2025 ni mwaka wa historia, upinzani wanakwenda kuchukua madaraka ya utawala. Kwa Mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa taifa hili

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,829
3,824
Kwanza nianze na chama tawala CCM, kwa hali ilivyo hadi sasa si shwari ndani ya chama cha CCM, kuna mpasuko mkubwa ,mpasuko huu umesababishwa na kutofautiana kiitikadi na misimamo. Kundi la kwanza ni lile lililokuwa kinyume na JPM, hili kundi lilikuwa halikubaliani na sera ya kujitegemea ya JPM, na kundi la pili ni lile ambalo lilikuwa linaunga mkono itikadi ya kujitegemea!

Samia pia, japo alikuwa ni miongoni mwa wapiounda serikari iliyopita lkn hakuwa muumini mwaminifu wa sera ya kujitegemea, hili limejidhihirisha baada ya Ndugai kutoa mawazo yake kuhusu kukopa na agenda ya kujitegemea, sote tuliona namna sakata hili lilivyoenda, hadi kupelekea Ndugai kushinikizwa na baadhi ya wabunge na wanachama wake ajiuzuru, akiwemo mwenyekit wake wa chama.

Mpasuko huu, hakuna namna tena ya kuuziba, kwani chama kwa sasa kina irani mbili tofauti, zinazopingana, na kwakuwa mwenyekit ndo mwenye mamlaka na nguvu ya maamuzi ndani ya chama, analazmisha sela yake ifuatwe, kitu ambacho ni kigumu kwani irani ya CCM iliyopo na inayofahamika na wote ni ile aliyoiacha JPM.

Kitu kinachotia hofu ni kuwa ilani ya CCM aliyoiacha JPM, iliwashika au niseme ilikubalika na wengi ndani ya CCM, kuliko wachache walioiona haifai. Hii inatupa picha kwamba mama anakundi dogo sana linalokubaliana na sera yake ndani ya CCM, na nje ya CCM, kibaya zaidi wanaopingana na sera ya samia ndani ya CCM, wananguvu sana ndani ya CCM na nje ya CCM, na wanakubalika kwa wapiga kura wengi, na hili ndo linalompa homa samia namna atakavyopenya 2025.

Kwanini nasema 2025 ni historia kwa upinzani kuchukua madaraka?

Iko wazi samia anajaribu kutumia dhamana aliyonayo kuwapunguza wale ambao anaona wako kinyume naye,na pia wananguvu na ushawishi ndani na nje ya CCM, sasa ikiwa atafanikiwa kuwafagia anaoona wanampa headache, na kimsingi hao ndo wanaowapa hata upinzani headache kwa uchaguzi wa 2025.

Kwa picha hii ,upinzani endapo dua lao likawa kweli ,la kuingia kinyang'anyilo na samia basi,njia kwao ni nyeupe ya kuchukua utawala,ikumbukwe ilani ya CCM aliyoiacha na ambayo tunaamini mpaka sasa ndio inayotambulika na CCM, mengi yalikuwa niya chadema, sema JPM aliwawahi akayaingiza yote ndani ya ilani ya CCM, na hapo chadema wakajikuta wanakosa mahali pa ku challenge na kutafuta ushwawishi kwa wananchi,mbowe pia aliwahi kukiri hili mwanzoni kabisa mwa utawala wa jpm.

Samia kwa kuwa sasa, si muumini wa ilani ya CCM iliyoachwa na ambayo inayotambulika na wanachama wote ,basi ni fursa kwa chadema na wapinzani, kuvuna, kundi la wana CCM ambao ni waumini wa sera ya inayopigwa vita na samia. Mpaka hapo upinzani njia ni nyeupe kabisaa kuchukua madaraka ya utawala.

Nawatakia kilalakheri upinzani!
 
Calm down.

Madaraka yanaweza yakabaki CCM ila siyo kwa macho malegezo.
 
Nimeacha kusoma baada ya kukuta umeandoka Irani badala ya Ilani

Nikajua hapa najaziwa matope kichwani kwangu
 
Haya mambo ya kujazana matumaini hewa kwenye hakuna, hayana maana

Siipendi CCM na ngependa ife hata leo, lakini kwa sasa hakuna mbadala wake kwa nchi yetu. So sioni hiyo 2025 upinzani wa kuiondoa fisiem madarakani
 
Acha kuota ndoto zakipuuzi, upinzan kuja kuchukua hii nchi wasahau, wamekosa dira ya chama, wamekosa maono wao kila siku wako bize kujadiri hotuba za rais na kumnanga ndugai huko clubhouse na spaces za Maria.

Sas unazan kwa tabia hii watafanya mambo yao yatakayo washawishi wananchi saangapi?

Acha ccm ivunjike mybe tunaweza pata mtu bora tokea ktk mvunjiko wa ccm, lkn kwa upinzan huu wa akina lema na mdude nyangari, hiyo sahau mjomba, kwanza ccm japo hawapendan lakini kamwe hawawez ruhusu rungu la urais lichukuliwe na mpinzan, watatumia kila njia kuushika urais.

Acha kuota mchana
 
Back
Top Bottom