2011 UDSM nilinusurika kukamatwa

Nilimaliza kwa amani.

Na baada ya masomo nimefanya mabadiliko.

Nimejituma kufanya kazi na siasa pia ninafanya kwa kufuata sheria za nchi.

Mabadiliko siyo kuandamana bila sababu ya msingi.
Kumbe hawakua na sababu ya msingi walikuwa wapuuzi tu
 
Sisi tulikuwa na test kule yombo asubuhi tulivyogawiwa tu mitihani tukavamiwa na ilikuwa si mchezo kukiwa na mgomo nyie mkasaliti mnachalazwa hatari tulivyosikia tu wanakuja wanaimba kila mtu haijulikani alitokaje mlangoni si kwa mbio zile kulikuwa na malecturer wawili wakisimamia mtihani walitimua km vichaa test ikawa imavurugwa baada wa mgomo kuisha tulitungiwa test nyingine ilikuwa ngumu km mpingo tulikoma
Nakumbuka sana hili tukio mgomo uliamuliwa baada ya waziri wa elimu ndugu Shukuru kawambwa kufika UDSM na kutangaza kupandisha boom mpaka shilingi elfu 7 kwa siku
 
Huyo huyo Ndunguru akafika revolution square pale, akaanza kutema hoja baada ya muda watu wakajaa, jamaa yuko peku peku anaongea balaa. Kilichokua kinasisimua zaidi ni hoja zilivyokua zinatolewa. Baada ya Ndunguru na wengine kukamatwa sasa ndio chuma Alshabab kilipoamka sasa,, akaanza peke yake ku mobilize watu na kuhubiri. The guy will make a very good politician sijui yuko wapi siku hizi.

Huyu mshikaji mwili wake ulikua hauendani na matendo yake mwili mdogo vurugu nyingi.....Ila kuna mbavu moja ya Duce tulikua tunapoa nayo mabibo ilikua inaamsha sana aisee
 
Hahaha halafu kama sijakosea huo mgomo watu wa COET kama vile walijitenga navyokumbuka ni kama vile walifunga geti lao ngwini wasiingie mule hahaha

Hamkuleta barua rasmi ya maombi kuwajoin kwenye mgomo

Sema mlizingua kuna siku tumepanga tukutane revo square chuo kizima saa4 , coet tukatimba nyie hamkutokea, mkaja saa7 Coet hatupo, mkajikusanya na mademu zenu mkaja kufanya vurugu Coet tuliwachapa tukafunga geti mazima tukaanza mgomo wetu mwingine wa kutaka mwana wenu aliekua discontinued arudishwe tulikiwasha mpaka college nzima tukatimuliwa
 
Nimemkumbuka Mwita alikuwa na kengeza.

Alianza kwa kuandika bango kwa Maker pen nyekundu maandishi makubwa yanasomeka "BOOM 10,000/=" halafu akaenda kusimama katikati ya Barbara ya Sam Nujoma maeneo inakoanzia University Road.

Alishika bango uelekeo wa Ubungo Mataa.

Ninakumbuka alivaa nguo za kaki enzi hizo CHADEMA iliwika sana.
Hapana ile picha aliyoandamana peke yake alikuwa amevaa suruali nyeusi, shati jeupe na tai nyekundu kama sikosei
 
Nilimaliza kwa amani.

Na baada ya masomo nimefanya mabadiliko.

Nimejituma kufanya kazi na siasa pia ninafanya kwa kufuata sheria za nchi.

Mabadiliko siyo kuandamana bila sababu ya msingi.
Unamaanisha yale maandamano yalikuwa hayana msingi?
 
Daah mabibo nilikaaga kuanzia 2nd year hadi mwaka wa mwisho kulikuaga fresh sana misosi pale kwa wale wapemba ilikua si mchezo, victoria hata siikumbuki ilikuaga ipo sehemu gani? Au ule mtaa wa nyuma ulioongozana masteshenari kama ukiwa unakula shato pori?
Haha chakula cha wapemba watu walikuwa wanadai kina walakini, walikuwa wanapima kingi sana watu walikuwa wanajaa hatari
 
Hamkuleta barua rasmi ya maombi kuwajoin kwenye mgomo

Sema mlizingua kuna siku tumepanga tukutane revo square chuo kizima saa4 , coet tukatimba nyie hamkutokea, mkaja saa7 Coet hatupo, mkajikusanya na mademu zenu mkaja kufanya vurugu Coet tuliwachapa tukafunga geti mazima tukaanza mgomo wetu mwingine wa kutaka mwana wenu aliekua discontinued arudishwe tulikiwasha mpaka college nzima tukatimuliwa
Ila na nyinyi mtu wenu aliekamatwa na chabo darasani tukawatoseni tukasema kumbe jamaa ni vilaza wacha wapambane na hali zao hahahaah...
 
Wengine tumesoma vyuo vya kanisa...kwetu utii ilikua ni ticket yako ya kumaliza chuo. Inaonekana nimemisi mavurugu mengi sana vyuoni, hivyo kuna chembe chembe fln za maisha ntakua nimekosa!!!
 
Ni kweli mkuu. Infact kama kuna watu walio andika historia ya kuongezewa pesa ni hawa jamaa akiwepo al shabab.

Ukiacha wale arobain na ngapi waliokamatwa wengi walirud chuo na wengine kuruhusiwa kuaplay maika inayofuata.

Ila main organisers sijui walipotelega wapi.

Bado tunawakumbuka maana through their tears we achieved

Hope huko walipo mambo yanawaendea sawa..
 
Wewe na mwenzio mnawakilisha wengi mno ninaowaona kwenye interviews. Hayo "mavyuo" ya hovyo yanatoa wanafunzi wengi tu kila mwaka, siyo wewe tu.
we mzee mbona una complicate maisha sana,,maisha simple sana haya unayafanya magumu..wazee kama nyie skuiz tunachapa bakora tu,na laana atupati.
 
Back
Top Bottom