2011 Tanzania haina miaka 50 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2011 Tanzania haina miaka 50

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyamahodzo, Apr 4, 2011.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwasasa watu wengi wanazungumia miaka 50 ya uhuru wa Nchi ya Tanzania.
  Swali ninalojiuliza, hivi ni lini Tanzania ilizaliwa hata kufikisha miaka 50?
  Au ndiyo mfululizo ule ule wa kudanganywa na kudanganyika kwa watanzania na kuiambiwa kuwa CCM imeliongoza Taifa hili kwa miaka 50 wakati ni miaka 34 tu?

  Zanzibar ilifanya mapinduzi yake Jan 1964, April mwaka huo ndipo Tanganyika iliungana na Zanzibar kupata Tanzania. Hivyo ki-ukweli Tanzania ilizaliwa 1964. Kwahiyo hadi leo hii Tanzania ina miaka 47 na sherehe yake inabidi ifanyike 26 April kila mwaka.

  Tanganyika yetu, wamekuzila huku wanakutamani.
  Wanawadanganya wana wako kuwa Tanzania ilipata uhuru1961 wakati ndiyo mwaka wako wa kuwa huru, wanajisifia kuwa Tanzania ndiyo nchi ya kwanza katika Afrika Mashariki kupata uhuru wakati wewe ndiyo wa-kwanza. Jina lako kwenye shughuli za kiserikali halitajwi, na kama likitajwa basi na kama kwa ajali kiasi cha kwamba hata mtajaji inabidi aangalie kuume na kushoto ili kuona kwamba hajawakosea waliopo katika meza ya hapo mahali. Jina lako Tanganyika limebaki kwenye vitabu vya historia na kuwa jina la makampuni kadhaa hapa udongoni pako. Inauma!!

  Tanganyika tunahitaji heshima yako irudi. Na udanganyifu huu wa kusema Tanzania inamiaka 50 ktk mwaka 2011 ukome. Wazanzibar wamekazana kutafuta heshima ya mama yao Zanzibar, sisi tunapumbazwa na hili kaniki linaloitwa muungano hata hatuoni ama hatutaki kumwona mama yetu Tanganyika. Inatosha.

  Wana wa Tanganyika, sasa ni wakati muafaka tunapoidai katiba mpya tudai na Tanganyika, itakayotupa utanganyika wetu ndani ya utanzania. Si jina la Tanganyika ila ni utaifa ama utamblisho wa yakuwa sisi tu wa-Tanganyika(nchi yenye uoto mzuri wa asili).

  Nawasilisha.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  @mnyamahodzo ulichoongea ni kweli tupu lazima kuwe na tafsiri halisi ya Kuweka bayana Tanganyika baada ya uhuru ilizikwa baada ya miaka mitatu kupata uhuru, sasa tutasemaje Tanzania ilipata uhuru miaka hamsini iliyopita wakati nchi hii haikuwepo miaka hamsini iliyopita ,sijui wajuzi wa mambo haya labda watujuze
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Penye red, is like a white elephant which was found in Mikumi National Park.
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Mwalimu wako alikuwa na kazi Sana kukufundisha .. Nani kakuambia watu wanafikiria kuwa Tanzania Inatimiza Miaka 50??? Hata mkulu wako kilaza kakushinda kwani alitamka vizuri katika hotuba yake ya mwezi january, kuwa Tanganyika ndio itatimiza miaka 50 ya Uhuru.... au unataka kuleta vurugu nchini
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0

  wewe ndiye kilaza namba moja hapa tanzania kwani uhai wa Tanganyika ni miaka mitatu tu .... na hadi leo hakuna nchi inayoitwa Tanganyika kiasi cha kusema tanganyika ndiyo inatimiza miaka 50 ...... fikiri ..... kwani mtoa mada anayo hoja
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,576
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Yani utawajua tu, hawa wezi kujificha wazee wa ZIDUMU FIKRA ZA MEWENYEKITI
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.

  Ile nchi iliyoungana na Tanganyika ilikuwa inaitwa kwa jina gani?

  Hebu jaza jina hapa...Tanganyika iliunganisha mambo 11 na ................. kuunda Muungano wa Tanganyika na ........................

  Leo ile nchi iliyounganisha mambo kumi na moja na Tanganyika ipo au haipo?
  Inaitwaje vile?

  Kama ile nchi nyengine ipo ni wazi kuwa Tanganyika ilibadilisha jina lake kinyemela tu. Rais wa serikali ya Tanganyika ndie alifanya "mazingaombwe haya"..Ni rais wetu lakini hapa aliturushia changa la macho.

  Kama huamini angalia hapa

  Map - Colonial Africa in the Twentieth Century

  halafu hapa
  Google Image Result for http://3.bp.blogspot.com/_oQr0xyi_dmg/TBFEC5mwaFI/AAAAAAAAABE/6D87Gxkxsdk/s1600/tanzania-map.gif

  Vipi? mbona unacheka?

  Wakuu, mnabishana kwa vitu vilivyo wazi !!!!...Je tanganyika ipo au haipo?

  mkuu umesoma giografia..Tanganyika ilikuwa inapatikana wapi katika longitude na latitude?
  Je hiyo sehemu iko wazi leo? hakuna pande la ardhi hapo?

  Sasa tudai tu,tutumie jina lake kama zamani na tudai serikali ya Tanganyika irudi.


  Muungano ujadiliwe upya na kusiwe na ubabaishaji.
  Nchi zinapoungana huwa hazifi, wala majina yake huwa hayapotei.
  Mwalimu tu ndiye aliweza kufanya miujiza hii.
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni kweli, Mwalimu wangu alifanya kazi kubwa sana kuhakikisha najua kusoma na kuandika, si mjinga, najua kuyatafuta, kuyapokea na kuyatumia maarifa, nakuwa na uwezo usiotegemezi wa kufikiri,kuchambua na kuamua mambo, n.k. Sasa, ndugu yangu unaona matokeo ya uvivu wa mwalimu (hakufanya kazi) wako <nafikiri hata wewe ulikuwa mvivu> yalivyokutengeneza wewe leo? Aibu!!


  Kama watu hawafikiri, unafikiri kwanini kwenye kalenda za taasisi za serikali ya JMT tar 9 Des inaandikwa kuwa siku ya Uhuru? Uhuru wa nchi gani kama si Tanzania?

  Hapo kwenye red, tujuze nchi ya Tanganyika iko wapi ktk dunia hii hata tusherehekee uhuru wake?

  Tanganyika iliishi miaka 3 tu ya uhuru wake, baada ya hapo ikafungiwa kusikojulikana tena kwa sheria, na kuhubiriwa na viongozi tuisahau. Sasa, utamsahauje mama yako?
   
 9. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Haya ni maswali ya msingi kujiuliza, thank you for Sharing!
   
 10. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mkuu.
  Lakini nini maana ya wazanzibari kuuliza Katiba ya Tanganyika ili wajadili muswada wa mabadiliko ya katiba ya JMT?
  Ni kwamba wao waijua Tanzania na hawaijui Tanganyika au wao wanaijua tanganyika lakini hawaijui Tanzania?
  A lot to ask but answers could lead us to somewhere.
   
Loading...