2015 kazi ipo lakini hali ikiendelea hivi ccm .............................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2015 kazi ipo lakini hali ikiendelea hivi ccm ..............................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wakuziba, Jul 4, 2012.

 1. w

  wakuziba Senior Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwanza niseme kuwa nimeandika makala hii kwa nia njema kabisa. natathmini hali halisi ya vyama vyetu vya siasa kwa ujumla. siku zijazo nitachambua chama kimoja baada ya kingine kwa kuelekea 2015.

  kitu kikuu ambacho raia wanakitegemea na wana haki ya kukipata kutoka katika serikali yao ni MAENDELEO NA MAISHA BORA. maendeleo ambayo yanaleta maisha bora kwa raia wote. tuna mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992 (1995). demokrasia inakua taratibu! si haba! kabla ya kuchambua kila chama kwa muhtasari, tujikumbushe kwanza kuhusu hulka ya mtanzania  HULKA YA MTANZANIA IKOJE?
  Mtanzania ana tabia ya uhafidhina. siyo mwepesi kubadilika. mifano ipo mingi lkn niende kwenye soka. tuna timu kubwa za simba na yanga. miaka nenda miaka rudi ni simba na yanga. azam, mtibwa, coastal, majimaji, jkt, kagera, toto nk... wamekua wasindikizaji kwa muda mrefu. nchi zilizotuzunguka, wana kawaida ya kuwa na mabadiliko kila mwaka kwenye uongozi wa ligi. kenya kulikua na gormahia na afc leopards kwenye chati, uganda kulikuwa na kcc, villa na express, malawi kulikua na bata bullets, na zambia kulikuwa na nkana red devils. hizi timu zilitamba miaka ya nyuma. raia wa nchi nilizotaja, wamekua wakishabikia timu inayofanya vizuri. hawana uhafidhina. HAPA KWETU HATA TIMU IKIFANYA VIZURI MADHALI SIYO SIMBA AU YANGA, watanzania hawana habari nayo. HII NI ISHARA YA UHAFIDHINA WA WABONGO. kumhamisha mtanzania na kubadili mtazamo na fikra zake ni kazi kubwa sana! kwa upande wa siasa, kuna watanzania ambao huwaambii kuitu kuhusu CCM. siyo mijini wala vijijini. wana imani kubwa sn na ccm. Na wako tayari kufanya lolote kuihami ccm. HII NI ISHARA NYENGINE YA UHAFIDHINA WA WABONGO.


  HALI YA VYAMA VYETU IKOJE?
  chama cha ccm ni chama kikongwe. kina makada wazoefu wa siasa za kila aina. siasa barid, siasa safi na siasa chafu. kina mabingwa wa propaganda. pana uwezekano, kina mamluki ktk KILA chama cha siasa. kina sifa kuu moja: kimeunganisha watanzania kutoka ktk kila kanda, dini, rangi na kabila. hali hii imetokana na kuwa chama pekee kwa miaka mingi hadi mwaka 1992. huwezi kusema ni cha wakristo au waislamu. wote ni chama chao. Kina kasoro nyingi ambazo zinatokana na KUKOSEKANA UWAJIBIKAJI NA UTAWALA BORA. kinasuasua ktk kuwaadhibu wanachama wake wanaotajwa ktk kashfa mbalimbali za rushwa. kukumbatia wala rushwa ni ishara ya kwamba rushwa ipo na imeshamiri. hali hii inatusababishia maendeleo duni. Baadhi ya wapinzani wanasema maana ya ccm ni chukua chako mapema. Kauli hii inatokana na wizi wa mali ya umma wakupindukia wa viongozi wa serikali.

  ccm wana hali ngumu kuhusu mgombea urais 2015 lkn wana sifa moja. wanaweza kwenda dodoma (kizota) wakiwa na tofauti kubwa. la ajabu wanatoka wakiwa kitu kimoja na wagombea wanapeana mikono. sijui huwa wanafanyaje!!!!!!!!!!!!!


  chama cha chadema ni chama ambacho kimefanya vizuri sana ktk uchaguzi wa mwaka 2010. idadi ya wabunge wake imeongezeka sana na ndiyo chama kikuu cha upinzani. kina viongozi jasiri ambao niwabunifu na hawana uwoga ktk kueleza na kutetea ukweli.
  Chadema kina kasoro kadhaa zifuatazo:-
  a). viongozi wake wakuu wana ushindani wa kisiasa, sifa na umaarufu. hili ni tatizo kuu chdm. kushindana huku kumewafanya waogopane na kuoneana wivu. wanaweza kuonekana wana safu moja lkn ukiangalia kwa jicho la kiuchambuzi utagundua kuwa slaa, mbowe, zitto, lissu, msigwa, mnyika nk...... wana matabaka ya ndani kwa ndani.

  b). chama chochote lazima kianzie ktk eneo mojawapo ktk nchi yetu. chdm kilianzishwa na mtanzania kutoka kasikazini. bila shaka mizizi yake ilianza kuimarika kaskazini. ccm wakatumiya mwanya huu kukipaka matope kuwa ni chama cha kikanda na kikabila hadi wakatafsiri chadema kuwa ni chagga development manifesto (ilani au mradi wa kuwaendeleza wachagga). hali hii imefanya watanzania wengine waogope kujiunga na chama cha chdm.

  c). ccm wamepakaza kuwa chdm ni chama cha wakristo. wakawa wanatoa mfano wa viongozi wake wakuu. wakasema dk. kabourou alipokua katibu mkuu, alipigwa vita kwa kuwa ni muislamu. kutodhihirika kwa majina ya kiislamu ya bob makani na zitto kabwe, kulifanya watu waamini kuwa viongozi wote wa chdm ni wakristo. chdm hawakujitahidi kuweka wazi kuwa bob makani, zitto kabwe na mzee arfi ni waislamu. japo mzee arfi anajulikana lkn amekua hapewi nafasi ktk majukwaa ya chdm licha ya kuwa ni makamu mwenyekiti. Propaganda za kuwa chdm ni chama cha wakristo, zimewafanya waislamu waliowengi waogope kujiunga chdm

  d). chdm kimeridhika kwa kuwa na mashabiki na siyo wanachama wakereketwa. kimesahau kuwa kasoro ya ccm ktk kura za maoni mwaka 2010, ndizo zilizochangia chdm kupata wabunge waliohama ccm. Vilevile baadhi ya wanaccm walikikomoa chama chao kwa kuipa chdm kura. Hii ilitokana na hasira za kura ya maoni ndani ya ccm. huu ndiyo ukweli kuhusu mwaka 2010. pana uwezekano mkubwa kuwa iwapo ccm itacheza karata vizuri, itarudisha sehemu kubwa ya viti vyake katika uchaguzi wa mwaka 2015. ufunguzi wa matawi ya chdm unafanywa sn vyuoni na nje ya nchi kuliko vijijini. hii ni kasoro!

  e). kinyang'anyiro cha kumtafuta mwenyekiti wa chama na mgombea urais mwaka 2015 nalo ni tatizo chdm. mbowe, zitto na slaa wote nadhani wana nia ya kugombea urais (japo kuna utata kwenye umri wa zitto). slaa alifanya vizuri 2015 lkn wengine wanamuona kama mzee ambae huenda asiwe na mvuto 2015. mbowe ana sifa lkn ile propaganda ya ccm kuwa chadema ina wenyewe, inamgharimu kwa kufanya wanachdm kutoka mikoa mingine wasimkubali.


  f). lugha inayotumiwa na wanachama wa chdm kuwaelimisha wanachama wa vyama vingine ni kali sn. Inatumika jazba sn kuliko busara! Hili jambo linafanya ongezeko la wanachama chdm kusuasua  chama cha wananchi cuf hakikufanya vizuri mwaka 2010 tofauti na chaguzi zilizotangulia. ni chama ambacho kina kasoro zifuatazo;
  a). uongozi wa juu wa chama haubadiliki. japo lipumba na maalim seif wamejaribu kufafanua kuwa wao ni wapiganaji ambao wako vitani. makamanda huwa hawabadilishwi kama nguo. malengo yatapotea. kutobadili viongozi wa juu kumetumiwa na ccm pamoja na chdm kuisulubu cuf.

  b). ccm ilianzisha propaganda kuwa cuf ni chama cha waislamu. kama ilivyo chdm, cuf nayo ilianzia sehemu mojawapo ya jamhuri yetu. wakazi wa eneo la visiwani wengiwao ni waislamu. cuf ikawa na wanachama wengi wa mwanzo wakiwa waislamu. hali hiyo ikatumiwa kisiasa na ccm kuwa cuf ni chama cha kidini na wakristo waliowengi jambo hilo limewatia hofu kujiunga cuf!

  c). licha ya profesa lipumba kuwa msomi lkn ameshindwa kuwavuta wasomi wenzake kujiunga na cuf. chdm kimefanikiwa kuwavuta wasomi wengi tu! kosa hili la lipumba limekiathiri sn chama.


  d). safari za mara kwa mara za lipumba nje ya nchi zinachangia kudumaza chama.


  e). hakuna asiejua hali na mpasuko wa kisiasa ulivyokua visiwani kati ya ccm na cuf. ilifikia waamue kuungana ili kusitisha tofauti zinazo irudisha nyuma znz. ni jambo zuri lkn chdm wamelitumia kwa kuisulubu cuf. wanaiita ccm B. si kweli kuwa cuf ni ccm b lkn kisiasa chdm wanahaki ya usema hivyo. cuf wanadai kuwa vile wamo serikalini, 2015 watachukua nchi. hawatoibiwa kura tena. yetu macho!


  vyama vya nccr, tlp, udp nk....... havifanyi vizuri sn. inasemekana kuwa ushindi wa nccr kigoma ni kutokana na mgombea wao urais wa 2010, mzee hshim rungwe kuwa mwenyeji wa kigoma. walimpa kura za "tusimuangushe mtoto wetu...". mrema kwishnei, cheyo yupoyupo........  KWELI CCM ITANG'OKA 2015?
  jibu la haraka ni kuwa HAPANA. pana uwezekano mkubwa wa ccm kushinda. kwa nn nasema hivi?

  1- ccm wanauzoefu wa kumpitisha mgombea na tofauti zao zikaisha. rasharasha huwepo lkn huwa chache sn!
  2- vijijini bado wana imani kubwa na ccm na hata baadhi ya miji.
  3- tofauti za safu ya juu ya chadema zinaweza kukipa zilzala (mtikisiko) kipindi cha uchaguzi wa mwenyekiti na mgombea urais. Hii itakua neema kwa ccm.
  4- propaganda za ukanda na udini zimekua mwiba kooni mwa chadema. hakikubaliki sn kwa waislamu. anae bisha apitie matokeo ya uchaguzi wa 2010 ktk tovuti ya NEC.
  5- cuf imekuwa ikiiharibia chadema. uwepo wa cuf ni kihunzi kwa chadema. na sasa uadui bungeni wa cuf na chdm ni mkubwa.
  6- ili ccm ifanye vizuri, pana uwezekano ikakubaliana kuwapa cuf znz ili wanacuf wa bara wote waipigie ccm. Mpango huu unaweza kuinufaisha ccm huku bara.
  7- siyo siri uchaguzi wa 2010 ulitawaliwa na udini (anaekataa hili atakua na matatizo). ccm ilikua na mgombea muislamu. cuf ilikua na mgombea muislamu. chdm ilikua na mgombea mkristo. wakristo wengi walipeleka kura zao chdm. kura za waislamu wengi zilikwenda ccm na cuf. mwaka 2015, pana uwezekano mkubwa ccm watampitisha mkristo. hali hii itapunguza kura za chadema. maaskofu ambao walikuwa upande wa chdm, wakiona mgombea mkristo ccm, watahama na wafuasi wao kwenda ccm.

  Wakatabahu: wakuziba
   
 2. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  Kuna machache unawezakuwa uko sahihi ila pia kuna mengi yaliyo base kwenye hisia,tetesi,dhana binafsi nk ambavyo kwa umoja wake vinaweza kuikosesha mada yako uzito uliostahili, kama hiyo ya maaskofu kuhama na wapiga kura wao sidhani!!kwani ndiyo haohao waliomsifia jk kuwa chaguo la mungu!hiyo ni hisia na si uhalisia kuna mambo mengi sana yanayoweza kugeuza upepo wa siasa,wala hutaweza kuorodhesha yote kwa kwenye siasa mlima wa mema huweza kufunikwa na kichuguu cha uovu,haya tuombe uzima.
   
 3. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  chdm sijui ni chama gani.mimi ni mwanachama wa cdm au chama cha demokrasia na maendeleo kuwa makini sana neno moja linaweza kupoteza wat
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Makala za aina hii zinapendwa sana na CCM. Subirini 2015 ndio mtajua wananchi walivyowachoka.
   
Loading...