2019 umekuwa mwaka mgumu kwa CHADEMA lakini wenye mafanikio kwa CCM na ACT Wazalendo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,901
141,840
Kiukweli mwaka 2019 unaoelekea ukingoni umekuwa mgumu sana kwa Chadema ambayo ilikimbiwa na wabunge wake wengi.

Kadhalika ni mwaka ambao Chadema ilimpoteza mwanachama wake maarufu kuliko wote mzee Lowassa aliyehamia CCM. Pia mzee Sumaye na mzee Mgeja na kundi kubwa la madiwani waliamua kuachana na chadema na kujiendea CCM.

Ni mwaka ambao viongozi wakuu wa Chadema wametumia muda mwingi mahakama ya kisutu kwenye kesi ya Akwilina badala ya kuwatumikia wananchi. Kawe, Bunda, Kibamba, Iringa mjini na Tarime wamekosa uwakilishi bungeni mara kadhaa.

ACT wazalendo wao wamefanikiwa kupata idadi kubwa ya wanachama baada ya maalimu Seif na wafuasi wake kuachana na CUF.

CCM ndio imepata neema kubwa baada ya kupokea wabunge zaidi ya 10 kutoka upinzani na mamia ya madiwani nchini kote.

Nawatakia Christmas yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Bahari huwa haikai na uchafu. Ukiangalia kwa jicho la haraka kuondoka kwa Lowassa na Sumaye ni kama cdm imepoteza, lakini kiukweli ni kuwa cdm imerudi kwenye uhalisia wake na sio hiyo idadi kubwa ya viongozi fake toka ccm. Katika jambo ambalo cdm inabidi ijirekebishe ni hiyo ya kubeba hizo taka ngumu toka ccm kisha kuwapa madaraka. Kwa sasa cdm imebaki na watu wake halisi wenye kuweza siasa za upinzani, na sio hayo matapeli yaliyokuja kusaka madaraka.

Ccm sio chama cha siasa bali ni taasisi ya kidola, na chini ya Magufuli ndio kabisa ccm imejikuta haifanyi siasa bali inajimwambafy. Hivyo badala ya kuisifia ccm ni bora usifie vyombo vya dola kutii madaraka ya rais yanayotumika vibaya. ACT wazalendo ni kweli inaweza kufaidi idadi ya wabunge huko Znz iwapo uchaguzi utaheshimiwa, lakini idadi hasa ya watu iko huku bara ambako hiyo ACT haina support kubwa. Huko bungeni watafanya nini, ndani ya bunge ambalo spika anazunguka kugawa vyakula kwenye safari za rais na kujipendekeza kulikopita kiasi?
 
chama dola CCM huwezi kukitenganisha na jeshi, huwezi kukitenganisha na mihimili yote na taasisi zote zenye mamlaka kamili
yani inamiliki usajili wa vyama vya siasa, mpaka tukieza kuzitenganisha taasisi hizi na kuzipa uhuru na mamlaka kamili ndipo tutaona matunda mema ya demokrasia # Mungu atuhurumie
 
Kwahiyo tuna upinzani bandia?
 
Bahari huwa haikai na uchafu. Ukiangalia kwa jicho la haraka kuondoka kwa Lowassa na Sumaye ni kama cdm imepoteza, lakini kiukweli ni kuwa cdm imerudi kwenye uhalisia wake na sio hiyo idadi kubwa ya viongozi fake toka ccm. Katika jambo ambalo cdm inabidi ijirekebishe ni hiyo ya kubeba hizo taka ngumu toka ccm kisha kuwapa madaraka. Kwa sasa cdm imebaki na watu wake halisi wenye kuweza siasa za upinzani, na sio hayo matapeli yaliyokuja kusaka madaraka.

Ccm sio chama cha siasa bali ni taasisi ya kidola, na chini ya Magufuli ndio kabisa ccm imejikuta haifanyi siasa bali inajimwambafy. Hivyo badala ya kuisifia ccm ni bora usifie vyombo vya dola kutii madaraka ya rais yanayotumika vibaya. ACT wazalendo ni kweli inaweza kufaidi idadi ya wabunge huko Znz iwapo uchaguzi utaheshimiwa, lakini idadi hasa ya watu iko huku bara ambako hiyo ACT haina support kubwa. Huko bungeni watafanya nini, ndani ya bunge ambalo spika anazunguka kugawa vyakula kwenye safari za rais na kujipendekeza kulikopita kiasi?
Unazungumzia kuondoka kwa Lowasa na wafuasi wake kama jambo jema na kwamba CDM itarudi ktk uhalisia wake
Unaujua uhalisia wa chadema .!??
...Ni chini ya 20% ya kura ukilinganisha na 40% alizopewa Lowasa
..Uhalisia wa CDM kabla ya Lowasa ni nusu ya Wabunge walioko CDM sasa
Uhalisia wa CDM ni ruzuku chini ya 200mls kwa mwezi ukilinganisha na zaidi ya 300mls kwa mwezi
Tambua hili ndio sababu Mbowe sasa anaanzisha mkakati wa kukusanya zaidi 15bls pa kufidia pengo. ANAJUA KIFUATACHO
Chadema ya asili baada ya kuwatupa kina Sumaye na Mwambe mnaowaita wasaliti na walilia vyeo ni Chadema ya mwaka 2010.
Sioni haja ya kuzungumzia ikulu kwa CDM ya 2013.
Ndio maana nakutaka Ndugu yangu usidharau ACT... kama kweli CUF wamemfuata Maalim Seif huko Zenji basi tambua wana uhakika wa Majimbo yote 18 ya Pemba na na angalau 7 ya Unguja... Ndio kusema wanategemea si chini ya wabunge 25 kutoka ZANZIBAR pekee. Kama haitoshi CDM imekuwa ikifaidika na minyukano ndani ya CCM kwa kuokota potential candidate wenye uwezo wa kupindua matokeo kibabe ambao wataenguliwa au kuhama Ccm kama ilivyokuwa kwa Cecil Mwambe. Sasa hao hawtoenda CDM baada ya kuona yaliyowapata watangulize wao na badala yake wataenda ACT. Idadi hiyo haiwezi kufikiwa na CDM bara. Ni wazi bunge Lijalo kambi rasmi itatoka ACT na sio CHADEMA... hilo pgo kubwa CDM na Mbowe mla RUZUKU. Zamu ya kula inahamia kwa Zito sasa, ndio maana anaweza kufikiri kugombea Uraisi kwa sababu Ruzuku watakayopata ACT itafidia pato la Ubunge.
 
Christmas yenye baraka kutoka kwa nani?
Kiukweli mwaka 2019 unaoelekea ukingoni umekuwa mgumu sana kwa Chadema ambayo ilikimbiwa na wabunge wake wengi.

Kadhalika ni mwaka ambao Chadema ilimpoteza mwanachama wake maarufu kuliko wote mzee Lowassa aliyehamia CCM. Pia mzee Sumaye na mzee Mgeja na kundi kubwa la madiwani waliamua kuachana na chadema na kujiendea CCM.

Ni mwaka ambao viongozi wakuu wa Chadema wametumia muda mwingi mahakama ya kisutu kwenye kesi ya Akwilina badala ya kuwatumikia wananchi. Kawe, Bunda, Kibamba, Iringa mjini na Tarime wamekosa uwakilishi bungeni mara kadhaa.

ACT wazalendo wao wamefanikiwa kupata idadi kubwa ya wanachama baada ya maalimu Seif na wafuasi wake kuachana na CUF.

CCM ndio imepata neema kubwa baada ya kupokea wabunge zaidi ya 10 kutoka upinzani na mamia ya madiwani nchini kote.

Nawatakia Christmas yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pimbi bana ccm wanna dola, polisi,jeshi,uwt,tumeccm,mahakama lakini bado wanaengua wagombea wa upinzani?wanaogopa wapinzani , aiseee.
 
Bahari huwa haikai na uchafu. Ukiangalia kwa jicho la haraka kuondoka kwa Lowassa na Sumaye ni kama cdm imepoteza, lakini kiukweli ni kuwa cdm imerudi kwenye uhalisia wake na sio hiyo idadi kubwa ya viongozi fake toka ccm. Katika jambo ambalo cdm inabidi ijirekebishe ni hiyo ya kubeba hizo taka ngumu toka ccm kisha kuwapa madaraka. Kwa sasa cdm imebaki na watu wake halisi wenye kuweza siasa za upinzani, na sio hayo matapeli yaliyokuja kusaka madaraka.

Ccm sio chama cha siasa bali ni taasisi ya kidola, na chini ya Magufuli ndio kabisa ccm imejikuta haifanyi siasa bali inajimwambafy. Hivyo badala ya kuisifia ccm ni bora usifie vyombo vya dola kutii madaraka ya rais yanayotumika vibaya. ACT wazalendo ni kweli inaweza kufaidi idadi ya wabunge huko Znz iwapo uchaguzi utaheshimiwa, lakini idadi hasa ya watu iko huku bara ambako hiyo ACT haina support kubwa. Huko bungeni watafanya nini, ndani ya bunge ambalo spika anazunguka kugawa vyakula kwenye safari za rais na kujipendekeza kulikopita kiasi?
Naona mnalamba matapishi yenu. Hizi kauli za taka chafu sijui bahari haikai na uchafu ina tofauti gani na kauli ya Oil chafu ya CCM iliyokua maarufu sana wakati wa uchaguzi Mkuu 2015 baada ya wanachama wake wengi ikiwemo mzee lowassa kuhamia Upinzani.

Ukweli ni kwamba CDM ikirudi kwenye uhalisia wake (uanaharakati) haitoweza kuwa na impact yoyote kwenye siasa za sasa kinaenda kuwa chama mfu. Mafanikio mengi ya CDM ya sasa yaliletwa na wahamiaji ambao wengi wao wameondoka kwenye hicho chama. Nakubaliana na wewe, kwamba Kosa kubwa lililofanywa na CDM ni kupokea wahamiaji na kuwafanya kuwa key aspects ya mafanikio yao.

Kilichotakiwa kufanyika sasa CDM ni kubadilisha uongozi wote uliokuepo including Mbowe na kutafuta watu ambao ni 'Games Changer' watu ambao wanajua kusoma political dynamics na kuendana nazo. Lakini bahati mbaya wameamua kukumbatia utamaduni wa kurudisha sura zile zile wakitegemea kupata matokeo tofauti. Uchaguzi wa 2020 utathibitisha haya niyasemayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unazungumzia kuondoka kwa Lowasa na wafuasi wake kama jambo jema na kwamba CDM itarudi ktk uhalisia wake
Unaujua uhalisia wa chadema .!??
...Ni chini ya 20% ya kura ukilinganisha na 40% alizopewa Lowasa
..Uhalisia wa CDM kabla ya Lowasa ni nusu ya Wabunge walioko CDM sasa
Uhalisia wa CDM ni ruzuku chini ya 200mls kwa mwezi ukilinganisha na zaidi ya 300mls kwa mwezi
Tambua hili ndio sababu Mbowe sasa anaanzisha mkakati wa kukusanya zaidi 15bls pa kufidia pengo. ANAJUA KIFUATACHO
Chadema ya asili baada ya kuwatupa kina Sumaye na Mwambe mnaowaita wasaliti na walilia vyeo ni Chadema ya mwaka 2010.
Sioni haja ya kuzungumzia ikulu kwa CDM ya 2013.
Ndio maana nakutaka Ndugu yangu usidharau ACT... kama kweli CUF wamemfuata Maalim Seif huko Zenji basi tambua wana uhakika wa Majimbo yote 18 ya Pemba na na angalau 7 ya Unguja... Ndio kusema wanategemea si chini ya wabunge 25 kutoka ZANZIBAR pekee. Kama haitoshi CDM imekuwa ikifaidika na minyukano ndani ya CCM kwa kuokota potential candidate wenye uwezo wa kupindua matokeo kibabe ambao wataenguliwa au kuhama Ccm kama ilivyokuwa kwa Cecil Mwambe. Sasa hao hawtoenda CDM baada ya kuona yaliyowapata watangulize wao na badala yake wataenda ACT. Idadi hiyo haiwezi kufikiwa na CDM bara. Ni wazi bunge Lijalo kambi rasmi itatoka ACT na sio CHADEMA... hilo pgo kubwa CDM na Mbowe mla RUZUKU. Zamu ya kula inahamia kwa Zito sasa, ndio maana anaweza kufikiri kugombea Uraisi kwa sababu Ruzuku watakayopata ACT itafidia pato la Ubunge.

Mkuu ACT ya sasa siyo ile ya kabla ya ujio wa Maalim Seif, Usitegemee kuwa hizo ruzuku unazozizungumza Zitto atazitafuna kirahisirahisi tu. Kwenye masuala ya fedha ya chama lazima maalim seif ataweka vijana wake wasimamie mana pato kubwa la chama la ruzuku na wafadhili litatokana na wao.
 
Naona mnalamba matapishi yenu. Hizi kauli za taka chafu sijui bahari haikai na uchafu ina tofauti gani na kauli ya Oil chafu ya CCM iliyokua maarufu sana wakati wa uchaguzi Mkuu 2015 baada ya wanachama wake wengi ikiwemo mzee lowassa kuhamia Upinzani.

Ukweli ni kwamba CDM ikirudi kwenye uhalisia wake (uanaharakati) haitoweza kuwa na impact yoyote kwenye siasa za sasa kinaenda kuwa chama mfu. Mafanikio mengi ya CDM ya sasa yaliletwa na wahamiaji ambao wengi wao wameondoka kwenye hicho chama. Nakubaliana na wewe, kwamba Kosa kubwa lililofanywa na CDM ni kupokea wahamiaji na kuwafanya kuwa key aspects ya mafanikio yao.

Kilichotakiwa kufanyika sasa CDM ni kubadilisha uongozi wote uliokuepo including Mbowe na kutafuta watu ambao ni 'Games Changer' watu ambao wanajua kusoma political dynamics na kuendana nazo. Lakini bahati mbaya wameamua kukumbatia utamaduni wa kurudisha sura zile zile wakitegemea kupata matokeo tofauti. Uchaguzi wa 2020 utathibitisha haya niyasemayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli mtupu!
 
Huenda unadhani unajadili na mtoto au mgeni wa siasa na mtu asiyejua lolote. Kwa taarifa yako mafanikio ya cdm yaliletwa na kazi kubwa ya siasa iliyofanywa na cdm mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010. Kipindi cha toka 2010 mpaka 2015 cdm ndio chama cha siasa kilichofanya mikutano na kukutana na wananchi wengi kuliko chama chochote cha siasa ikiwemo ccm. Na hilo halina mjadala, wakati hayo yakifanyika hizo taka ngumu toka ccm chini ya Lowassa walikuwa wanazunguka kwenye nyumba za ibada kugawa pesa. Ingekuwa hao wanaccm walienda TLP au TADEA kisha wakapata viti hivyo hapo ungekuwa na hoja.

Usitake kupotosha kiwaziwazi jambo tunalolifahamu, wengi wa hao wanaccm walikuja cdm miezi miwili au mitatu kabla ya uchaguzi, na kilichowabeba ni kukubalika kwa cdm. Kwa hili la cdm kuokota hizo taka ngumu ilibidi Mbowe na kamati yake wakae pembeni kwa kuchukua vodafasta, matokeo yake zaidi ya 90% wamerudi walikota. Muda mrefu sana nimesema hata Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm hivi sasa ni kosa kubwa la kiufundi, kwani hana jipya.

Hiyo 2020 mnayotishia nayo watu sio kwakuwa ccm iko imara au kwakuwa cdm ni mbovu, ila ni madaraka ya urais yanayotumika vibaya. Wote tumeshuhudia chaguzi zote toka awamu hii imeingia madarakani zikinajisiwa waziwazi, kukiwa na uhayani, ukatili na ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, na yote haya yanafanyika chini ya uratibu wa vyombo vya dola. Kile kilichowapa ushindi wa fedheha ccm kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ndio jicho hicho kitawapa ushindi 2020 na sio kwa uwezo wa kisiasa. Hayo ya kwamba kuna maendeleo, au viongozi waliondoka cdm zitatumika tu kama sehemu ya kufichia ukweli, lakini ukweli hasa ni mamlaka zote za uchaguzi kuwa na hofu ya madaraka ya rais yanayotumika vibaya fullstop.
 
Back
Top Bottom