2017: Wito wangu kwa baba na mama wa familia zetu

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,770
2,000
Herini za mwaka mpya 2017

Katika pita pita zangu za huku mtaani kwenye msimu wa sikukuu hii na baada ya kupata mialiko kwa familia tofauti nimekutana na hiki kitu.

hali ya wa baba na wa mama wanakuwa wana miili mizuri(wanene) mpaka vitambi ili hali watoto wana kwashariokor. kinachonishangaza siku nyama ikipikwa watoto wanakaa jikoni kuisubiria iive. mfano; kuna baba mmoja siku moja nilimkuta anakula kuku mzima mgahawa flani sasa cha ajabu siku nyingine nikamkuta anawaambia watoto wake watafute kuni wapike makande nilichoka.

naomba wazazi wangu, mjitahidi kula nyumbani kama chakula kikiwashinda cha nyumbani basi mjue kiliwashinda watoto wenu siku nyingi. sio tabia nzuri ule kuku na vinono alafu chakula cha nyumbani wanakula makande, maharage na vinginevyo duni. kuleni nyumbani acheni ufisadi wa kula vinono nje huku nyumbani watoto wakilia njaa

asanteni
 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
16,962
2,000
Mie ujumbe wangu ni, ewe mzazi kama unapenda ssna kilevi, ukitoka kazini chukua take away zako 3 baada ya kupata mlo wa usiku na familia basi fungua chupa zako 3. Hii itasaidia kujenga familia zenu na kuepuka vishawishi na marafiki wabaya wa usiku.
 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
16,962
2,000
Kwanza mlo wa jioni/usiku ni muhimu kujumuika na familia, saa ngapi utawafundisha watoto table manners!
Kabisa ila wanaume wengi jukumu hilo wanawaachia wake zao.... shame on them (those men)
 

Sakayo

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
56,541
2,000
Wanaume jaman ndo wana hizo tabia, nyama choma ataila jumatatu mpaka jumatatu lakini nyumbani watoto wataila jumapili tu, nafikiri wanaume wote wenye familia wangekuwa wanajumuika na familia zao hakika baa zingekuwa zinafungwa saa moja
 

Jael

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
68,346
2,000
Mie ujumbe wangu ni, ewe mzazi kama unapenda ssna kilevi, ukitoka kazini chukua take away zako 3 baada ya kupata mlo wa usiku na familia basi fungua chupa zako 3. Hii itasaidia kujenga familia zenu na kuepuka vishawishi na marafiki wabaya wa usiku.
Amen.
 

Jael

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
68,346
2,000
Kwanza mlo wa jioni/usiku ni muhimu kujumuika na familia, saa ngapi utawafundisha watoto table manners!
Sio table manners tu, utapata pia wasaa wa kuongea na watoto hata kujua matatizo yao.
 

Jael

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
68,346
2,000
Mie wito wangu kwa wazazi ni kujitafakari kwa kina ni aina gani ya maisha wanayajenga kwa watoto wao, je ni maisha ambayo wao wangependa kuishi(kama watoto)?

Ndoa na jamii zinalalamikiwa sana siku hizi, lkn vyote chanzo ni katika familia,je unamlea mwanao kuwa nani kesho?

Lakini pia mtoto wa mwenzio ni mwanao,hivyo mtendee namna ambavyo ungependa wako atendewe.

It beggins with you/us.
 

griffin2

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
634
1,000
ni bora mzazi ulale njaa , ila watoto wale.
Haka katabia ka kijichana kapo sana maeneo ya PWANI, TANGA na DSM
Tena mtoto ananunua mihogo yake ya kunywea chai wakati huo huo baba anajichana na chapati na samaki.huruma sana.
 

Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
26,927
2,000
Sio table manners tu, utapata pia wasaa wa kuongea na watoto hata kujua matatizo yao.
Kweli kabisa. Ukikaa karibu na watoto ni rahisi kujua shida zao, tatizo tunatafuta pesa tukisahau kuwa tunamtafutia nani.
 

Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
26,927
2,000
Tena mtoto ananunua mihogo yake ya kunywea chai wakati huo huo baba anajichana na chapati na samaki.huruma sana.
Nadhani wazazi wengi tuna ubinafsi!! Sasa kama umeacha hela ya ugali-harage, unaenda kupiga kuku mchemsho, tuseme nini kama sio ubinafsi!!
 

J C

JF-Expert Member
Dec 12, 2013
2,636
2,000
Wababa wanakilio wasichojua wakipeleke wapi. Unaleta kuku home anavyopikwa ni hatari ya kutisha yaani vibaya vibaya sana. Unaacha pesa nyumbani inapigwa panga yananunuliwa matembele. Unaleta mchele home mawe yake mpka jino linataka kutoka alafu unakuta bokoboko au haujaiva. Dagaa sasa zimejaa mchanga tupu mchuzi pipa. Unamwambia wife apike chakula fulani unakipenda anakwambia hana muda kwani amekuwa na kazi kibao. Sasa baba anaamua atafute chocho linalopika chakula murua anagonga balaa home anawaachia dagaa na dona ili waangaike navyo na hili ni sawa maana haiwezekani uache elfu ishirini nyumbani au zaidi wakatj wewe baba huvili wala uvifaidi kwa uzembe wa familia na mkeo.
Nina mjomba angu alikuwa mkali kwa mabinti zake hasa kwenye mapishi sasa ukute ni mke inakuwa aibu kumuadhibu kwa kosa hili ati kashindwa kupika cha kufanya unasepa tu kwenye restaurant bora unagonga msosi murua kwa afya yako ili upate nguvu ya kutafuta ada na mahitaji mengine ya familia ya msingi bila ya kusahau dagaa na unga wa dona pamoja na nyanya chungu kwa ajili ya familia kwani kula huko hawatokufaaaaaa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom