Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,600
Wahenga wanasema, ‘’siasa ni maisha, lazima uyaishi’’. Kwa namna moja ama nyingine, siasa itashawishi mtindo na mwelekeo wa maisha yako. Yaweza kuwa mwelekeo wa peponi wa kukenua meno ama yaweza pia kuwa mwelekeo wa maisha ya kuzimu ya jasho la damu.
Kuna nchi tumeshuhudia zilikuwa na maisha ya furaha, amani, na maendeleo lakini kutokana na matokeo ya maisha ya siasa mambo yamebadilika kwa haraka. Nchi kama Venezuela, ambayo kwa wakati mmoja iliwahi kuwa nchi yenye uchumi mkubwa America ya Kusini lakini leo hii imedumbukia kuzimu. Zimbabwe na Libya hali kadhalika kwa wakati mmoja zilikuwa nchi zilizopigiwa mfano hapa barani Afrika.
Hiyo ni mifano ya namna gani mambo katika nchi na raia wake yanaweza kubadilika ndani ya kipindi cha mda mfupi. Na ubaya wa kuogofya ni kwamba katika nchi hizi zote, ilichukua mda mchache sana kuanguka kwenda kuzimu, na tangu waanguke ni miaka sasa hawana dalili za kuinuka tena. (Hili tuliweke akilini)
Madhila yaliyowakuta Venezuela, Zimbabwe, na Libya ni sababu zinazofanana. Na nchi zote hizo ziliadhibiwa bila huruma na viranja wa dunia baada tu ya viongozi wao wa kisiasa na serikali zao kuonesha vitendo ambavyo vilitafsiriwa na viranja wa dunia kama ukiukwaji wa haki za binadamu.
Ni ukweli usiopingika, kwa namna mambo yanavyojidhihirisha kwa sasa, Tanzania na sisi kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, tupo katika rada ya viranja wa dunia. (Hakuna wa kupinga hili) Tupo katika rada ya kuelekea kushughulikiwa kama zilivyoshughulikiwa nchi nilizozitaja hapo juu. (Kwa maoni yangu).
Kwa sasa viranja wamejipanga kila idara, kikubwa kinachongojewa ni uchaguzi wa October 2020. Wenyewe wameshajua kwamba ni vigumu uchaguzi ukawa wa haki na usawa, hata sisi watanzania wengine tunajua kwamba uchaguzi hauendi kuwa wa haki na usawa. (Nadhani pia ndo mana wamenza kuzikoki bunduki zao mapema tayari kutulenga).
Wapinzani wenyewe wanajua hatuendi kuwa na uchaguzi huru, haki na usawa, kwa hiyo nahisi kinachofanyika; wanaenda kuwa chambo ya kudhihirisha dunia ni namna gani Tanzania inavovunja haki za binadamu.
Mbinu za kushughulikiwa ni zile zile za kibepari ambazo matokeo ndo yataleta shuruba kwa maisha ya watanzania.
Ni dhahiri usipojipangwa lazima hii 2021 ikupange. Mabepari hawana huruma, wanataka wakianza kupiga dunia ishuhudie, na dunia haiwezi kushuhudia kama Raia hawatoki jasho la damu.
Niwalaumu tu viongozi wetu moja kwa moja kwa kutuingiza kwenye hii madhila, Iwe iwavyo, fikiria kwa vyovyote, Viranja wa dunia wanataka regime change Tanzania, wasipoipata regime change lazima watafute namna tushughulikiwe.
Huku na huku wakina Bibi Kidawa Manzese wanakuambiwa CCM Mbele kwa Mbele. Hivi akina Bibi Kidawa wanajua viranja wa dunia wamepanga kitu gani?
Nipo kujiandaa na 2021
N.Mushi

- Kwanza kabisa, vikwazo vya kibiashara havikwepeki,.. (Nachoka akili nikifikiri kwamba tukizuiwa kuuza madini na mazao) tutapataje fedha za kigeni.. (KIZA KINENE)
- US na EU wanaweza kuzuia raia wao kuzuru Tanzania ( hapo utalii ndo mwanzo wa mwisho).. Hii ilifanyika ZIMBABWE na kwetu itaweza fanyika pia
- Misaada yote ya donnors pia ndo inapata ground za kukatwa moja kwa moja kwa kigezo cha ukiukwaji wa haki za binadamu.
- Moody’s lazima waingie kazini halafu waanze kusema wamei downgrade Tanzania. (Ikumbukwe nchi ikishakuwa Downgraded means hapo inakuwa ngumu hata kupata mikopo nje ya nchi maana wanakuambia risk of default inakuwa ni kubwa)
- Hii reserve yetu kiduchu ya dola nadhani ndo itatuumbua mapema sana, mambo yakishakuwa hovyo demand ya dola itaanza kuwa kubwa, hao makabachori wana passport mbili mbili huwez kuwaona bongo tena watataka ku change mipunga yao wapeleke kwenye dola watimke mpaka mambo yatapokaa sawa. Hapo sasa ndo kimbembe unaweza shangaa mwezi wa 12 dola ishafika 3000.
- Dola ikianza ku shoot inflation na yenyewe inaanza kuitikia ni pua na mdomo ( Jiuulize ni kwanini nchi kama Venezuela, Zimbabwe soon baada ya kushughulikiwa ni kwanini inflation zili shoot sana?)
- Hapo tusiombe machafuko, maana yakitokea, ICC wapo hapo matakoni yaani ni shida kila idara.