2011 UDSM nilinusurika kukamatwa

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Huu mwaka sitausahau pale mlimani.

Washikaji zetu ,Christopher mbusule, Lusako ,Ndunguru na wengine wengi tu walipoteza chuo.

Mlimani city ilikuwa jumba la maficho . Tulikimbia tukajificha kwenye maduka. Wale jamaa walikuja na hasira kama za simba wakitutafuta.

Poleni sana washikaji wote mliopoteza chuo kipindi Hicho. Harakati zenu zilifanyika neema kwa wengine.

Mungu bado anatupigania . Siku zimepita na maisha yanaendelea.
 
Aiseee Ndunguru alikua mbishi kwelikweli alianza kuandamana peke yake akiwa peku,, daaah Tanzania kuna watu walikua na mioyo ya kipekee sana,, imagine alikua na mkopo na alikua mwaka wa tatu anamaliza lakini alishindwa kukaa kimya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza alipokosa mkopo. Halafu akaja funga kazi aliejiita alshabab,,
 
Ila kuna watu ni hatari nakumbuka alshabab kipindi cha mgomo tulikuwa pale utawala mwanadada akaanza kutiririsha maneno maprof walitoka kwny ofisi zao wakasimama kule juu gorofani wakimsikiliza walibaki wanatikisa tu vichwa vipaji vyao vingeendelezwa tungekuwa na wapembuzi na wanasiasa makini sn,
 
Saizi Revo sikwea sidhani kama ipo tena maana hawa waliopitia Jkt wamekuwa kama mlenda
 
Aiseee Ndunguru alikua mbishi kwelikweli alianza kuandamana peke yake akiwa peku,, daaah Tanzania kuna watu walikua na mioyo ya kipekee sana,, imagine alikua na mkopo na alikua mwaka wa tatu anamaliza lakini alishindwa kukaa kimya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza alipokosa mkopo. Halafu akaja funga kazi aliejiita alshabab,,
Aliyeandamana peke yake ni Ndunguru au Mwita?
 
Sisi tulikuwa na test kule yombo asubuhi tulivyogawiwa tu mitihani tukavamiwa na ilikuwa si mchezo kukiwa na mgomo nyie mkasaliti mnachalazwa hatari tulivyosikia tu wanakuja wanaimba kila mtu haijulikani alitokaje mlangoni si kwa mbio zile kulikuwa na malecturer wawili wakisimamia mtihani walitimua km vichaa test ikawa imavurugwa baada wa mgomo kuisha tulitungiwa test nyingine ilikuwa ngumu km mpingo tulikoma
 
Huyo huyo Ndunguru akafika revolution square pale, akaanza kutema hoja baada ya muda watu wakajaa, jamaa yuko peku peku anaongea balaa. Kilichokua kinasisimua zaidi ni hoja zilivyokua zinatolewa. Baada ya Ndunguru na wengine kukamatwa sasa ndio chuma Alshabab kilipoamka sasa,, akaanza peke yake ku mobilize watu na kuhubiri. The guy will make a very good politician sijui yuko wapi siku hizi.
Aliyeandamana peke yake ni Ndunguru au Mwita?
 
Mimi sijasema.
Ila UD nilijiunga 2010 na nilikutana na masekeseke sana.
Na masekeseke nilianza nayo secondary, kama unakumbuka 2008-2010 shule nyingi zilikuwa na fujo sana.
Kipindi hicho shule nyingi zilikuwa zinakabiliwa na baa la njaa, kama kumbukumbu ziko sawa kipindi hicho wazabuni waligoma kwa sababu serikali ilikuwa haijawalipa kwa muda mrefu, baadhi ya shule zilifikia hatua ya kufungwa kwa ukosefu wa chakula
 
Back
Top Bottom