2020 KIZURI CHAJIUZA...

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Wanajukwaa,

Mtifuano wa kisiasa uliopo uwe wa kutengenezwa au halisi, umenikumbusha methali ya kiswahili "KIZURI CHAJIUZA NA KIBAYA CHAJITEMBEZA".

Ukiona katika familia fulani paka kalala katikati ya mafiga au njia ya kwenda toilet imeota magugu, huna haja ya kuuliza, "je, kuna uhai hapa?"

Methali hii ni HUKUMU kwa mwaka 2020; ama tuendelee na MTAWALA/UTAWALA uliopo au TUMPE MWINGINE.

Wewe kama mpiga kura, je, hizi ahadi za JPM wakati wa kampeni mwaka 2015, ni ahadi zipi zimetekelezwa ndani ya miaka 3 tukiwa tumesalia na miaka 2 tu?

1. Kutoa ajira

2. Kutoa milioni 50 kila kijiji.

3. Kujenga viwanda vya kilimo, mifugo uvuvi na madini.

4.. Kuleta pembejeo za kilimo kwa ajili ya wakulima.

5.. Upatikanaji wa majisafi na salama kwa 95% mjini na wananchi wa vijijini 85%.

6. Kujenga vituo vya afya, zahanati na hospitali katika maeneo mbalimbali.

7. Kumaliza tatizo la ukosefu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu

8. Kupandisha mishahara, vyeo, madaraja na stahiki mbalimbali.

9. Kujenga barabara za lami zinazounganisha mikoa nchi nzima pamoja na barabara za juu kwa Dar es Salaam.

10. Kujenga reli ya kisasa kwa viwango vya Standard Gauge na kuboresha bandari na usafiri wa anga.

11. Kukomesha ujangili.

12. Kulinda masilahi ya wafanyabiashara. Wafanyabiashara wadogo na wakubwa wote watalipa kodi.

13. Kulinda uhuru wa habari na wanahabari.

14. Wasanii kupewa hakimiliki na wao pamoja na wanamichezo kuanzishiwa mfuko kwa ajili ya kuwasaidia katika mambo mbalimbali.

15. Kuanzisha mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi.

16. Kuhakikisha mama lishe hawabughudhiwi.

17. Kulinda Muungano na usalama wa nchi.

18. Kutoingilia utendaji kazi wa Bunge na Mahakama.

19. Kuheshimu mawazo ya vyama vingine vya siasa.

20. Kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama.

21. Kuendeleza uchimbaji wa madini.

22. Kutoa elimu bure hadi kidato cha nne.

23. Kusimamia nishati ya gesi.

24. Kuwasaidia walemavu.

Tusidharau watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa uchache wao, hao ndio wanaweza ku-mobilize wengine na hatimaye kumwinua au kumwangusha.
 
Hapa kwenye viwanda sijui watakuja na story gani 2020.

Labda tumsubiri Mengi na hivyo vya simu na magari.
 
Tunamtaka kiongozi anaejuwa kuongea kingereza na mataifa makubwa duniani
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom