2016 majipu yametumbuliwa, je vidonda vimepona?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,559
Mdau, kwa kawaida jipu likitumbuliwa kidonda huoshwa na kupakwa dawa ili kipone. Majipu mengine huoshwa kwa utambi kabla ya kupakwa dawa. Niliambiwa utotoni kuwa kidonda cha jipu kisipooshwa sawasawa na kupona basi jipu lingine linaweza kuibuka sehemu ileile.

Sasa wadau naomba tuyajadili haya majipu ya kisiasa na kiutendaji yaliyotumbuliwa, je yamepona? Au mengine yana viashiria vya kujirudia labda hayapata dawa ya kutosha? Kwa jipu la NSSF naona kama vile limepona kabisa sasa sijui huko Bandari, TRA, RAHCo na kwingineko kulikotumbuliwa hali ikoje.

Karibu tujadili karibu mwaka mpya 2017 ahsante.
 
Hakukuwa na majipu bali ubadilishaji wa nafasi za kazi.Tusubiri Masamaki na yeye apate ubalozi naona atapangiwa Nigeria.Mtoto wa nyumbani LUGUMI asubiri ukuu wa wilaya.Na yule mwanasheria wa Singa singa asubiri tunampa ujaji maana alifanikisha mchoro wa ESCROW.CCM OYEEEEEEEEEE.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom