2016: Mwaka wa tumbua-teua, lalama-chagama, kamata-achia na igiza-ingiza!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,065
2,000
  • Ulikuwa ni mwaka wa watumishi wa umma kutenguliwa teuzi zao, kusimamishwa kazi. Lakini, wengine waliteuliwa.
  • Wananchi wamelalamika mwaka mzima wakidai hali ya maisha ni ngumu;pesa imepotea. Lakini, wananchi hao wameendelea kupambana na kusonga mbele katika kuzoea kinachoendelea.
  • Wananchi, wanasiasa, watumishi na hata wanahabari wamekamatwa vya kutosha kwa makosa mbalimbali hasa yahusuyo matumizi ya mitandao;uchochezi, ujangili na kadhalika. Lakini, wengi wao wameachiwa kwa dhamana; wamelipa faini na wengine wameachiwa huru kabisa na mahakama.
  • Viongozi wa kiserikali wamepigana vikumbo mwaka mzima katika kubuni 'vya kumfurahisha' Mkuu wa nchi, mteule wao. Waliofanikiwa kubuni vyema, waliingiza/walipata sifa na vyeo vipya.
  • 2016 ulikuwa mwaka wa kipekee. Unaishia na kusakwa, dead or alive, kwa Ben Saanane wa CHADEMA.
Merry Christmas and prosperous New Year JF Members!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 

Mibas

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
3,723
2,000
Mlianza vibaya na hatimaye mmemaliza vibaya 2016, ccm laana ya mwenyezimungu iwe juu yenu.
 

sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,825
2,000
Tuombe uzima tukisubiri 2017, bila shaka timu itakuwa ishajuana vya kutosha na iwe muda wa kusukuma mashambulizi kwenda mbele.
 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,002
2,000
Mwaka wa kawaida tu, kwani hao waliotenguliwa hawapati mshahara...?
 

Transcend

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
20,171
2,000
Nilitegemea nione tumbua tumbua inazaa matunda ila naona upuuzi tuu...

Kama mtu mlimtumbua na ana kosa kweli peleka mahakamani..

La kuchekesha kabisa waziri wa sheria anakwambia watu wamechange hadi mahakama umekosa kesi...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom