27 wafariki dunia kwa jali ya basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

27 wafariki dunia kwa jali ya basi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 11, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,873
  Likes Received: 83,351
  Trophy Points: 280
  Kuna breaking news kwenye gazeti la Mwananchi kwamba basi la Tashriff limepata ajali na watu 27 wamepoteza maisha. Mwenye habari zaidi aziweke hapa ukumbini. Haya mabasi yanatumaliza tu Watanzania kwa ajali ambazo zinaweza kabisa kuzuilika.
   
 2. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimesikia watu 29 wamepoteza maisha- Tashrif bus imepata ajali mbaya jana saa 3 usiku. Ilitokea DAR kwenda TANGA, ilipofika Hale pale kituo cha mafuta cha Makinyumbi iligonga gari la magogo lililokuwa limepaki pembeni kwa matengenezo, ni baada ya kujaribu ku-overtake gari nyingine! Watu wengi walipoteza life palepale na mmoja kufia Muheza hospital kufanya idadi ya vifo kuwa 27 ama 29 hivi.
  MUNGU awalaze mahala pema peponi. Amen
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Jamani, tukiacha suala la madereva wazembe, je amuoni kama hizi barabara zilivyofinyu na hazina highway patrol za kuyavuta magari mabovu na kuyaondoa barabarani pia zinachangia. Kwa nini serikali isianzishe mradi wa kuzipanua barabara, kuwalipa matrafiki mishahara mizuri na kuakikisha wavunja sheria wanachangia katika kujenga hizi barabara kupitia faini. Mfano trafiki anapata bonus kulingana na magari anayokamata kwa makosa barabarani etc.

  Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,873
  Likes Received: 83,351
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  A passer-by stare at the wreckage of the fateful Tashriff bus. (Photos by Mroki Mroki).
   
 5. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana nawe, lakini hili la mishahara mizuri si kwa trafiki tu, kila mtu TZ anahitaji kipato kitakachokidhi mahitaji yake, hapo ndio tutaondoa kwa kiasi fulani ama kupunguza rushwa. Hawa trafiki hutoza madereva wanaovunja sheria, hilo lipo, na nakumbuka juzijuzi Kamanda Kova alitangaza kiasi kilichopatikana. Lakini fedha nyingi huishia kwa hawa jamaa, wakimkamata mtu huchukua rushwa na kumuachia, vilevile mtu akijua kuwa kosa lake ni kutoa 50,000 akifika polisi, basi hutoa 20,000 anayoambiwa na kuachiwa. Pia mabasi huwa yanajaza fomu fulani kuonesha waliondoka saa ngapi, ili wakifika katika kituo cha ukaguzi waonekane kama wanaenda mwendo wa kawaida, lakini hili halisaidii, wakifika kwenye hivi vituo hutoa rushwa. Sasa hivi njia ya Mwanza mpaka Dar es Salaam ni kama imeisha, gari zinakimbizwa vibaya mno, na ni hatari, wafuatiliaji ndio hao.

  Lakini na raia nasi tuna lawama, gari likikimbizwa kupita kiasi huwa tunakaa kimya, na kama ukisema utaoingwa na wengine kuwa tunataka kuwahi. Mwisho wengi wa madereva ni wabovu, kwa kuwa kila kitu pale TZ waweza pata kwa hela, hawa madereva wengi hupata leseni kwa kuhonga, bila hata kufanyiwa majaribio kwa undani.
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Shadow... una mawazo mazuri ya ubunifu! Lakini sio wengi wanojishughulisha kubuni kama wewe. Viongozi wengi wamekaa kungojea ajali zitokee watoe "vapour" zao halafu kesho yake "business as usual". Akili zao sio tofauti na za nyani ambao wakipigwa na baridi usiku wanajikunyata na kusemezana... "kesho asubuhi na mapema lazima tujenge nyumba". Inapofika asubuhi jua likitoka wanasahau kila kitu....... Ndio akina Makamba na CCM hao... Maneno meeeeeengi...
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ama kweli nyani haoni kundule...!
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Jan 11, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Al-hamdu lillahi rabbil 'alamin... "Inna Lillahi Wa Inna Ilayhi Raji'oon"

  All the praises and thanks be to Allâh, the Lord of the Universes...

  “To Allah we belong and to Him we shall return”

  Since we do not know when we will die, we must be prepared for it all the time.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,873
  Likes Received: 83,351
  Trophy Points: 280
  Tayari tumeshapoteza Watanzania wenzetu 38 kwa ajali za barabarani mwaka huu. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi~AMEN.

  Basi laua watu 27
  Anna Makange, Tanga na Mroki Mroki, Korogwe
  Daily News; Sunday,January 11, 2009 @21:15​

  Watu 27 wamekufa papo hapo na wengine 23 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria Kampuni ya Tashrif walilokuwa wakisafiria, kuligonga lori la magogo katika Kijiji cha Hale-Kijijini wilayani Korogwe, mkoani Tanga.

  Hiyo ni ajali kubwa ya pili tangu kuanza kwa mwaka huu, baada ya Januari 4, mwaka huu, kushuhudia watu 11 wa familia moja wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro kufariki kwa ajali ya gari eneo la Uchira Moshi Vijijini, wakitokea katika shughuli ya kipaimara wilayani Hai.

  Ajali ya Tashrif ilitokea juzi saa 2:30 usiku katika Barabara Kuu ya Muheza -Segera wakati basi hilo lilipokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Tanga. Kati ya majeruhi hao, wawili hali zao ni mbaya sana na wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza.

  Basi hilo la Tashrif lenye namba ya usajili T768 ALW lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja tu la Mdoe au maarufu Osama, liliacha njia na kulivamia lori la magogo aina ya Isuzu Scania lenye namba za usajili T594 APA lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara hiyo.

  Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Simon Sirro alisema dereva wa basi hilo alikimbia baada ya tukio hilo na wafanyakazi wengine watatu wa basi hilo waliokuwamo kwenye gari wakati wa tukio, wamefariki dunia papo hapo.

  Kamanda Sirro alisema chanzo cha ajali hiyo, ya pili kubwa mkoani Tanga ikitanguliwa na ile ya basi la No Challenge la mwaka 1998, lililoua abiria wapatao 70, ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa basi hilo na uchunguzi unaendelea. No Challenge lilibadilishwa jina na kuitwa Tashrif.

  Akizungumza jana mchana, Kamanda Sirro alisema waliotambuliwa na ndugu zao ni 18 tu na kwamba tisa hawajatambuliwa kabisa. Alitaja majina ya waliokufa kuwa ni Idrisa Bakari, Hamidu Titu, Salama Ramadhan (30), Mbaruku Salum, Mussa Hussein, Msahamu Alli, Rahabu Jamali, Shaban Bakari, Hamad Ali na Omari Salehe.

  Wengine ni Amiri Sanyo, Salim Mussa, Omari Aljabri, Napendaeli Msangi, Said Abdallah na askari Polisi wilayani Muheza, Koplo Mariam; askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Koplo Mbaraka Mafoni na Koplo Deo Zakaria; wote kwa pamoja umri wao haukufahamika mara moja.

  Alisema kati ya marehemu hao, 14 ni wanaume; watano ni wanawake; watoto wa kiume wawili; wa kike watatu; Polisi mwanamke mmoja na askari jeshi wawili wanaume. Alisema mipango ilikuwa ni kuwahamisha majeruhi wote katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo ili watambulike kirahisi na kupata matibabu ya haraka.

  Majeruhi Jeremia Mkali (48) ambaye amelazwa Bombo, alisema idadi kubwa ya waliokufa ni wale waliokuwa katika harakati za kushuka kwenye basi hilo baada ya kufika kwenye makazi yao hapo kwenye mji mdogo wa Hale.

  Naye Koplo Omar Khalfan ambaye ni askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha Maramba wilayani Mkinga, alisema yeye na wenzake wawili ambao kwa sasa ni marehemu, walipanda basi hilo katika eneo la njiapanda ya Segera wakija Tanga; na yeye alipata kiti cha kukaa na wenzake walisimama.

  Alisema baada ya muda mfupi, alipitiwa na usingizi ambapo ghafla alishtushwa na sauti na kelele za watu na kwamba alipoangaza macho vizuri, ndipo alitambua kwamba kuna gogo pembeni yake na lilikuwa limeingia kupitia kioo kikubwa cha mbele cha basi hilo na kutokea kioo cha nyuma ya basi.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mohamed Abdulaziz aliungana na mamia ya waombolezaji waliojitokeza kutambua maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Bombo sambamba na kutoa salamu za rambirambi kwa wafiwa.

  Kwa upande wake, Rais Jakaya Kikwete ametuma salamu kutokana na ajali hiyo, na kueleza kuwa amesikitishwa sana na jinsi maisha ya Watanzania yanavyoendelea kupotea katika ajali za barabarani. "Nimesikitishwa sana na jinsi maisha ya Watanzania wenzetu yanavyoendelea kupotea katika ajali za barabarani.

  Napenda kwa dhati kabisa kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa watu 27 waliopoteza maisha yao katika ajali ya basi la Tashrif na namwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi Amini," alisema Rais katika rambirambi hizo. Katika tukio lingine, mamia ya wananchi wa eneo la Michungwani wilayani Korogwe, jana waliziba barabara kuu ya Chalinze - Segera kwa zaidi ya saa tatu wakishinikiza barabara ya eneo hilo iwekwe matuta.

