2015 tunahitaji Rais atokanaye na mtandao binafsi?

kwitega

Senior Member
Apr 10, 2012
166
49
Wakuu,

Nimeamua kuleta kwenu hoja hii ili tuijadiri kwa kina kutokana na hali ya kisiasa nchini kuelekea 2015. Kama tunavyokumbuka; mara baada ya kuingia madarakani mwaka 2005, Rais Kikwete alisema alianza maandalizi ya kusaka urais tangu mwaka 1995. (kuunda mtandao). Mtandao huo ambao ulikuwa chini ya mtuhumiwa wa kashfa ya Richmond Edward Lowassa ulifanya mengi katika kuhakikisha unashinda. Vyombo vya habari vilitumika kadhalika baadhi ya viongozi wa dini walidiriki kusema JK ni chaguo la Mungu. Hata hivyo kauli hizi leo zinaonekana mbele ya wengi kuwa ulikuwa ni mkakati wa wanamtandao kwani kila uchao ni afadhali ya jana mjini na vijijini.

Mtandao chini ya Lowassa uliwachafua akina Dk Salimu, Sumaye na wengine. Yote hayo yalifanyika kuhakikisha kuwa JK anaingia Ikulu 2015. Kibaya zaidi mara baada ya kuingia madarakani; JK aliteua viongozi mbalimbali serikalini kwa kuangalia nani alifanikisha nini kumfikisha hapo alipo. Matokeo yake tunayaona hadi sasa. Baadhi ya watu wanajiona wanaubia katika urais wake, hawezi kuwawajibisha hata wanapokwenda kinyume na maadili ya uongozi. Ndiyo hapo tunawasikia watu wa aina ya Lowassa wakisema serikali haichukui maamuzi magumu. Lakini Lowassa anasababu ya kutoa kauli hizi wakati yeye mwenyewe alikuwa kinara wa mtandao unaolitesa taifa hadi sasa? Au kwa vile alikumbwa na kashfa ya Richmond akaachia ngazi sasa anajaribu kujiosha?

Akiwa mmoja wa wanasiasa wanaotajwa kuwania urais 2015, Lowassa anadaiwa kutoa pesa nyingi Wilayani na Mikoani ili kuhakikisha kuwa wagombea anaowataka kwa nafasi mbalimbali ndani ya CCM wanashinda. Hii ni aina ya mtandao ule ule alioongoza hadi kumfikisha Ikulu rafiki yake ambaye hawakukutana barabarani. Kama ilivyokuwa mwaka 2005, kwa vyovyote vile wapo pia wafanyabiashara halali na haramu kwa ajili ya kutunisha mfuko wa kuhonga wapiga kura sasa na baadaye kama atafanikiwa kufika huko. Kumbe rais wa nchi hii anaweza kufadhiriwa na wafanyabiashara haramu. Je, akipata madaraka wafanyabiashara hao hawatamwamuru kufanya wanavyotaka wao iwe kwenye biashara zao au kwa raslimali za taifa? Je, kwa uzoefu ule ule wa 2005, kama Lowassa atapitisha na ccm kugombea urais na kisha kwa njia halali au haramu akashinda au kutangazwa mshindi wa kiti cha rais, ataacha kugawa vyeo kama njugu kwa mtindo ule ule wa kwamba huyu ni mwenzetu alifanikisha mtandao kwa kiasi fulani apewe nafasi hii au ile? Je, kama Lowassa atafanya hivyo; yale maamuzi magumu anayosema kwamba rafiki yake hachukui, yeye atakuwa na ubavu wa kuyachukua kwa maslahi ya taifa? Hii si pata potea? Tunahitaji tena rais mwingine anayetokana na mtandao? Naomba tujadiri bila kujali matumbo yetu leo, baali kuangalia maslahi ya taifa zaidi leo na siku zijazo.
 
Back
Top Bottom