2015 mgombeya uraisi wa tanzania awe mzanzibari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2015 mgombeya uraisi wa tanzania awe mzanzibari

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtwike, Mar 30, 2011.

 1. M

  Mtwike Senior Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni jambo la kusikitisha, toka kuanza kwa vyama vingi, hapajakuwako na chama chochote cha siasa kilichopendekeza mgombeya Uraisi wa Jamhuri ya Muungano, kutoka visiwani! Hii inatowa taswira gani, hawana uwezo au hawastahiki? kuna haja Katiba mpya, ibaini wazi kuweko uongozi wakupishana, vinginevyo itatowa fikra ya kuwa daima watawala ni Wabara na wavisiwani watawaliwa,

  Naomba kutoa hoja!
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  RAIS WA TANZANIA AJAYE (TULIYE NA HAMU KUBWA KUMPATA CHINI YA KATIBA MPYA) ATAPATIKANA TU KWA MISINGI YA USHINDANI MKALI NA UBORA WA SIFA ZA MGOMBEA NA WALA SI KUPANGA LOLOTE KABLA YA SIKU YA MNADA!!!

  Sawa tu, kwani shida iko wapi??? Ni sifa tu ndizo zitakazogomba laa sivyo hakuzuiliwi mtu hapa.

  Isipokua ikumbukwe kwamba tulihiari wenyewe kuingia na kushiriki mfumo mpya wa vyama vingi ambapo kikubwa zaidi ni kwamba kila kitu ni sharti kiendeshwe KIUSHINDANI na wala si kutengeana viti kama ambavyo tulivyozoea huko nyuma kwenye mfumo wa chama kimoja ambapo competitive edge ilikua ni kwa misingi ya POLITICAL MONOPOLY of decisions and destinies.

  Kwa mantiki hii, mpangilio wa ndani ya chama fulani kujiamulia kwamba wao wanajipangia rais atoke mkoa fulani au kona fulani ya nchi kamwe haitoathiri NDHANA MPYA WA SIASA ZA USHINDANI ambapo sheria kuu ya mchezo katika Mfumo huu mpya ni kule Wapiga Kura, Vyama Vya siasa na Wagombea wenyewe wa nafasi mbali mbali nchini KUTOKUACHA MWANYA WOWOTE WA KUHISIWA kukaa mahala na kupanga bei (wagombea gani washiriki) na hivyo kufanya kushindwa kwa Soko la Siasa KUTOKUA HURIA na hata nguvu za Demand and Supply kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

  Wenye wagombea wenu wa urais kichwani, CCM na vyama vya upinzani, kumbukeni kwamba siku zote Ng'ombe Hanenepeshwi siku ya Mnada hivyo fanyeni kazi na kujaribu kuonyesha YOUR BEST tangu hivi sasa maana huko mbeleni hakutokwepo na SHORT-CUTS (Uchakachuaji) tena wala kutafutwa kwa SECOND CHANCE kama hivi sasa Mhe Kikwete anavyolihangaikia na kulilalamikia usiku na mchana kwa CHADEMA.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ACHENI JAKAYA KIKWETE AISHI KWENYE MABAWA YA MIDEGE ANGANI AKICHAGUA ILMRADI GHARAMA YA KODI ZETU KUIFADHILI MIRADI HIYO HAIZIDI ROBO YA TIJA TUNAYOVUNA KWENYE MAPENZI YAKE HAYO!!!

  Hivi PakaJimmy, huenda huyu mwenye bandiko lake,anayeshabikia ovyo matembezi ya Mhe Jakaya Kikwete Wizara moja baada nyingine bila kutupa VERIFIABLE FACTS and FIGURES juu ya ushabiki wake, akawa ni Rweyemamu wa Ikulu kule Magogoni, Katibu Mwenezi na Propaganda CCM au ndio tuseme Zilipendwa Mzee Tyson Wassira Waziri wa Uhusiano leo hii kaamua kutoka Ki-Doti-Komu vile nini??

  Tathmini ya huu Mradi wa ziara ya Mhe Kikwete Mi-Wizarani kamwe haitofanywa na akili za kilabuni hivi; tutakwenda mbele kidogo na kutaka ripoti iliyoandaliwa baada ya kutumia vigezo vya kisayansi (Project Monitoring and Evalution) ili kubaini kwamba tangu anapanga ziara hii.

  Ni sharti JK atujibu kwa mtaji wa kodi zetu anazoendelea kutumia hivi sasa katika 'Kikwete Tembelea Wizara Project' (KTWP) na wal si kutupigia kelele za kishabiki hapa; huko kwenye siasa za kishabiki Vijana hatumo bali ni kwamba TIJA tu ndio tuwekewe mezani kweupe. Washiriki wa KTWP watujibu maswali kama vile Kikwete: (1) alikua na makusudio yepi, (2) kakuta hali halisi ikoje, (3) hali hiyo inajilinganisha vipi na kipinda cha mara ya mwisho mradi kama huo ulipotendeka, (4) Wa-Tanzania tumelazimika kuwekeza kiasi gani katika hiyo Month-Long Kikwete Project na iko wapi thamani ya kodi zetu mle????

  Dr Bila ripoti tunaomba tangu ziara na familia yako mbugani na kote huko mikoani. Wapinzani na wabunge wote kwa ujumla nanyi tutawabana sana juu ya jinsi gani Viongozi Waandamizi wanavyotumia kodi zetu na TIJA za wazi zinazopatikana kwenye kile watendalo tukilinganisha na gharama iliotumika. Tukizingatia nidhamu kama hii tangu ikulu hadi nyumba kumi mitaani kwetu basi wananchi tutaona ACCOUNTABILITY wa hali ya juu!! Huko nyuma JK ameripotiwa kuwa na ziara nyingi sana na hata wakati mwingine kudaiwa kuwakera walipa kodi.

  Kwangu mimi sitojali ziara zake ni nyingi kiasi gani ba ni thamani ya tija iliyopatikana ukilinganisha na gharama tulizowekeza mle. Tena mimi nitamuunga mkono sana JK akiweza basi kila siku awepo tu kwenye pipa angani kila kukicha ilmradi UNPOLITICISED WATCHDOG POLITICAL GROUPS AND PARLIAMENT wanaturidhisha katika hili bila swali kubaki kichwani mwetu.

  Tunasupibi ripoti bungeni juu ya matumizi kwenye mradi huu na vile vile kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi akajikite katika TIJA zenye kugusika na kuonekana tulizozivuna kwenye KTWP. Hatutaki blaa blaa na longo longo nyingi za mwaka wa 47 ambayo ndio haswa imetunashisha kama taifa kwenye huu umasikini gundi mabegani.

  Mhe Kikwete kama CEO wa Tanzania kwa sasa, kama angelikua anaongoza kampuni ya kibiashara lazima angelazimika kuridhisha Wajumbe wa Bodi (Wahe Wabunge, nchi wahisani na Asasi za Kiraia husika) na haswa wamiliki wa kampuni (sisi wananchi) juu ya kila atendalo na faida ya kuonekana bila siasa, kwa nini ishindikane kwa ngazi ya taifa endapo kweli hatukusudii kuja kupata misaaada to Rwanda au hata Kenya kutupa LIFTI KWENYE NDEGE YAO toka kwenye hatari Libya????
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Zanzibar ya nini?
  Wana raisi wao mimi naitaka Tanganyika yangu,...sioni umuhimu wa Zanzibar zaidi ni mzigo kwetu, wana feed on us kama kupe kwenye ng'ombe!

  Afu leo waongoze Tanganyika? Kwanza nani huyo wa kuongoza Tanganyika toka zanzibar?
  Gi'me a break
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Vipi yakhe? Mnataka mle kwenu na kwetu pia? Mnaye rais wa Zanzibar na makamu wake. Mnae makamu rais wa mwungano ambaye ni Mzanzibari. Mbona mnakuwa waroho?
   
 6. M

  Mtwike Senior Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lamsingi, tunaposema Tanzania ! nimetowa hoja juu ya hali iliotanguliya toka kuanza vyama vingi!

  Ikiwa tutakuwa na Tanganyika, hakuna ugomvi, lakini kitu Tanzania ni Muungano na kila mwenye hisa katika muungano ana haki sawa na mwenziye. Ni kwa mantiki hii ndio zanzibar ina haki ya kuwa na mgombeya wa Tanzania. Ama hoja ya wazanzibari wana Raisi wao, ni sehemu ya mapungufu! kwani hana madaraka Bara, na kinyume chake, wabara ana madaraka visiwani!
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Ninyi endeleeni na kujadili katiba mpya na Muungano na muundo wake.
  mukishindwa kutumia bahati hii iliyojitokeza ndio musahau kuona rais wa serikali ya TZ kutoka Zanzibar.

  Kama nchi moja mbia wa muungano, ninyi munaweza kuja na proposal ya ku-rotate huo urais wa Muungano.
  Kama munao wanasheria wazuri basi watumieni ili kuweka hoja hiyo kisheria lakini musije mukachukua mawakali kama wa Tanesco kwenye kesi ya dowans! Itakula kwenu.
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.

  Mimi nafikiri hoja aliyoleta mleta mada inahitaji tafakari.
  kwa sababu gani?
  Wanazungumzia Serikali ya Muungano.
  Kweli wao wanae Rais wao, rais wa Zanzibar.
  Sisi tunapokimbia kujifanyia self criticism basi tutabaki katika kuwakejeli Wazanzibari au kujenga chuki ambayo inatokana na uvivu wetu wa kufikiri.
  Vipi wao wawe na serikali ya Zanzibar ,sisi tusiwe na serikali yetu ya "Tanganyika" aka Tanzania bara?

  Kama tunachukua jukumu hili la kufikiri basi itatupelekea kuwataka wabunge wetu wa "Tanzania bara" waturejeshee serikali yetu ya Tanganyika.

  Hii serikali ya Muungano inaweza kuchukua models za EAC au EU na hivyo kutuondoshea huu unafiki na usanii tulionao leo.

  Lazima ifike siku na muda tuseme ukweli, tusiendelee kujidanganya.
  Why our union should be so special and unique yet so complicated and itching?
   
 9. M

  Mtwike Senior Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thnx 4 ur comments.
  Hakuna kitu mawakili wazuri, system imeshika mpini, watakalo huwa! Kwani umesahau tume ngapi zilikuja na mapendekezo mazuri, lakini zikapigwa na chini! haikuwa ya Nyalali akiwa madarakani, ikatupwa huko, usichezee system bro. husubiri mpaka mambo yawageukiye, kama ya Mubarak....!
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Speaker
  It refreshing to see more and more people use the original name of our beloved country, Tanganyika instead of Tanzania bara.

  Let us not stop there!
  We need a movement to get Tanganyika back on the map of the world!

  Nani wa kumfunga paka kengele?
  Will this remain only a key board noise?
   
 11. M

  Mtwike Senior Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani tatizo ni jina la hiki kacheo cha raisi wa Zanzibar! hivi ana madaraka gani zaidi ya Mkuu wa Mkoa? ni kiini macho tu, eti ana bendera ana wimbo wa taifa, anapiga baruti 21 akipokeya mgeni, lakini ana Nchi ikiwa haina "sovoreignity"?
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mtwike.

  Tatizo ni tatizo lakini kujua tatizo ndio mwanzo wa kupata mwanga wa kutatua tatizo lenyewe.
  kwangu mimi hilo si tatizo kubwa. Ni tatizo la kujitakia.
  Hapo Zamani za kale...miaka 47 iliyopita nchi mbili ziliunganisha mambo kumi na moja. muungano wa mambo hayo ukazaa Muungano ulioitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Baadaya ya miezi kupita , yule mjanja mmoja akasema ,Hili jina ni refu kwa hiyo tuyaunganishe...Akatutengenezea jina Tanzania...kwa bahati mbaya jina moja la nchi mbia likasukumwa chini ya zulia. na kila anayelitaja anaonekana ni mhaini.

  Kale kanchi kengine kadogo kikaendelea kutumia jina lake.

  Sasa kama kanchi kadogo hakistahili tena kuwa nchi sasa kiwe kamkoa hili kweli ni tatizo, tena sio tatizo dogo....yaani hata kama ningekuwa mimi ndio mmoja wa wananchi wa nchi hiyo..ningepigana na yeyote ambaye anataka kanchi kangu kawe mkoa.

  Guys, we have a big problem here.
  Vipi ungeweza kunishawishi, nchi inayofanya muungano na nchi nyengine ikubali kuwa mkoa?
  Halafu usiri wa kutoonekana hati original ya makubaliano ya Muungano pia yanaongeza kiwingu juu ya tatizo hili la kujitakia.
   
 13. M

  Mtwike Senior Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili si tatizo la kujitakia bro, ni tatizo lilopangwa!
  Mwezi mmoja tu baada ya Muingereza kutoa Uhuru, nchi yapinduliwa na waliowengi, miezi Mitatu kanchi kaungana na nchi kubwa zaidi ya mara Mia kiiukubwa na idadi ya Raiya, upanda wa pili wa bahari tena hawana common tribe wala common culture! yote haya kujitakia? call a spade a ........
   
 14. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  At the time Zanzibar was insecure. If the sultan had organised himself and sought assistance from his kith and kin in the Middle East he could have retaken the islands back. Karume new that and that is why he agreed to the Union. He was not forced. He wanted protection. Now that they are sure the sultan is not coming back they can't stop whining. I sincerely believe even today Zanzibar is getting more out of the Union than Tanganyika. What would we lose if the union broke down? I would say 'not much'. What would they lose if the union broke down? Quite a lot ..... residences on mainland (every Zenj leader has at least one house on mainland), businesses (wapemba shops), land (they are entitled to land on mainland but we are not in Zanzibar), cheap goods (especially foodstuffs. Most of their food is sourced from mainland tax free), political positions and influence (they have MPs in the Union Parliament which also happens to be the Tanganyika Parliament. They therefore make laws for us. We don't have representation in their Baraza la Wawakilishi. Lets face it. Being in the Union gives them clout on the international stage which they otherwise would have as an island nation). I think we should grant them their wish to break the union and then tighten the screws on other fronts to let them learn the real facts instead of political demagoguery.
   
 15. M

  Mtwike Senior Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ufinyu wa maarifa yako kuhusu Zanzibar, unanizuiya kukujibu kwa data! unasahau znz ilikuwa ni nchi yenye uwezo kiuchumi, taaluma kimaendeleo na mambo mengi kuliko Bara, kabla Muungano? nikuthibitishiye vipi ikiwa unamuona Sultani ni mgeni na Karume ni mwenyeji! I can't help it, Ican't correct your ignorance, sorry!
   
 16. M

  Mtwike Senior Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maskini, unakwepa mkojo na kukanyaga kinyesi, unaukataa ubwana na kuutaka utumwa? Wote CCM na Chadema are birds of the same feathers!
   
Loading...