  Wananchi hao wakiwa na marungu, waliiziba barabara hiyo kwa makopo, mawe, magogo na kuchoma matairi barabarani wakishinikiza kuwekwa matuta baada ya lori la mizigo kugonga mtu mmoja na kuvamia nyumba kando ya barabara, ambako inadaiwa watu wawili waliokuwamo ndani ya nyumba hiyo walikufa.

  Zahama hiyo ilisababisha magari yanayotokea wilayani mkoani Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Dar es Salaam na Morogoro kukwama katika eneo hilo huku mamia ya abiria wakiwa hawajui hatma yao. Miongoni mwa viongozi walioathirika ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza akitokea Dar es Salaam, ambaye lilazimika kwenda kuzungumza na wananchi ili waruhusu magari yapite na hatimaye alifanikiwa.

  Barabara hiyo ilifungwa kuanzia kituo cha mafuta cha BP cha Michungwani hadi kituo cha mafuta cha Copec cha Segera. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Simon Sirro alikuwapo katika tukio hilo na kuwasihi wananchi kuondoa vizuizi na magari kupita kuanzia saa tisa alasiri. Aidha, magari kadhaa yameharibiwa kwa kuvunjwa vioo kwa mawe. Wananchi hao wamesisitiza kuwekwa matuta katika eneo hilo. Walihakikishiwa kuwa yatawekwa ifikapo saa mbili asubuhi leo hii.
   
 11. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi ajali kama hii zinapotokea serikali husema ni uzembe wa madereva. Ukiangalia vizuri, sababu kubwa ni uzembe wa serikali.

  Ajali nyingi ni za kuganga lori lililoegeshwa barabarani. Kukosekana kabisa kwa sehemu za kupaki pembeni mwa barabara ndiko kunafanya magari yaegeshwe barabarani.

  Barabara ya Dar hadi Tanga naijua sana. Haiwezekani kuegesha gari pembeni kwani hakuna pembeni. Ukiegesha gari lazima uegeshe barabarani. Ni nyembemba kupita kiasi, na haina parking shoulders.

  Uzembe wa serikali ulijitokeza tangu kwenye design. Ilibidi ziweko parking shoulders.

  Vile vile, uzembe wa serikali unajitokeza wazi wazi sehemu ambazo zimewekwa matuta. Ni wenda wazimu kuweka tuta barabara ya lami bila kulipaka rangi za kuhakiksha linaonekana kabla halijafikiwa.

  Chanzo kikubwa cha ajali za magari Tanzania ni uzembe wa serikali. Ni serikali mbovu.
   
  Last edited: Jan 12, 2009
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hivi kuna anayekumbuka 80's ile ajali ya mabasi ya Mzalendo na KAMATA?

  nilikuwa pale Hospitali kuu ya mkoa Morogoro... since then, kila ajali inapotokea na hatua zinazochukuliwa na serikali 'kuzimamoto' naona utani tu,...

  eti speed governors, mara seat belts,... vipi hayo malori yanayoharibika halafu yanaachwa kwenye highways? wanachukuliwa hatua kweli?
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  you are absolutely right, mpaka barabara zinazojengwa leo tatizo ni hilo hilo... ukiwa umekanyaga ghafla kwenye kona unakumbana na gari la mkaa lipo juu ya mawe, na kulia linakuja dala dala, inabidi kufunga macho tu... so sad.
   
 14. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuondoa tatizo hilo magari yote ya abiria yaendeshwe na trafiki kwa kushirikiana na kitengo cha chuo cha usafirishaji kwani wao wamesomea sheria za barabarani, mmiliki wa gari akishanunua apeleke maombi serikalini ili apatiwe dereva-ni maoni yangu mnasemaje???
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,873
  Likes Received: 83,351
  Trophy Points: 280
  Pia madereva hawataki kufuata sheria za barabara. Huyu dreva wa lori lililoegeshwa barabarani kwa maoni yangu inabidi akamatwe kwa makosa aliyoyafanya na huyo dreva wa bus kuna uwezekano mkubwa labda alikuwa katika speed kali sana na si ajabu haoni vizuri usiku hivyo anahitaji miwani ya kumsaidia kuona vizuri. Kuna haja ya kuwa na sheria kali za barabarani, na pia kupambana na askari wa barabarani wahuni ambao wanabasababisha sheria za barabarani kutoheshimiwa kwa uchukuaji wao wa rushwa.

  Tanzania watu wengi wanaendesha bila leseni hawajui chochote kuhusu sheria za barabarani na hata wale wanaozijua sheria hizi hawaziheshimu matokeo yake ndiyo hizo za ajali zisizokwisha zinazosababisha maelfu ya Watanzania kupoteza uhai wao kila mwaka au kupata vilema vya maisha.
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kuna ulazima kuwa na highway police patrols, kwa maana ya ku patrol ki kweli kweli, i.e after several kilometres wawe wanatega na "farasi weupe" wao kudhibiti nyendo kasi, magari mabovu mabarabarani, na madereva walevi... kinyume na hapo...!
   
Loading...