2019 Africa Cup of Nations Special Thread

Nimejitahidi kufuatilia hii michuano tangu awali mpaka tamati, nimegundua machache yafuatayo kuhusu soka letu la afrika.

1. Tuna tatizo kubwa sana la clinical finishing, wachezaji wanatoka na mpira nyuma vizuri tu wakifika golini maamuzi sahihi yanakosekana na ndio maana tunaona attempts nyingi magoli machache, na hili ni tatizo la muda mrefu sana.

2.Wachezaji wetu wa kiafrika hawajajua jinsi ya kutumia ipasavyo mipira ya adhabu na kona hasa kwenye mechi muhimu hili kuiokoa timu na ikitokea basi ni mara chache sana.

3.Wachezaji wetu wanaofanya vizuri ulaya wakija huku wanaonekana wakawaida ni kwasababu huko ulaya wanacheza kwenye mifumo mizuri yenye wachezaji wazuri wengi na pia wanalipwa vizuri kulinganisha na huku.

4.Waafrika wa kaskazini wanajua sana kucheza mpira wa kimatokeo dhidi ya waafrika wenzao pale inapobidi.

5.Vipaji tulivyonavyo siku hizi ni vya kawaida sana kulinganisha na miaka ya nyuma, yaani hakuna maajabu yoyote mtu akishika mpira unajua kabisa ataufanyaje na ndio maana hata viwanja havina mashabiki.

6.Bado tutaendelea kuwa washika mkia kwenye world cup pamoja na kutumia idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza ligi zenye ushindani ulaya. Maana wakija kwenye timu zao za afrika wanacheza kiafrika zaidi.

7.Taifa stars ndio timu iliyocheza mpira mbovu kupindukia kuliko timu zingine zote kwenye hii michuano.

8.Waamuzi wetu wa kiafrika ni waamuzi wa ovyo kupindukia na sioni referee yoyote kutoka afrika akichezesha mechi kubwa kama fainali ya world cup hivi karibuni.


******Hongera sana kwa Algeria tangu mwanzo mlionekana mna stahili ubingwa huu******

tukutane Cameroon 2021 february


🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Mashallah nimeipenda sana hii 👇🏿

Screenshot_20190720-102502_Instagram.jpg



From now, Timu yangu ya kushabikia ni Algeria 😍😍😍😍😍

Ukipata unamshkuru Allah, na ukikosa pia unatakiwa umshkuru Allah.

Victoire
Mwifwa
 
Back
Top Bottom