2025 Upinzani mkishindwa kuingia madarakani,miaka 100 CCM itakuwa madarakani

Udhindani wa sasa hauwezi kushinda kuchukua nchi Tanzania, ingawa ni muda sahihi sana watu wanahitaji altenaltive chama kingine kikubwa.

Ukweli ni kwamba hawana Uongozi, Sera,mikakati na wataalamu sahihi wa kuwasaidia kuunganisha Tanzania. Hilo Hata sidhani ni lengo lao.

Kuna wengi hawana vyama, wana CCM wasioridhika na mwenendo wa sasa. Mamilioni.

Wao wamekomalia kutukana nchi, Wasukuma wote, CCM wote, wote wasiounga hoja zao.

Mikakati sahihi ni kuungana nao, kuangalia na wapi tunakubaliana, tofauti zetu tunazikabili vipi.

Mfano issue ya Mbowe, matatizo ya sasa ya Maji, umeme, ajira , kodi, tozo, biashara, kilimo, wengi hawakubaliani na jinsi CCM inavyokabiliana nayo.

Hakuna kwa sasa kiongozi mwenye mashiko kama Dr Slaa anayeonyesha njia mbadala kutumia lugha sahihi, convincing language.
Mchaga achukue nchi? Aagh wapi
 
Mchaga achukue nchi? Aagh wapi

Haha, inachekesha kidogo. Unatukana kanda yenye watu zaidi ya milioni 20, wenye ushawishi mkubwa Tanzania nzima. Waliooa makabila yote sababu hawana ukabila wameoa sana tu uchagani, upareni, kaskazini, kusini, ukanda wa Pwani, Tanzania nzima.

Kanda yenye nguvu kazi, wachapa kazi, rasilimali lukuki. SSH, (Chifu Hangaya) ameenda kule mara tatu au zaidi, Mbowe campaign yake ya katiba mpya aliizindua pale.

Hawa wana akili, wanajua ukiungwa mkono kule, you are half way there.

Hapa ni kama kijiwe wakati mwingine, changamsha genge, uhahubiri kwa waumini badala ya kuvutia waumini wapya. Sasa kama waumini wenyewe ni 3m unachukuaje nchi ya watu milioni sitini.

Maths, strategies, honest, seriousness, humbleness, is what is needed.
 
Mchaga achukue nchi? Aagh wapi

Mchaga anaweza kupata Urais akiwa genuine Mtanzania yoyote anaweza kupata Urais.

Mrema 70% ya Watanzania wote walimwamini, walimkubali sababu ya kazi zake kabla, maneno yake, vitendo vyake.

Alikuwa kama JPM, alishugulika na Majambazi, wezi, mafisadi, rushwa, wahuni kweli kweli.

Sera zake zilikuwa kuondoa uhuni, ufisadi uliotamalaki wakati wa Mzee ruksa. Nyerere pia alimuunga mkono usalama na Polisi walipotaka kumuonea.

Nasikia alishinda ule uchaguzi figisu zikafanyika, hakuwa mdini, mkabila, mkanda. Alijiona ni Mtanzania.
 
Back
Top Bottom