwa na kesi 385 kusikiliziwa, kufungua mashauri 2,256 ya Rushwa na kesi 1926 kutolewa maamuzi pamoja na kuokoa kiasi cha Billion 273.38 zilizokuwa zinakwenda kwenye midomo ya Mafisadi na Wala Rushwa.

Tayali Ilani ya CCM ya Mwaka huu 2020 imeelekeza zaidi kwenye Sura ya 6 kipengele cha 116 kuendelea kupambana na Rushwa na Ufisadi kwa Kuimarisha mifumo ya TAKUKURU, Kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi na Kuhamasisha zaidi Watanzania kuripoti matukio ya Rushwa na Ufisadi.

Bwanku M Bwanku

TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.
 
UCHAMBUZI WA ILANI YA CCM 2020-25.

KUONGEZA FURSA ZA AJIRA.

Katika kujenga Uchumi imara na Maendeleo ya mtu mmoja mmoja, Ilani ya CCM imegusa kila eneo la kutoa nafasi za ajira hasa kwa kundi la Vijana. Ilani hii kwenye Sura ya Pili kipengele cha 31 (d) imeeleza mafanikio makubwa ya utoaji wa Ajira takribani 6,032,299 katika Sekta rasmi na isiyo rasmi kwenye miradi ya Maendeleo ya Serikali ya kimkakati na zile Ajira zilizozalishwa kwenye Sekta zisizo rasmi, Kutoa mikopo ya takribani Billion 17.9 kwa makundi ya vijana 535 yenye wanachama 3745 kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri za mamlaka Serikali za mitaa.

Zaidi Mafanikio ya mafunzo ya Vijana 67,243 kwenye eneo la kukuza ujuzi na stadi za kazi, kutoa mafunzo kwa vitendo kwa Wahitimu 5975 mahali pa kazi, Halmashauri 111 kutenga maeneo yenye ukubwa wa ekari 217.8 ili kuwawezesha vijana kufanya shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji, biashara na viwanda.

Zaidi Serikali kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita imefanikiwa kuongeza fursa za ajira kupitia miradi mikubwa ya kimkakati ambayo Serikali imeendelea kuitekeleza ikiwemo Standard Gauge iliyotoa ajira 11,756 Ubungo Interchange ajira 449, upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere Terminal III ajira 997 na mradi wa kufua umeme wa Mwl Nyerere ajira 2783.

Katika miaka mitano ijayo Ilani ya CCM imepanga kuongeza ajira mpaka kufikia Million 7 kwenye Sekta rasmi na zisizo rasmi huku ikitia mkazo zaidi kwa Halmashauri zote nchini kuendelea kutenga na kutoa fedha kwa makundi ya Vijana, akina mama na walemavu, Vijana kuhamasishwa kushiriki shughuli za ujasiriamali kwa kuwapatia mafunzo, kuendelea kutoa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa vijana, kuhakikisha miradi mikubwa ya kimkakati inaongeza zaidi ajira kwa vijana, kuimarisha SACCOS na Sera kuwawezesha vijana kupata mikopo na kujiajiri.

TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.

Bwanku M Bwanku
 
BIASHARA

CCM inatambua kuwa biashara ni kichocheo cha maendeleo ya viwanda na sekta nyingine za kiuchumi na kijamii. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita CCM iliendelea kuisimamia Serikali kuhakikisha sekta ya biashara inaendelea kuimarika na kutoa fursa za masoko kwa mazao na bidhaa.

Ilani hii ya CCM kwenye sura yake ya pili katika kipengele cha 49 ukurasa wake wa 60-61 kwa kutambua umuhimu wa sekta ya biashara imeelekeza vyema katika kipindi cha miaka mitano ijayo itahakikisha mchango wa sekta ya biashara unaendelea kuimarika na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi kwa kutekeleza yafuatayo:-

(a) Kuweka mazingira wezeshi ya biashara na kuhakikisha kwamba zinapatikana fursa nafuu za kibiashara ili kuchochoea ujenzi wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora kwa kimataifa.

(b) Kufanya mapitio na maboresho ya sera na mikakati mbalimbali itakayoimarisha mazingira ya ufanyaji biashara na kukuza biashara ndani na nje ya nchi.

(c) Kubuni na kutekeleza mikakati ya kurahisisha mazingira ya ufanyaji biashara nchini kwa kuimarisha utekelezaji wa mpango kazi wa kuboresha mazingira ya biashara nchini (Blueprint for Regulatory Reforms to Improve the Business Environment) ikiwemo kuhakikisha taratibu bora za udhibiti na utoaji wa leseni za biashara.

(d) Kuratibu ujenzi wa masoko ya kimkakati katika maeneo ya mipakani ili kuwapa wakulima, wajasiriamali wadogo hususan wanawake na vijana fursa ya kuuza mazao nje ya nchi.

(e) Kubuni na kutekeleza mikakati ya kutoa elimu na kuondoa vikwazo vya utaratibu wa stakabadhi ya mazao ghalani ikiwa ni pamoja na kuhamasisha sekta binafsi kujenga miundombinu ya maghala bora ya kuhifadhia mazao mbalimbali hususan vijijini.

TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE KWA PAMOJA.
 
Ulaya hasa Uholanzi nasikia wanateknolojia ya kuondoa chumvi na maji ya bahari kuwa maji mazuri kwa matumizi ya majumbani.

Ikiwa tumebarikiwa bahari toka kwa Mungu, ewe Rais wetu peleka mainjinia Ulaya wakachukue technology hiyo ili Tanzania inufaike.

Ningependa kwenye msafara huo niwemo na hivi sijawahi fika Ulaya achilia mbali kupanda tu ndege bado. Asante
 
Wanatumia kwa matumiz ta kufulia na kunwagia pamoja na kuogea tu hayaruhusiwi kupikia wala kunywa hata dubai oman hii ipo na sheria ji hizo hizo kuna gar zinagawa maji ya kunywa na kupikia za serikal wanalipia kwa bill
Nina shaka,yana ubaya gani ikiwa tu maji ya chooni ya kuflash hugeuzwa na kuwa safi na wanakunywa sembuse ya bahari ndugu.
 
Tanzania tuna maji fresh mengi sana, (fresh water body), mfano lake Victoria, lake Nyasa, lake natron, lake eyas, lake Rukwa, bila kusahau mito mingi mfano: Ruaha (Rufiji) , Pangani, Malagarasi, Songwe, Ruvuma, Ruvu, Wami, Mara, n.k.

Hivi kweli tumeshindwa kutumia maji matamu yote hayo kwenye matumizi yetu ya kibinadamu kama nyumbani , kilimo na viwandani, kiasi cha kuyavuta tu kwenye mabomba na kuweka pumps za kuyasukuma, hadi tuje kuingia gharama kubwa ya technology kwenda kununua ujuzi huo ulaya na kuja kuweka baharini kwa pesa ndefu?!

Tutumie kwanza haya maji baridi, mengi aliyotujaalia Muumba tena buree, kuwafikishia watanzania , hiyo gharama ya maji ya bahari tuwaachie kwanza nchi zenye majangwa kama uarabuni,
 
Ndugu mito hukauka si ya uhakika,au kina chake hupungua,pia I'll kupunguza cost na uendeshaji bora chanzo kiwe kimoja nacho ni bahari kwa kigoma na mikoa ya kusini ziwa Tanganyika na nyasa ni sahihi kuwa chanzo cha maji majumbani.
 
Ndugu mito hukauka si ya uhakika,au kina chake hupungua,pia I'll kupunguza cost na uendeshaji bora chanzo kiwe kimoja nacho ni bahari kwa kigoma na mikoa ya kusini ziwa Tanganyika na nyasa ni sahihi kuwa chanzo cha maji majumbani.
Hivi hiyo lake Tanganyika unaijua vizuri??
 
Acha maji ya bahari kuwa maji ya matumizi, hata akibadili "KINYESI" kuwa "UDI/MARASHI". Hatumtaki. Eleweni hatumtaki!!!
 
Taabu yote ya nini? Desalination wanatumia wasio na vyanzo vya kutosha vya maji baridi kama Saudi Arabia, Australia, Israel n.k

Sie tumezungukwa na ziwa nyasa, victoria na tanganyika, kuwa na shida ya maji pamoja na kushindwa kukuza kilimo cha umwagiliaji ni kielelezo cha ujinga na umbumbumbu wa serikali tunazoziweka madarakani.
 
Back
Top Bottom