2015 Wenje akagombee Rorya na Adam Chagulani agombee Nyamagana

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
wana JF,
Nikiwa mtanzania mwenye nia njema na nchi yangu,haya ni maoni yangu binafsi.nitakubali kupokea changamoto au maoni toka kwa mwana JF yoyote mwenye maoni tofauti na mimi,pia hata wahusika waheshimiwa wenyewe kama wamo humu.

Kulingana na hali halisi ya siasa za Rorya,nikizingatia kauli niliyowahi kumsikia mheshimiwa Lameck airo katika kituo cha televisheni ya ITV akisema (ilikuwa kipindi cha ahadi majimboni) hatagombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa 2015.

Ni dhahiri kuwa Nafasi hiyo itakuwa wazi kwa CDM kulichukuwa,tukizingatia kuwa tuna kijana mzalendo wa kweli ambaye ni mzaliwa wa jimbo husika Mh Ezekiel wenje. Ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika medani za siasa nchini na uwakilishi wa kweli.

Katika jimbo la Nyamagana kumekuwa na tabia mazowea ya kutomrudisha mbunge mmoja katika nafasi hiyo kwa awamu mbili mfululizo,bali wana uwezo wa kukipa chama nafasi ya uwakilishi bungeni kwa vipindi kadhaa,lakini kwa mgombea mpya kwa kila awamu (historia imetuonyeshha mara zote katika chaguzi zilizotangulia )

Sijui ni kwa nini tabia hii imechukuwa nafasi,(hili nalo linahitaji mjadala kulijadili). kwa hali halisi bado CDM wana nafasi kubwa na ushawishi wa kutosha mpaka sasa.na ninaomba mungu hili liendelee kuwa hivyo. Hadi mwaka 2015.

Mwaka 2015 ifanyike reshufle na tumchukuwee kijana msomi mwihgine ambaye ni mheshimiwa Diwani wa Kata ya Igoma,Mh Adam chagulani awe mgombea wa Nyamagana.

Kitendo cha CDM kulichukuwa Jimbo la Rorya kitaimarisha chama katika ukanda wa Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla.na kutufanya tuweze kujitanua zaidi hadi serengeti na kwingineko katika kanda ya ziwa..

Naomba kuwakilisha kwa nia nzuri, lakini nikitarajia maoni mbalimbali kwa nia nzuri na kwa maslahi na ustawi wa taifa letu na vizazi vijavyo.
 
Kulingana na hali halisi ya siasa za Rorya,nikizingatia kauli niliyowahi kumsikia mheshimiwa Lameck airo katika kituo cha televisheni ya ITV akisema hatagombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa 2015.
Ni dhahiri kuwa Nafasi hiyo itakuwa wazi kwa CDM kulichukuwa,tukizingatia kuwa tuna kijana mzalendo wa kweli ambaye ni mzaliwa wa jimbo husika Mh Ezekiel wenje. Ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika medani za siasa nchini na uwakilishi wa kweli.

Katika jimbo la Nyamagana kumekuwa na tabia mazowea ya kutomrudisha mbunge mmoja katika nafasi hiyo kwa awamu mbili mfululizo,bali wana uwezo wa kukipa chama nafasi ya uwakilishi bungeni kwa vipindi kadhaa ilimradi wabunge teule wanakuwa watu makini.
Na wanaokubalika .
Sijui ni kwa nini tabia hii imechukuwa nafasi,ingawa kwa hali halisi bado CDM wana nafasi kubwa na ushawishi wa kutosha mpaka sasa.na ninaomba mungu hili liendelee kuwa hivyo.
Hadi 2015 .
Mwaka huo tufanye reshufle na tumchukuwee kijana mwihgine ambaye ni mheshimiwa Diwani wa Kata ya Igoma,Mh Adam chagulani awe mgombea wa Nyamagana.

Kitendo cha CDM kulichukuwa Jimbo la Rorya kitaimarisha chama katika ukanda wa Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla.na kutufanya tuweze kujitanua zaidi hadi serengeti na kwingineko katika kanda ya ziwa..

Naomba kuwakilisha kwa nia nzuri, lakini nikitarajia maoni mbalimbali kwa nia nzuri na kwa maslahi na ustawi wa taifa letu na vizazi vijavyo.

Mkuu sizijuhi sana siasa za kanda ya ziwa,ila pia itategemea na kukubalika kwa Wenje Rorya!ila ni wazo zuri ulilolitoa
 
wazo zuri ni kweli jimbo la nyamagana kuna historia ya kutomchagua mbunge kwa mala ya pili mfululizo. support
 
mawazo mazuri lakini tupime mazuri ya wenje uchaguzi ujao.lakini mimi ni mzaliwa wa rorya nimekaa sana rorya,ila wenje ameonesha njia ila kwa wananchi wengi wa rorya hafamiki sana.kama wana rorya wakimkubali ni vema.ila kwangu mimi nngefurahia sana kama mabere marando angegombea 2015 kwa sababu anafahamika sana na wananchi bado wana kiu naye kuchukua jimbo tena sana.
 
acha kudanganya kuhusu marando. Marando akigombea rorya hapati kabisa, kwani wananchi wa rorya bado wanajua na kukumbuka jinsi alivyowasaliti kipindi chake cha ubunge. Marando alivyokuja dar hakupata kurejea tena na kuonana na wananchi mpaka uchaguzi mwingine. Chadema wakimpeleka tu marando, rorya hawaipati kabisa.

Wazo la wenje kidogo inaweza kuleta maana japo maandalizi yaanze sasa.
 
Bonge la mtihani kwa CDM...Adam yuko powa sana na nilimshuhudia ma juzi pale Kirumba kwenye kimbembe cha uchaguzi mdogo akiwa kampeni meneja wa mgombea wa CDM...Yaani dogo ana mvuto kama ule wa Wenje.
 
Pumba tupu. Mnajadili kwa historia,mmesahau kuwa mambo hubadilika na nyakati?.NANI KAWAAMBIA NYAMAGANA WAMEMCHOKA Jembe?.Au bado mnahisia za Ki-Masha Diallo?. Magamba bana,yanahangaika sana.
 
kwa nini adamu chagulani asiende kugombea rorya?
kwasababu rorya ni kijijini na kamwe hawawezi kumchagua mtu ambaye siyo mzaliwa wa rorya. Tofautisha mazingira ya mjini na kijijini. Ni hakika kwa rorya ni lazima awe mzaliwa na kijana wa fulani au marehaemu fulani. Tofauti na hapo ni maumivu tu.
 
Wanaoafiki waseme ndio ....Kimya.Wanaokata waseme sio ....Siooooo.Waliosema sio wameshinda.
 
Kumbuka watu wa Kanda hiyo Tarime/Rorya wana tabia ya kuchagua mtu ambaye anakuwa nao karibu awe mzaliwa wa huko na anakaa huko au hata kama hakai huko lakini muda mwingi amekuwa akiwatembelea kabla ya kutangaza nia, ndio maana hata yule wa Tarime ambaye walimpa kibano; mbinu chafu zilitumika akachaguliwa na asipokuwa makini huenda asirudi.
 
mawazo mazuri lakini tupime mazuri ya wenje uchaguzi ujao.lakini mimi ni mzaliwa wa rorya nimekaa sana rorya,ila wenje ameonesha njia ila kwa wananchi wengi wa rorya hafamiki sana.kama wana rorya wakimkubali ni vema.ila kwangu mimi nngefurahia sana kama mabere marando angegombea 2015 kwa sababu anafahamika sana na wananchi bado wana kiu naye kuchukua jimbo tena sana.

