2020 CHADEMA watalazimika kumuomba tena mzee Lowassa awe mgombea wao wa urais kwa sababu za kifedha

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,750
139,549
Kwa sasa Chadema imekuwa kama timu ya Yanga hali yake kifedha si shwari na inaishi kwa kutegemea ruzuku ya serikali.
Kutokana na ukweli huo wagombea wote wa chadema iwe wa udiwani, ubunge au urais itawalazimu kujigharamia gharama za kampeni, chama kinaweza labda kutoa bendera.

Kwa namna ya ukubwa wa kampeni za urais nchi nzima simuoni wa kuweza kumudu gharama zake pale Ufipa zaidi ya mzee Lowassa.

Hivyo ni vyama Chadema ikamueleza mapema Tundu Antipas Lisu kwamba asilitelekeze jimbo la Singida mashariki kwa matumaini ya kupewa nafasi ya kugombea urais, nahofia yale ya Dr Slaa yasije yakajirudia 2020.

Ni katika kukumbushana tu
Maendeleo hayana vyama!
 
Lissu kapewa fedha ya kutosha na hawa watu wa hapa hivo usidhani hawana hela wamejipanga na wengine wamemuahidi mambo mengisana wakati wa kampeni kwamba amuangushe Magufuli, lakini hizo ni kazi za kupoteza muda Magufuli ataendelea kuwa ikulu hadi 2025 na mbaya zaid wao watagombana wao kwa wao kuhusu kugombea
 
mtoa uzi ni mpuuzi huwa namlinganisha kama shaka s.shaka kiongozi wa ccm aliye na mahusiano na bwana salumu mpelembwe aliyekuwa kiongozi wa uvccm kule tanga. mpuuzi sana huyu bwana
 
Kesheni mkiomba Lissu asigombee, Lissu hawezi kuwa rais bora hilo halina mjadala. Lakini ndiye atakuwa mgombea sahihi kuliko Lowassa. Lissu anakubalika kwa mbali kuliko Magufuli, hivyo uchaguzi huo iwapo Lissu atagombea itabidi ccm ifanye mauji sana kwa kutumia madaraka ya rais na utakuwa ni uchaguzi utakaovunja sheria sana ili ccm kutangazwa washindi. Hilo sio tatizo, tatizo ni mgawanyiko mkubwa kama taifa baada ya rafu zitakazochezwa kwenye uchaguzi huo.
 
Tanzania na africa kwa ujumla wake hakuna vyama vya upinzani. Na hakuna duniani kote nchi inayoendeshwa kidemocrasia. Na haku na system ya kipumbavu na ya kijinga kama democracy. Siku nikitamani kuwaambia nitawaambia, ila wengi wetu hatujui sababu tumezaliwa ndani ya ujinga unaoitwa democracy. Jiulize tu toka tumeletewa hili zimwi linaloitwa democrasia, ni faida gani tumepata africa zaidi ya kutwangana sisi kwa sisi. Ujamaa ndo system nzuri sana niiipendayo kwani huna chako ukimiliki zaidi unanyanganywa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesheni mkiomba Lissu asigombee, Lissu hawezi kuwa rais bora hilo halina mjadala. Lakini ndiye atakuwa mgombea sahihi kuliko Lowassa. Lissu anakubalika kwa mbali kuliko Magufuli, hivyo uchaguzi huo iwapo Lissu atagombea itabidi ccm ifanye mauji sana kwa kutumia madaraka ya rais na utakuwa ni uchaguzi utakaovunja sheria sana ili ccm kutangazwa washindi. Hilo sio tatizo, tatizo ni mgawanyiko mkubwa kama taifa baada ya rafu zitakazochezwa kwenye uchaguzi huo.
Mkuu, unajidanganya sana! Lisu hana kipya ni sawa na kina lema tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Yohana Mbatizaji johnthebaptist habari za jioni. Niko nje ya mada kidogo. Hivi unamjua mtu anayeitwa USSR ? Nisaidie kumwambia kuwa Mungu sio mwanadamu. Na matunda ya chuki hayawezi kuwa matamu hata ukichanganya katikati ya tende na halua.
 
oya usilete kujuana hapa jukwaani fanya yaliyokufanya ulipie bando sip kufuata maisha ya watu
Sasa mbona wewe ni kinara wa kutaka mimi niache hicho unachofanya wewe na ulichozoea kufanya kila uzi na kila siku? Inakuwaje wewe kila uzi unacomment upupu tu? Kaa kimya ficha upumbavu wako.
 
Yani lowassa umpambanishe na lissu kweli!!!!! Punguza mahaba kwa lissu ndugu.
Kesheni mkiomba Lissu asigombee, Lissu hawezi kuwa rais bora hilo halina mjadala. Lakini ndiye atakuwa mgombea sahihi kuliko Lowassa. Lissu anakubalika kwa mbali kuliko Magufuli, hivyo uchaguzi huo iwapo Lissu atagombea itabidi ccm ifanye mauji sana kwa kutumia madaraka ya rais na utakuwa ni uchaguzi utakaovunja sheria sana ili ccm kutangazwa washindi. Hilo sio tatizo, tatizo ni mgawanyiko mkubwa kama taifa baada ya rafu zitakazochezwa kwenye uchaguzi huo.
 
Kesheni mkiomba Lissu asigombee, Lissu hawezi kuwa rais bora hilo halina mjadala. Lakini ndiye atakuwa mgombea sahihi kuliko Lowassa. Lissu anakubalika kwa mbali kuliko Magufuli, hivyo uchaguzi huo iwapo Lissu atagombea itabidi ccm ifanye mauji sana kwa kutumia madaraka ya rais na utakuwa ni uchaguzi utakaovunja sheria sana ili ccm kutangazwa washindi. Hilo sio tatizo, tatizo ni mgawanyiko mkubwa kama taifa baada ya rafu zitakazochezwa kwenye uchaguzi huo.

..naomba kutofautiana na wewe.

..there is a softer side of TL ila tatizo watu hawajauona upande huo.

..he is also very well read. Anapenda kujifunza wakati wote.

..ni mtu anayependa kusikiliza na haogopi kukosolewa. He does not take himself too seriously.

..anajali sana UTU wa binadamu, na anaamini ktk HAKI. And he would go to the extreme kutetea HAKI.

..Naamini mtu mwenye vigezo hivyo na vingine vya ziada anaweza kabisa kuwa kiongozi bora.
 
Bila kupinga maoni yako kwani nakuheshimu sana. Sikuwahi kumshuhudua Lissu akijihusisha na siasa za maendeleo. Nimemuona Lissu akiwa mzuri kwenye utetezi wa watu na mzuri katika ushawishi wa kisiasa, na yuko vyema kwenye sheria, huenda akatupa katiba mpya. Wasiwasi wangu anaweza kujikita kwenye eneo moja la kisheria na kuacha maeneo mengine. Pia ni hatari kuwa na mtu mwenye misimamo mikali kama tunavyoona kwa Magufuli sasa. Kwa mfano sasa tunaoona rais akijikita Zaidi kwenye miundo mbinu na kushindwa sehemu nyingine kama ajira, demokrasia, kilimo, uchumi nk.

Bila kuficha mtazamo wangu, kwangu Zitto anaweza kuwa rais bora kuliko wengine wote kwani ana misimamo ya wastani, ni rahisi kuwaunganisha watu wote, anaujua uchumi, anaweza siasa za maendeleo, anaiheshimu demokrasia, anajua mambo ya kijamii nk. Kwangu Zitto ni bora kuliko Magufuli au Lissu hiyo 2020 kwa sasa. Iwapo Lissu atapitishwa na cdm nitamuunga mkono, sio kwakuwa nategemea ubora toka kwake, lakini naamini atakuwa bora kuliko Magufuli.
 
Toka umemfahamu Lowassa ni lini umemuona hata akihutubia nusu saa point zilizonyooka? Niambie siku alitoa hutuba ikakugusa zaidi ya sifa zote kumwagwa na wapambe?
Kuhutubia sio inshu, inshu.niupepo lissu hana kashfa yoyote zaidi ya usaliti,lakini lowassa pamoja kuwa na kashfa yote stil bado alikuwa ana hamsha amsha ya watu kumuelewa.
 
Kesheni mkiomba Lissu asigombee, Lissu hawezi kuwa rais bora hilo halina mjadala. Lakini ndiye atakuwa mgombea sahihi kuliko Lowassa. Lissu anakubalika kwa mbali kuliko Magufuli, hivyo uchaguzi huo iwapo Lissu atagombea itabidi ccm ifanye mauji sana kwa kutumia madaraka ya rais na utakuwa ni uchaguzi utakaovunja sheria sana ili ccm kutangazwa washindi. Hilo sio tatizo, tatizo ni mgawanyiko mkubwa kama taifa baada ya rafu zitakazochezwa kwenye uchaguzi huo.
Mkuu ni kweli Lissu hawezi kuwa rais bora maana naye ana hulka za kidikteta kama Magufuli, pia atapoteza Muda mwingi mwenye mapinduzi ya baadhi ya sheria kuliko kuwajibika generally kama rais, hata Magufuli anaonekana kubase sana kwenye ujenzi wa miundombinu kuliko sekta Nyingine,

Ila kwa uhakika upinzani kushinda urais kwa miaka ya karibuni ni vigumu, maana vyama vya upinzani mbali na mazingira ya ushindani yasiyo rafiki lakin hawajajiandaa vema kuhusu uongozi
 
Bila kupinga maoni yako kwani nakuheshimu sana. Sikuwahi kumshuhudua Lissu akijihusisha na siasa za maendeleo. Nimemuona Lissu akiwa mzuri kwenye utetezi wa watu na mzuri katika ushawishi wa kisiasa, na yuko vyema kwenye sheria, huenda akatupa katiba mpya. Wasiwasi wangu anaweza kujikita kwenye eneo moja la kisheria na kuacha maeneo mengine. Pia ni hatari kuwa na mtu mwenye misimamo mikali kama tunavyoona kwa Magufuli sasa. Kwa mfano sasa tunaoona rais akijikita Zaidi kwenye miundo mbinu na kushindwa sehemu nyingine kama ajira, demokrasia, kilimo, uchumi nk.

Bila kuficha mtazamo wangu, kwangu Zitto anaweza kuwa rais bora kuliko wengine wote kwani ana misimamo ya wastani, ni rahisi kuwaunganisha watu wote, anaujua uchumi, anaweza siasa za maendeleo, anaiheshimu demokrasia, anajua mambo ya kijamii nk. Kwangu Zitto ni bora kuliko Magufuli au Lissu hiyo 2020 kwa sasa. Iwapo Lissu atapitishwa na cdm nitamuunga mkono, sio kwakuwa nategemea ubora toka kwake, lakini naamini atakuwa bora kuliko Magufuli.
Ninyi mnadhani Lissu anaweza kuwa rais bora zaid hata ya Magufuli???? Ni suala ambalo haliwezekani
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom