VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
- Ulikuwa ni mwaka wa watumishi wa umma kutenguliwa teuzi zao, kusimamishwa kazi. Lakini, wengine waliteuliwa.
- Wananchi wamelalamika mwaka mzima wakidai hali ya maisha ni ngumu;pesa imepotea. Lakini, wananchi hao wameendelea kupambana na kusonga mbele katika kuzoea kinachoendelea.
- Wananchi, wanasiasa, watumishi na hata wanahabari wamekamatwa vya kutosha kwa makosa mbalimbali hasa yahusuyo matumizi ya mitandao;uchochezi, ujangili na kadhalika. Lakini, wengi wao wameachiwa kwa dhamana; wamelipa faini na wengine wameachiwa huru kabisa na mahakama.
- Viongozi wa kiserikali wamepigana vikumbo mwaka mzima katika kubuni 'vya kumfurahisha' Mkuu wa nchi, mteule wao. Waliofanikiwa kubuni vyema, waliingiza/walipata sifa na vyeo vipya.
- 2016 ulikuwa mwaka wa kipekee. Unaishia na kusakwa, dead or alive, kwa Ben Saanane wa CHADEMA.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam