2021 tujifunze kuwa na nidhamu binafsi

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
340
300
Tupo mwanzo wa mwaka mioyo yetu imejawa na matumaini na imani kubwa kwamba mwaka huu mabadiliko yanaenda kutokea maishaini mwetu.

Kawaida mwanzoni mwa mwaka kila mmoja wetu hupanga mipango huku akiwa na malengo ya kufikia hatua flani maishani.

Inawezekana una mipango mingi na mizuri lakini napenda kukukumbusha kama utakosa nidhamu binafsi ni vigumu sana kufikia malengo yako uliyoniwekea kwa mwaka huu.

Maana ya nidhamu binafsi ni uwezo wako wa kudhibiti hisia, mawazo, na tabia zako mbele ya vishawishi na misukumo unayokutana nayo kila siku.

Nidhamu binafsi ni kiuanganishi bora cha mafanikio na mipango yako.

Kwa mfano, mwanzoni mwa mwaka jana matumizi yangu ya bundle(MBs) kwa yalikuwa yana nigharimu kati ya shilingi 7k mpka 10k kwa wiki.

Ilikuwa hivi, nilitumia muda mwingi kuangalia video za mpira, muziki pamoja na kusoma habari za wasanii Instagram.

Kadri siku zilivyokuwa zinaenda gharama ziliongezeka na kujikuta napoteza muda mwingi kwenye mambo ya kijinga huku kila siku mambo yangu mengi ya msingi ya kikwama.

Nakumbuka ilipofika mwezi wa tatu, nilifanya tathmini binafsi na kugundua sipo katika njia sahihi na something must be done.

Nilijiuliza kwanini nina matumizi makubwa ya Mbs huku sifanyi biashara mtandaoni?

Niliweka mipango mikakati ya namna bora ya kutumia Smartphone pamoja na muda wangu.

Mkakati wa kwanza niliojiwekea ulikuwa kutokuingia online ninapoamka mpaka pale ninapomaliza kufanya shughuli zote za asubuhi.
Kuanzia pale nilijikuta naweza kuwasha data saa sita mchana huku tayari nimekwisha fanya mambo yangu ya msingi.

Mkakati wa pili nao ulikuwa ni ku-unfollow baaadhi ya wasanii na pamoja na watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii (Instagram) pamoja na kuacha kuangalia kile video ninayoikuta YouTube.

Sambamba na hiyo nilianza ku-follow watu ambao naweza kujifunza na kupata taarifa muhimu ya mambo yanayoendelea duniani.

Hatua hii ilinisaidia kupunguza muda ninaotumia kwenye mitandao ya kijamii pamoja na kujua mambo muhimu yanayoendelea duniani.

Baada ya kupunguza muda mwingi ulikuwa unapotea kwenye mitandao ya kijamii pamoja na kuokoa fedha nilijikuta kwenye muda wangu wa ziada akili imetulia na kufikiria mambo ya msingi kuhusu maisha.

Tokea pale niliweka ratiba ya kutumia angalau saa moja kwa siku kusoma vitabu pamoja na kuandika makala mbalimbali kuhusu maisha, uchumi pamoja na siasa.

Ndugu zangu, nidhamu binafsi ina umuhimu na nguvu kubwa kuliko hamasa kutoka kwa watu wanaotuzunguka na ndiyo njia pekee ya kutuwezesha kufanya yale tuliyoyapanga kwa mwaka huu.
 
Hiyo ya ku-unfollow watu insta niliifanya mwaka Jana, saiz sijafollow watu zaid ya 20.
Azam sports 2, jamii forums, na shafii dauda (ONLY 3) ndo pekee niliowategeshea kwa ajili ya taarifa mbali mbali za ndani na nje.

Saizi bundle siweki kihasara hasara kutokana na kwamba:
1 Kuna free basics
2 sitengenezi hela mtandaoni
3 mitandao imekuwa wezi
 
Hiyo ya ku-unfollow watu insta niliifanya mwaka Jana, saiz sijafollow watu zaid ya 20.
Azam sports 2, jamii forums, na shafii dauda (ONLY 3) ndo pekee niliowategeshea kwa ajili ya taarifa mbali mbali za ndani na nje.

Saizi bundle siweki kihasara hasara kutokana na kwamba:
1 Kuna free basics
2 sitengenezi hela mtandaoni
3 mitandao imekuwa wezi
Jambo jema sana ndugu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom