Jurrasic Park
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 3,792
- 6,768
Herini za mwaka mpya 2017
Katika pita pita zangu za huku mtaani kwenye msimu wa sikukuu hii na baada ya kupata mialiko kwa familia tofauti nimekutana na hiki kitu.
hali ya wa baba na wa mama wanakuwa wana miili mizuri(wanene) mpaka vitambi ili hali watoto wana kwashariokor. kinachonishangaza siku nyama ikipikwa watoto wanakaa jikoni kuisubiria iive. mfano; kuna baba mmoja siku moja nilimkuta anakula kuku mzima mgahawa flani sasa cha ajabu siku nyingine nikamkuta anawaambia watoto wake watafute kuni wapike makande nilichoka.
naomba wazazi wangu, mjitahidi kula nyumbani kama chakula kikiwashinda cha nyumbani basi mjue kiliwashinda watoto wenu siku nyingi. sio tabia nzuri ule kuku na vinono alafu chakula cha nyumbani wanakula makande, maharage na vinginevyo duni. kuleni nyumbani acheni ufisadi wa kula vinono nje huku nyumbani watoto wakilia njaa
asanteni