2015 Ubunge Moshi vijijini hapatoshi ni Kati ya Cyrili Chami Dr. VS Hansi Mmassy

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,808
1,225
Cyrili Chami na Hansi walikutana kwenye kinyang'anyiro cha ubunge 2010 wote wawili kupitia tiketi ya CCM. Chami alibwaga Hansi na kupeperusha bendera ya CCM, ambako final Chami alipambana na komu wa Chadema na alimshinda Komu na kuwa Mbunge wa Moshi vijijini. Kwa sasa Chami amekuwa akitoa kauli kama vile ni mpinzani au anataka kuhamia upinzani lakini ukweli ni kwamba atagombea tena Ungune kwa kupitia tiketi ya CCM.

Hansi Mmassy tayari amejikita jimboni kuhakikisha kuwa anang'oa Chami na anatumia advantage ya udhaifu wa Chami kushindwa kutatua kero za wananchi na amedhamiria vilivyo kumng'oa Chami.

Kwa upande wa Komu yeye hajaonyesha activeness yeyote jimboni amejikita zaidi na mambo ya CDM makao makuu.
 
Tiba

JF-Expert Member
Jul 15, 2008
4,596
2,000
College mate hao wanapambana. Nafahamu Dr. Cyril Chami, Hans Mmassy na Komu walikuwa chuo kikuu cha DSM mwaka mmoja.

Tiba
 
MT KILIMANJARO

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
4,217
1,225
Cyrili Chami na Hansi walikutana kwenye kinyang'anyiro cha ubunge 2010 wote wawili kupitia tiketi ya CCM. Chami alibwaga Hansi na kupeperusha bendera ya CCM, ambako final Chami alipambana na komu wa Chadema na alimshinda Komu na kuwa Mbunge wa Moshi vijijini. Kwa sasa Chami amekuwa akitoa kauli kama vile ni mpinzani au anataka kuhamia upinzani lakini ukweli ni kwamba atagombea tena Ungune kwa kupitia tiketi ya CCM.

Hansi Mmassy tayari amejikita jimboni kuhakikisha kuwa anang'oa Chami na anatumia advantage ya udhaifu wa Chami kushindwa kutatua kero za wananchi na amedhamiria vilivyo kumng'oa Chami.

Kwa upande wa Komu yeye hajaonyesha activeness yeyote jimboni amejikita zaidi na mambo ya CDM makao makuu.

Mmassi amejichelewesha mwenyewe kua mbunge kwa 2010 kupoteza dira wakati wananchi walikua wanamkubali. 2015 labda ajie upande wa pili lkn kwa ccm hana chake. KOMU yeye hana mvuto wa kisiasa na amekua mzigo kwa wana moshi vijijin yaani hauziki. Naishauri cdm mda wakuachana na Komu kama mgombea mosh4 vijijini umeisha tutafute anayekubalika. Mimi nikiwa mpiga kura wa mosh4 vijin tokea kata ya old mosh magharibi nasema Komu na Chami hawatufai.
 
NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,808
1,225
Muda wa kupita majukwaani bado fanya kazi ugombee wewe.

Unanishauri nigombee kwa Chama gani? kwa nini na wewe usigombee? Muda wa majukwaani bado lakini kwa sasa ndio wanafanya ground work
 
kitongoroso

Member
Nov 3, 2013
29
0
chami hajafanya chochote jimboni japokuwa nasikia ameshaweka pesa mingi ya lowasa mfukoni anataka kuja kuwanunua tena wananchi wa moshi vijijini. Kwa kifupi chami namshauri atafute kazi pale UDSM atusaidie kufundisha vijana huku aliko ni kutuibia tu. Anapita jimboni na kujidai kujenga bara bara ila kiuhalisia bara bara hizo ni ahadi ya mh raisi kama zilivyojengwa mikoa na majimbo mengine kwa kifupi hata kama chami au jimbo lisingekuwa na mbunge bara bara zingejengwa tu. Nasikia alienda ulaya akaleta mavitabu outdated na kuvigawa jimboni kwenye mashule, vijtabu vile havina msaada wowote kwa wanafunzi sijui atawaambia nn wananchi wa moshi (v) 2015.

Kwa upande wake Hans sijamfahamu vizuri nasikia ni mfanya kazi wa vodacom na ameshaanza ground work vikao vimeshamiri kweli. Ila nafikiri moshi vijijini mnahitaji sura mpya ambayo haijawahi kugombea ili kuondoa mtifuano huu uliopo.
 
gilbert14

Senior Member
Oct 17, 2014
133
0
hans nani akupe kura jitambue kwanza ndo ugombeee chami ni nguzo ya wana kb mtajikomba sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom