Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Tusiombeaneni "laana" wakuu. Viongozi wasiwaombee laana raia na raia wasiwaombee "laana" viongozi wao. Hata kama mtu anadhani amefanyiwa uovu, ni vizuri akawa na moyo wa subra na akajiepusha kutoa "laana" pasipo ulazima wa kufanya hivyo. Nasema hivi kwa sababu "laana" si kitu kizuri, inaweza kumkumba aliyemo na asiye kuwamo. Kwa mfano; ukimuombea laana kiongozi na laana yako ikamshika, atazidi kuharibu, na akizidi kuharibu wakati wewe uko nyuma yake, nawe utazidi kuumia. Kwa hiyo ni bora kujitahidi kuwa na roho za kiasi ili kupata unafuu.
Ukimlaani dereva, na akawa kweli ana makosa laana inaweza kumpata, laana ikimpata akachanganyikiwa wakati anaendesha atadondosha gari, akidondosha gari nawe umo ndani utavunjika kiuno. Heri ya nusu shari kuliko shari kamili.
Kama mtu anaona kiongozi fulani anafanya jambo lisilostahili na pengine linalomuumiza moyo, amueleze kama anaweza, ila sana sana amuombee kwa Mungu ili abadilike badala ya kumlaani.
Wakunielewa wamenielewa.