2019 laki moja inanunua nguo nne tu

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,131
3,911
Mavazi ni mahitaji ya msingi lakini kipato cha mtanzania kikidumaa kila siku.Jana kwenye shopping zangu nikasema 100,000 ngoja niitumie kwa mavazi leo.Nikapita mitaa ya sinza na mabibo.Yaani nimeambulia kadeti moja 28000,shati moja 25,000 na t-shirt mbili za low quality za 20,000 each.Hizi ni nguo za mchina za kawaida sana ukipita wala mtu hageuki eti umependeza.

Kwa nchi za wenzetu unapozungumzia "Thousands" ni hela nyingi sana.

imagine December sikukuu una watoto watatu tu wanataka nguo za sikukuu na January Ada,mshahara mfano 700,000 bado makato.
 
Hio laki 1 ukienda pale woolworth unaweza kuishia kununua T-shirt 1 tu lkn hio hio Laki 1 ukienda kwny 'chagulaga' utabeba mzigo wa kutosha.

So itategemea na umechagua wapi.
 
Nenda mtumbani suruali mf.12000 ukarekebishe kwa fundi 3000 hadi 5000 au akuharibie kabisa.Hii naongelea maduka ya kawaida sana.Mitumba inaanza kupotea siku hizi na kwa nini uvae mtumba?
Uwe unavaa mitumba tu kama kipato cha kuungaunga yanini kuilazimisha haja kubwa itoke wakati wasaa wa kutoka bado
 
Nenda mtumbani suruali mf.12000 ukarekebishe kwa fundi 3000 hadi 5000 au akuharibie kabisa.Hii naongelea maduka ya kawaida sana.Mitumba inaanza kupotea siku hizi na kwa nini uvae mtumba?
Mitumba pia ina grades kama hizo nguo za dukania pia , naiamini sana mitumba

Af hiyo bei ya kurekebisha ulotaja wewe itakua ya mitaa ya kipapaa , buku au buku mbili unapunguziwa kitu fresh tu
 
System ya kuwazoesha watoto eti kuwanunulia nguo ni mpk sikukuu ni ya kishamba sana.
Hii ni kweli yani mtoto avae nguo zilizochoka kila siku halafu apendeze sikukuu tu daah, kama ni kupendeza anatakiwa kupendeza kila siku hata yeye mwenyewe inamfanya awe na furaha
Na kuna ile tabia mtoto anavalishwa nguo nzuri akienda kanisani ,akirudi anaambiwa abadilishe halafu anavaa za nyumbani zilizochoka
Daah ngoja nitafute pesa kwa nguvu watoto wangu waje wafurahie maisha.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom