2024 US Election Results: Too Big To Rig, Really?-Makubwa Haya!

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
24,689
24,717
Salaam wanajamii na hasa wafuatiliaji wa jukwaa hili.

Ni jana tu tumepata matokeo ya uchaguzi ya ndugu zetu wa Marekani, ambapo Trump, Donald aliibuka Kidedea. Sema nimeshangazwa kwa nini jukwaa hili halikuchangamkia uchaguzi wa mwaka huu wa Marekani! Wadau wataeleza.

Trump apongezwe kwa ushindi huu ukizingatia yale aliyopitia. Mbali na matokeo haya, nimevutika kufuatilia zaidi mfumo wa uchaguzi wa Marekani. Tumeambiwa mara nyingi kuwa sehemu ya kupigia mfano katika kuendesha chaguzi ni Marekani. Wasemaji wana sisitiza kuwa mfumo wa uchaguzi wa Marekani hauna dosari, na hakuna namna unaweza kuchezea mfumo huo kubadili matokeo. Hata hivyo, wakati natafuta habari zaidi juu ya mfumo wa uchaguzi wa Marekani, nikakumbana na na video ya kipindi cha Trumpet Daily kikiwa na caption ya too big to rig! Kwa tafsiri isiyo rasmi ya kiswahilini kuwa ushindi wa Trump ulikuwa mkubwa kiasi ilikuwa vigumu kuchakachua matokeo.

Kwa maelezo ya kwenye video inaonyesha kuna uwezekano mkubwa mfumo wa uchaguzi wa Marekani unachakachulika. Nawakaribisha wasisitizaji wa kuwa mfumo wa uchaguzi wa Marekani hauchakachuliki kunishawishi tena, maana kwa video hii , nimerudi nyuma sana katika kuamini umadhubuti wa mfumo wa uchaguzi wa Marekani kutochakachulika.

Karibu.
Link ya video hii hapa:
View: https://rumble.com/v5md5tq--trumpet-daily-11.6.24-9pm-est.html?e9s=rel_v2_ep
 
Back
Top Bottom