Nadhani wewe ndo umeongea suala la msingi sana. Mabere agombee huko rorya, Sisi wananyamagana tunamhitaji Wenje wetu; Suala la nyamagana kutorudisha mbunge, ni hali halisi ya CCM kushindwa kutumikia wananchi ambayo ilifanya watu waoneshe hasira zao kwa Mbunge aliyekuwepo; SASA wenje hayuko CCM yuko CDM na ni ukweli kuwa CDM inatumikia wananchi, Wenje tunamshauri apige kazi nyamagana bado ni yake kwa mihura kadhaa.

Namshauri huyo diwani wa Igoma aende Magu mjini, Busega etc akahuishe chama na aombe ubunge kupitia majimbo hayo
 
Wenje akigombea Rorya hapati hata kwa dawa! Watu wa Rorya nawafahamu na mimi mwenyewe ni mwanarorya!
 
wana JF,
Nikiwa mtanzania mwenye nia njema na nchi yangu,haya ni maoni yangu binafsi.nitakubali kupokea changamoto au maoni toka kwa mwana JF yoyote mwenye maoni tofauti na mimi,pia hata wahusika waheshimiwa wenyewe kama wamo humu.

Kulingana na hali halisi ya siasa za Rorya,nikizingatia kauli niliyowahi kumsikia mheshimiwa Lameck airo katika kituo cha televisheni ya ITV akisema (ilikuwa kipindi cha ahadi majimboni) hatagombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa 2015.

Ni dhahiri kuwa Nafasi hiyo itakuwa wazi kwa CDM kulichukuwa,tukizingatia kuwa tuna kijana mzalendo wa kweli ambaye ni mzaliwa wa jimbo husika Mh Ezekiel wenje. Ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika medani za siasa nchini na uwakilishi wa kweli.

Katika jimbo la Nyamagana kumekuwa na tabia mazowea ya kutomrudisha mbunge mmoja katika nafasi hiyo kwa awamu mbili mfululizo,bali wana uwezo wa kukipa chama nafasi ya uwakilishi bungeni kwa vipindi kadhaa,lakini kwa mgombea mpya kwa kila awamu (historia imetuonyeshha mara zote katika chaguzi zilizotangulia )

Sijui ni kwa nini tabia hii imechukuwa nafasi,(hili nalo linahitaji mjadala kulijadili). kwa hali halisi bado CDM wana nafasi kubwa na ushawishi wa kutosha mpaka sasa.na ninaomba mungu hili liendelee kuwa hivyo. Hadi mwaka 2015.

Mwaka 2015 ifanyike reshufle na tumchukuwee kijana msomi mwihgine ambaye ni mheshimiwa Diwani wa Kata ya Igoma,Mh Adam chagulani awe mgombea wa Nyamagana.

Kitendo cha CDM kulichukuwa Jimbo la Rorya kitaimarisha chama katika ukanda wa Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla.na kutufanya tuweze kujitanua zaidi hadi serengeti na kwingineko katika kanda ya ziwa..

Naomba kuwakilisha kwa nia nzuri, lakini nikitarajia maoni mbalimbali kwa nia nzuri na kwa maslahi na ustawi wa taifa letu na vizazi vijavyo.
Ni wazo nzuri,kamanda wenje namkubali na anafaa kuwakilisha rorya,tuombe naye akubali,nitapiga kambi utegi kwa nguvu zangu zote
 
hv nyie huyo adam mnamjua au mnamsikia igoma imemshnda nyamagana ataiweza? anaongea sawa lakn hatumii busara tumepigana kupata udiwan amepata tu akahama na igoma kaenda kupanga nyakato mara kashkwa na mke wa mtu.ajichunge sana fika stend igoma uone ilivyokuwa 2010 na leo, sa hv hamna hata bendera moja ya cdm cjui kawafanya nn wanaigoma
 
ushauri mzuri lakini kwa msisitizo lipitishe kwenye chama zaidi ili wakiona inafaa wakweke mkakati wa kulitekeleza
 
Back
Top Bottom