2020 Wacha waseme wewe Fanya

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,435
5,404
Leo tunaanza Mwaka 2020

Ni mwaka mpya.Kuna wanaofikiri kwamba ni tarehe u imebadilika na ni siku kama siku nyingine.Na kuna wanaofikiri tofauti.Kwa wajasiriamali na wale wanaotamani kuwa na Utajiri au kuwa mamilionea au kuwa na Uhuru wa kifedha kila siku mpya ni siku tofauti na ambayo inafaida zake.

Leo nataka nizungumzie kitu kimoja na cha kipekee kabisa ambacho kina thamani ya zaidi ya milioni 100.Msingi wa hoja ni huu,(Wacha Waseme wewe Fanya).Lengo la somo hili ni kukuwezesha wewe kuingiza katia ya TZS milioni moja hadi milioni 10 ndani ya siku thelathini hapo ulipo kwakufuata muongozo sahihi nitakaokupa wa siku kwa siku.Mada hii pia inaweza kuwa Tengeneza milioni 10 ndani ya siku 30 au tengeneza milioni 1 ndani ya siku 30.

Kabla ya kuendelea kusoma ningependa ufahamu kwamba elimu hii naitoa bure lakini ina gharama kubwa.Inaweza kuwa na gharama kubwa kwako zaidi kuliko kwa mu mwingine yoyote yule hivyo basi ni muhimu ukahakikisha unaelewa thamani yake kabla ya kuanza kuifanyia kazi.Usianze kuifanyia kazi iwapo uoni thamani yake.

Andiko hili peke yake linauzwa kati ya TZS 2500 hadi 25000 likiwa pamoja na support ila hapa JF nimeliweka sio ulitumie bure bila kulipia bali utakapoona lina kufaa na unataka kulitumia basi kabla hujaanza kulifanyia kazi uhakikishe kwamba unatafuta namna ya kunilipa mimi kwa kukupatia andiko hili.Kama umepatiwa andiko hili na mtu mwingine msisitize akuambie alikolipata na jinsi ya kulipia.Ukilipia kabla ya kutumia andiko hili unawezak ulipa katia TZS 2500 hadi TZS 25000 tu.Ukilipia baada ya kulitumia na ukaona matokeo yake tafadhali hakikisha unalipa 20%(asilimia ishirini ya chochote utakachopata)

Najua kuna sauti inakuja kwenye akili yako,wameanza kusema ila wewe waache wao waseme wewe FANYA ndipo utaona matokeo yake.Ni kawaida yao kusema.Wazo hili unalitekeleza huku ukiwa huna pesa yoyote taslimu mkononi wala ukiwa huna namna yoyote ya kupata pesa taslimu hata kwa mkopo wa marafiki bali unatakiwa uanze na ulicho nacho.Ila hakikisha ulicho nacho ndicho utakachohitaji kwa ajili kutimiza lengo lako.Sasa nianze moja kwa moja na melezo kamili ya wazo lenyewe.

SIKU YA KWANZA:JENGA WAZO LAKO NA JENGA PICHA KAMILI YA WAZO LAKO(THINK THROUGH AND VISUALIZE YOUR IDEA)
Katika siku hii kazi yako ni moja tu kufikiri na kujenga picha.Fikiri kwa umakini sana.Fikiri wazo lako katika ukamilifu wake,fikiri jinsi utakavyo litekeleza kwa ukamilifu wake,fikiri changamoto za kulitekeleza,fikiri jinsi ya kuliuza,jinsi ya kupokea malipo jinsi uatakvyotumia pesa utakayopata na jinsi utavyofurahia wazo lako baada ya kukamilika.Fikiri kwa umakini na tumia hata saa zote 24 kufanya jambo hili.

Kumbukua unapotumia muda wako mingi kuwaza jambo kwa umakini na uzamifu basi unajipa nafasi kubwa ya kulifanya na kufanikiwa.Hivyo basi jipe muda wa kutosha kuliwaza kwa uhakika wazo lako.Usiogope ukubwa wa wazo lako wala usiogope udogo wa wazo lako.Usiogope udhaifu wa wazo lako wala usilione kwamba ni wazo gumu.Hakikisha unalifikiri kwa umakini.

Andika baadhi ya mambo muhimu kuhusu wazo lako ili usiyasahau.Kumbuka wazo lako ni muhimu sana na yote unayowaza yana msingi katika kuhakikisha kwamba unafanikiwa.
Wazo ninalofikiri kulifanya mimi ni la kuandika kitabu kinachohusu kitu ninacho kifahamu sana.Kitu ambacho ninafahamu taarifa zake kwa uhakika,kitu ambacho ninaweza kupata taarifa zake kwa urahisi na kwa uhakika.Unaweza kuandika kuhusu magonjwa ya kina mama iwapo unaufahamu nayo na unaelewa tiba mbadala kuyahusu na unaweza hata kuandika kuhusu jambo lolote ambalo unaona kabisa kwamba watu watakuwa tayari kununua na kujifunza kuhusu jambo hilo.Unaweza pia kuandika kuhusu malezi ya familia,unaweza kuandika jinsi ya kutambua vipaji vya watoto na kuvilea,na unaweza kuandika juu ya tiba lishe na lishe kwa ujumla.

Kumbuka lengo lako ni kuingiza katia TZS milioni 1 hadi 10 hivyo kitabu chako unaweza kukiuza kati ya TZS 1500 kwa nakala hadi TZS 5000 kwa nakala.Lengo lako ni kuuza kati ya nakala 1000 hadi nakala 10,000 na utalenga kuwauzi watu katika mfumo wa nakala ngumu(Print) na Nakala line(Soft copy).Hakikisha kwamba Bei ya Nakala Laini inakuwa kubwa kuliko bei ya nakala Ngumu(Actual Price) hivyo ni muhimu ukafahamu hilo ili kuhakikisha kwamba andiko lako linakuwa salama(SIO LAZIMA)

SIKU YA PILI:UTAFITI WA SOKO NA MFUMO WA KUUZA(MARKET RESEARCH AND SALES METHOD?CHANNEL)

Katika siku hii ya pili lengo lako ni kufanya utafiti wa masoko.Katika kufanya utafiti wa masoko unaangalia kama kuna bidhaa/kitabu kinachofanana na chako kilichopo sokoni au kama kuna watu wanafanya kazi kama ya kwako ya uandikaji wa vitabu pepe( E books) ni jinsi wanavyotengeneza pesa.Ni muhimu sana kufahamu kabisa juu ya soko lako.Katika hatua hii ni lazimi uchague watu utakao wauzia mfano:KANISANI KWAKO,MSIKITINI KWAKO,SHULENI KWAKO,OFISINI KWAKO na HATA KWA MAJIRANI NA RAFIKI ZAKO na HATA ndugu zako.

Katika kila kundi hapo juu hakikisha kwamba unafahamu idadi ya watu katika kundi lengwa,kisha wewe lenga kuwauzi angalau 10% ya watu wote kwenye kundi husika.Mfano kama ofisini mpo watu 20 basi wewe lenga kuuzia watu wawili.Ukikokotoa utapata kwa hakika idadi kamili ya watu ambao unataka kuwauzi na hao ndio utawatumia kuamua bei ya kitabu chako kwa kuzingatia gharama za kukiandika.Mfano kama utapata kwamba 10% ya watu kutoka makundi yote jumla yake ni watu 200 basi hio ndio target market yako na hivyo ukishaamua kuhusu gharama za kuzalisha vitabu utawatumia kuamua gharama ya kuuza.Ni muhimu sana kuwa na target Market.

SIKU YA TATU:TENGENEZA ORODHA YA UTAKAOWAUZIA KWANZA (PRE RELEASE SALES LIST)
Hii ni orodha ya watu wa mwanzo ambao utawauzia bidhaa au kitabu chako.Ni muhimu sana ukahakikisha kwamba hawa ni watu ambao unaelewa kipato chao,mtazamo wao,uwezo wao kifedha,na utayari wao wa kukuunga mkono.Hawa ndio watakuwa watu wa kwanza kabisa kukona kitabu chako na ambao pia watakupa mrejesho juu ya ubora wa wa kazi yako.

Orodha hii hakikisha ni ya watu ambao utakuwa na emails zao,namba za simu na unafahamu wapi ulipo na itapendeza ikiwa pia na wao wanakufahamu vizuri ila sio lazima

SIKU YA NNE HADI YA SITA :ANZA KUKUSANYA TAARIFA ZA ANDIKO LAKO(FANYA UTAFITI WA ANDIKO LAKO)
Hapa ndipo unaanza kufanyia kazi andiko lako na usiwe mvivu.Tumia mitandao,vitabu na uzungumze na watu wenye maarifa ya kutosha ili upate taarifa za kutosha.Zungumza na watu ambao wana taarifa sahihi kuhusu eneo husika na hakikisha unatumia nukuu sahihi ili kuongeza mvuto na umakini katika kazi yako.

Andaa kabisa mpangilio wa kazi yako,mtindo wa uandishi na uhakikisha unakuwa na mtindo ambao ni rahisi kufuata,unaoeleweka kulingana na hadhira yako.Kumbuka kitakachofanya andiko lako liuzike sana na urahisi wa kusoma na kueleweka na utajiri wa maarifa yatakayopatikana kutoka na andiko lako.Hivyo basi ni muhimu ukachagua kichwa/Title au Jina ambalo linavutia mtu kutaka kufahamu zaidi na linalogusa hisia kwa undani.Pia ni muhimu ukahakikisha kwamba mpangilio wa kazi yako una mtiririko mzuri na wenye urahisi wa kusoma na kueleweka.

SIKU YA SABA HADI YA KUMI:ANZA KUANDIKA KAZI YAKO KWA KINA NA UMAKINI

Katika hatua hii ndio unaandika andiko lako kwa kina kabisa na kwa umakini.Hakikisha unatumia kwa usahihi taarifa zote ulizokusanya katika siku ya nne hadi ya sita katika kukuongoza katika uandishi wako.Usiibe andiko la mtu na kulitumia bila kuonyesha umenukuu kutoka wapi kwani unaponesha nukuu unakuwa umeheshimu yule aliyeandika na pia unakuwa umejijengea heshima wewe mwenyewe.

Si lazima kazi yako iwe ni kurasa nyingi au maarifa mengi.Hakikisha unampa mtu maarifa yale tu anayohitaji na yatakayomfaa.Faida za kuwa na andiko jepesei kueleweka na kufanyiwa kazi ina maana watu wengi watasoma andiko lako na kukupa mrejesho wa kina.REJEA andiko hili.
Unapoandika kitabu chako kiwe katika mfumo wa A4 ila iwapo unataka kukichapa kwenda hardcopy utabadili format kulingana na mahitaji ila ni muhimu kabisa ukahakikisha kwamba andiko lako linakuwa katika mfumo wa A4 kwa itakuwa ni rahisi hata kwako wewe kuandika.

Unapoandika kumbuka kwamba unachoandika sio kitu ambacho hukifahamu na kukielewa.Ni kitu unachokifahamu hivyo basi unapoandika ni muhimu kabisa ukahakikisha kwamba huandiki mambo mengi magumu bali unaandika mambo ambayo yanaeleweka kwa urahisi na yanaweza kumafnya mtu atake kujifunza zaidi.

SIKU YA KUMI NA MOJA :KUHAKIKI KAZI YAKO-PROOF READING
Katika hatua hii unachofanya ni kusoma kazi yako kwa umakini kama mtu ambaye anasoma kitabu hicho kwa mara ya kwanza.Unaposoma unakuwa unaangalia kama kuna maeneo ambayo yana makosa ya kisarufi au kimantiki.Unaweza kuanza kurekebisha mara moja ila hakikisha unakuwa na nakala mbili za kazi yako.Moja ni nakala ya kwanza na nyingine ni nakala yenye marekebisho.Umuhimu wa nakala hizi ni katika kuhakiki ubora wa kazi yako

Unaweza pia kumpatia mtu ambaye unafikiri anaweza kufanyia uhakiki kazi yako ili na yeye apitie na kufanya uhakiki wa kina wa kazi yako.Uhakiki ni muhimu kwa sababu unakusaidia unapokuwa unapeleka kitabu chako sokoni kisiwe na makosa mengi.

SIKU YA KUMI NA MBILI:UHAKIKI WA MWISHO NA MPANGILIO

Katika hatua hii unachofanya ni kuweka mpangilio mzuri wa kazi yako kwa ajili ya kupeleka sokoni.Hakikisha kunakuwa na COVER PAGE NZURI,TABLE OF CONTENTS INAYOELEWEKA,UTANGULIZI,NUKUU,FAHRASA,MAELEZO YA HATI MILIKI na kama unaweza JIPATIE ISBN numbe kwa ajili ya kurajisi kijitabu chako.WEKA MAWASILIANO Yako YOTE MUHIIMU KATIKA KITABU CHAKO

SIKU YA KUMI NA TATU:MTEMBELEE MPIGA CHA(VISIT A PRINT SHOP)
Tembelea au wasiliana na mpiga chapa mjadiliane kuhusu gharama,muda na mfumo wa uchapaji wa Kitabu.hakikisha unakuwa na gharama za nakala chache na nakala nyingi.Hakikisha unakuwa pia na gharama ya nakala moja na pia ufahamu muda anaotumia katika kukamilisha kazi.

Negotiate the best deals kulingana na budget yako pamoja na lengo lako na ukiona kama gharama haziendani na malengo yako jaribu kuongea na Mchapaji mwingine huku pia ukirekebisha hesabu zako ziendani na gharama husika.

SIKU YA KUMI NA NNE HADI KUMI NA TANO:TENGENEZA TOVUTI MAALUM YA KITABU CHAKO(BUILD A WEBSITE FOR YOUR BOOK

Tengeneza website
maalum kwa ajili ya kitabu chako na hakikisha kwamba inakuwa na taarifa maalum kama vile muhtasari wa kitabu,gharama za kitabu,namna ya kukipata n.k.

SIKU YA KUMI NA SITA:WATUMIE EMAIL WATU WA PRE RELEASE LIST
Watumie watu wako uliowaweka katika orodha yako siku ya tatu ukiwajulisha kwamba umeandika kitabu chako kuhusu somo fulani ni kwamba wao ni moja kati ya watu wachache ambao wanaweza kupata fursa ya kuwa wa kwanza kabisa kusoma kitabu hicho kwa bei ya punguzo.Unaweza kuwapa punguzo hata la 50% kulingana na bei yako na gharama zako.Hakikisha unawapa mwisho wa ofa yako kwao na kwamba wakitaka kununua wafanyeje,mfano watume PESA,Wapige simu,Wajibu email kwa maelekezo zaidi etc.

Kumbuka unapotuma email hii tayari umeanza kuuza na hivyo basi hakikisha unakuwa mwepesi katika kuhakikisha kwamba unawahudumia wateja wako vizuri kwa kutazama emails zako mara kwa mara na kuwasidia ipasavyo

SIKU ya KUMI NA SABA HADI ISHIRINI:TEMBELEA MADUKA YA VITABU,BOOKSHOP
Tumia siku
hii kuwatembelea wamiliki wa maduka ya vitabu kuwajulisha kuhusu kitabu chako hicho,bei yake ya kununua/JUMLA na REJA REJA na unaweza kuwapa website wakitazama wataelewa zaidi.

SIKU YA ISHIRINI HADI ISHIRINI NA TATU-TEMBELEA VYOMBO VYA HABARI (REDIO,TV,MAGAZETI)
Katika vyombo vya habari jaribu kutafuta iwapo kuna kipindi ambacho kinazungumzia lile suala ambalo umeliandikia kitabu ili wawez kukupa nafasi ya kuzungumza(AIR TIME) au kukupa collum uandike makala.Vyombo vingi vya habari vinaweza kukupa nafasi bure iwpo wataona taarifa yako itawapa wasikilizaji wao maarifa mapya

SIKU YA ISHIRINI NA NNE HADI ISHIRINI NA NANE

Te
mbelea walengwa wako uliowatambua katika siku ya pili ili kuwajulisha pia kwamba kuna bidhaa mpya kwa ajili ya huku ukiwaleza jinsi ya kukipata,gharama na kuwapa jina la tovuti ya kitabu chako kwa melezo zaidi.Kulingana na makubaliano yako na mchapaji unaweza kuwa na nakala unazotembea nazo kwa ajili ya kuziuza kwa wale watakaotaka kununua PAPO kwa HAPO

SIKU YA ISHIRINI NA TISA HADI THELATHINI

Hizi ni siku za kufanya tathmini na kuangalia muelekeo wa mradi wako na iwapo kila kitu kinaenda sawa huku ukitazama jinsi order za kitabu chako zinavokuja.Unaweza pia kuwasliana na wateja ambao ulisha zungumza nao ili kuwafahamisha kwamba kitabu kipo tayari ili muweze kufanya biashara.Ni muhimu ukahakikisha kwamba.Unafuatilia kwa umakini taarifa za mauzo yako ili kufahamu iwapo una kipato cha kutosha kulingana na lengo lako.

MWISHO.

ANDIKO Hili ni sehemu ya KITABU kiitwacho,VUNJA MWIKO,FANIKIWA KATIKA UJASIRIAMALI NA BIASHARA ambacho kinamaandiko mbalimbali ya kibiashara,simulizi za wajasiriamali waliofanikiwa,changamoto za kibiashara,michanganuo pamoja na miongozo ya kibiashara ambacho kiko jikoni kinapikwa.KITABU hiki kitapatikana kwa gharama ya TZS 7500 kitakapokuwa tayari katika mfumo wa EBOOK.Iwapo ungependa kuwa wa kwanza kukipata tafadhali tuma EMAIL kwenda masokotz@yahoo.com

NAKUTAKIA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO.


Iwapo ungependa kuchangia kiasi kidgo cha PESA katika uandishi wa makala kama hizi basi tuwasiliane kwa ajili ya kupatiwa namba ya malipo unayoweza kutumia.ASANTE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom