2011 ni mwaka wa Mfumuko wa Bei, maisha magumu na Ujambazi juu!

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
Wanasiasa wanakoipeleka hii Tanzania siyo,

Pazeni sauti, umeme bei ikipanda, bei ya mkate pia itakuwa juu,

Kataeni Ufisadi, asiye na Kipato lazima atakuwa Kibaka.

Licha ya Mvua kutonyesha,bado sisi viongozi wetu wanaendelea kuwa manyapara wa mafisadi.

Kila kitu, tunampa huyo mhindi hadi PPF zetu tumemwachia.

Napata hofu sana, vibaka watakuwa wengi mitaani,ujambazi utakuwa hatari sana.

Jameni jameni amkeni,

Nchi imekwenda
 
Mkome ulifikiri zile fulana na kapelo mlizopewa zilikuwa za bure?sasa ndio mnalipa
 
Ukitathmini kwa makini utaona mfumuko wa bei unaweza kufuka zaidi 30%
 
:msela::msela:Watanzania wenzangu, jana nilikwenda sokoni kupata mahitaji mbalimbali na mama watoto, nilichokikuta huko, nilishangaa sana, bei ya vyakula imepanda kwa kiasi kikubwa mno! Kwa mfano, sukari last month nilinunua sh. 1600 kwa kilo, jana nikakuta sh.2000, ngano kg 5, ilikuwa 5000, jana nimekuta ni sh. 6200, mafuta ya kula (alizeti) lita 5 ilikuwa sh. 13500, jana imepanda hadi sh. 18000. Hoja yangu hapa ni je, kwa maisha haya, serikali haioni kwamba imeshindwa kuongoza nchi? Je serikali ya CCM kwanini isiondolewe madarakani au kwa nini JK ashiondolewe madarakani kwa nguvu ya umma kama TUNISIA na EGYPT? Naomba kuwakilisha!!!!!!!!!!!!!!!!!:msela::msela:
 
KASI ya kupanda kwa gharama za maisha kumeaanza kuitikisa nchi, huku wananchi wakikumbuka awamu ya uongozi uliopita.

Pamoja na hali hiyo mbaya ya uchumi, wananchi wengi wamechukizwa na Serikali kuandamwa na kashfa nyingi za ufisadi, ukiwamo uamizi wa kuilipa kampuni ya Dowans mabilioni ya shilingi wakati nchi ikiwa katika hali mbaya kiuchumi.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa vitu vingi muhimu vimepanda bei mara mbili na kuathiri mfumo wa maisha ya watu hasa wa tabaka la chini, ambao ni zaidi ya nusu wa Watanzania wote.

Ingawa serikali inajitetea kuwa hali ni shwari, habari kutoka ndani ya Serikali zinaeleza kuwa inakabiliwa na upungufu wa fedha kiasi cha baadhi ya malipo kuyasitisha.

Habari zilizotufikia zinaeleza kuwa mzunguko wa fedha sokoni ambao unatokana na fedha za Bajeti ya Serikali unaonyesha kupungua kwa kasi na Serikali imelazimika kupunguza matumizi yake ya bajeti iliyopanga kutokana na kupungua kwa makusanyo ya kodi.

Wasomi, wanasiasa na watu mbalimbali nchini wameitahdahrisha Serikali kwamba isiporekebisha hali hiyo inaweza kusababisha mambo mengine.

Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Semboja Haji akizungumzia hali hiyo alisema kupanda kwa bei ya bidhaa nyingi muhimu kunatokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

Alisema nchi zinazozalisha mafuta hivi sasa zimepandisha bei ya bidhaa hiyo na wafanyabiashara wa hapa nchini wanatumia nafasi hiyo kupandisha bei ya mafuta hata kama walikuwa na akiba ya kutosha ya mafuta waliyonunua kwa bei ya kawaida.

Dk Semboja pia alisema matatizo ya mgao wa umeme yamechangia pia hali hiyo kwani baadhi ya viwanda vidogo vya uzalishaji vimepandisha bei ya bidhaa kutokana na tatizo hilo.

"Ni cycle (mzunguko) ya uzalishaji, hali hii hutokea, kinachotakiwa kwa serikali ni kuhakikisha kukusanya mapato yake kupitia kodi na vyanzo vingine vya mapato na kusimamia matumizi yake," alisema Dk Semboja.

Waziri Mkulo
Alipoulizwa kuhusu hali hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema hana cha kuongeza kwa kuwa hali ya uchumi ilishatolewa ufafanuliwa na Profesa Ndulu alipozungumza na waandishi wa habari.

"Sina cha kuongeza kwa aliyozungumza Gavana, wewe kaandike Waziri amesema anakubaliana na yaliyozungumzwa na Gavana," alisema Mkulo.

Gavana Ndulu
Hivi karibuni Gavana wa Benki Kuu, Prof Benno Ndulu alisema hakuna mfumoko wa bei unaoweza kuangusha uchumi wa nchi.

Alisema ni kweli kasi ya kukua kwa uchumi ni ndogo, lakini akasisitiza kuwa nchi inapiga hatua kimaendeleo.

Profesa Ndulu alisema tatizo lililopo ni watu kusahau walipotoka na kuona kama hakuna juhudi zinazofanyika, huku akitoa mifano ya kukua kwa pato la mtu mmoja mmoja kutoka Sh200 hadi 300 na kufikia Sh500 badi 600 na sasa ni Sh1,000.

Hata hivyo, Gavana Ndulu alikiri kuwa kiwango hicho hakitoshi na juhudi zaidi zinahitajiwa kufanyika.

Tundu Lissu
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu, alisema kukua kwa uchumi kunakotajwa na serikali ni kwa watu wachache na si Watanzania walio wengi.

Alisema kama hali ya uchumi ingekuwa nzuri kama inavyodaiwa na serikali, kusingekuwa na malalamiko ya makali ya maisha kutoka kwa wananchi.
"Hali hii italeta machafuko, wananchi wamechoshwa na wamechoka kuona wachache wakifaidi, angalia matatizo vyuo vikuu, angalia matokeo mabaya ya wanafunzi, fedha zimeliwa badala ya kupelekwa kuboresha shule," alisema Lissu.

Wananchi
Mkazi wa Dar es Salaam, Joseph Kaengera alisema kupanda kwa gharama za umeme kumechangia hali ngumu yabh na kwamba tangu bei ya umeme ipande Januari mwaka huu ameamua kutumia kibatari.

"Awali nilikuwa nikienda kununua Luku, nikitoa Sh5,000, pamoja na kukatwa gharama za kila mwezi za Tanesco, nilikuwa napewa uniti 19, lakini juzi nilitoa fedha hizo hizo nikapewa uniti saba tu," alilalamika Kaengera ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vyakula Temeke.

Wakazi wa Mkoa Kilimanjaro wakiwemo wanasiasa,wasomi na wafanyabiashara wamependekeza mabadiliko makubwa yatakayowezesha kupatikana viongozi wanaojali maisha ya Watanzania ikiwamo kudhibiti mfumuko wa bei.

Wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti jana mjini Moshi, wananchi hao walidai kuwa matumaini waliyokuwa nayo kwa Serikali yanazidi kutoweka kutokana na ugumu wa maisha kuzidi kuongezeka.

"Tunachohitaji sasa mabadiliko ya katiba yatakayotuwezesha kupata kiongozi bora na anayejali watu wake…hivi unaweza kurudi nyumbani umelewa halafu ukasema huna pesa?alihoji Mfanyabiashara Akwiline Kinabo.

Kinabo alisema maisha ya Watanzania yanazidi kuwa magumu kutokana na bei za bidhaa muhimu kupanda mara dufu katika kipindi cha miezi miwili iliyopita na hakuna kauli yoyote inayotolewa na serikali kuhusiana na hali hiyo.

Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mwanga ya Chama cha Mapinduzi(CCM), Rodgers Msangi alisema uchumi wa Tanzania unapitia kipindi kigumu kiasi kwamba Watanzania sasa wanamkumbuka Rais mstaafu, Benjamin Mkapa.

"Kwa kweli hali ni mbaya sana angalia petroli ilivyopanda awamu ya Rais Kikwete kutoka Sh800 kwa lita hadi sh1,900,"alisema Msangi.

Mbunge wa Viti maalumu, Grace Kiwelu (Chadema) aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa Watanzania wanaumia hivi sasa kwa kuwa viongozi wa Serikali hawana mipango thabiti na inaonekana uwezo wao wa kufikiri umefika mwisho.

"Tatizo hata viongozi wetu hawana huruma na Watanzania, ukichunguza utaona nguvu kubwa na mawazo yao yameelekezwa katika uchaguzi wa 2015, nchi inakwenda mrama ni kama jahazi linalozama,"alisema.

Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Karanga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT),Fred Njama alisema Tanzania haiwezi kusonga mbele hadi watakapopatikana viongozi wenye dhamira ya dhati ya kuwasaidia Wananchi.

"Nakuambia tutaendelea kuumia mpaka tutakapopata viongozi wenye dhamira ya dhati ya kuwaletea Watanzania maendeleo kwamba kila wanachokisema wanakitafsiri kwa vitendo sio maneno matamu tu,"alisema mchungaji huyo.

Mchungaji huyo alisema viongozi wa Serikali wanafahamu kuwa kilimo cha jembe la mkono na cha kutegemea mvua si cha kutegemewa hata kidogo, lakini hadi leo hakuna mapinduzi ya dhati ya kilimo kikiwamo cha umwagiliaji.

Bei ya bidhaa
Katika vituo vya petroli hasa katika jiji la Dar es Salaam, bei ya petroli imefikia Sh1,880 kwa lita na dizeli Sh1,870. Bei hizo zimepanda kutoka Sh1,694 kwa petroli na Sh1,720 dizeli, mwishoni mwa waka jana.

Bei ya soko la dunia kwa sasa pipa moja ni dola 100 kutoka dola 80.

Sukari ambayo ilikuwa ikiuzwa kwa Sh 1,200 kabla ya Desemba hivi sasa inauzwa kwa Sh 2,000 kwa kilo moja.

Benki Kuu ya Tanzania

Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania, makusanyo ya kodi yalifikia Sh2,093.8 bilioni chini ya makadirio ya Sh2,236.2 bilioni.

Wakati hayo yakiendelea, deni la nje limeongezeka na kufikia dola za Marekani 8,575 milioni sawa na Sh12 trilioni kwa Novemba mwaka jana kutoka Dola 8,377.5 milioni sawa na Sh11.73 trilioni Julai mwaka jana.

Pia deni la ndani limeongezeka kutoka Dola 2,064.4 milioni sawa na Sh2.89 trilio Julai mwaka jana hadi dola 2,288.3 milioni sawa na Sh3.2 trilioni Novemba mwaka jana.

Taasisi ya Uchumi (Economist Intelligence Unit) ya nchini Uingereza, imetabiri kwamba mfumuko wa bei Tanzania utakuwa asilimia 6.5 juu ya mipango ya serikali mwaka huu.

Taarifa ya hiyo, ambayo gazeti hili limeipata inaonyesha kupanda kwa mfumuko wa bei kunasababishwa na na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, kushuka kwa thamani ya sarafu shilingi na kupanda kwa bei ya vyakula.

Bei mahindi kwa mfano, imepanda kutoka Sh31,803 hadi kufikia Sh36,965 kwa gunia la kilo 100 na mchele umepanda kutoka Sh91,664 hadi Sh112,100 kwa gunia moja kuanzia Novemba mwaka jana hadi sasa.

Kuhusu kukua kwa uchumi, Profesa Ndulu alisema mgawo wa umeme kwa kiasi fulani kinaweza kuadhiri ukuaji wa uchumi katika robo ya mwisho, ambapo alisema unatarajia kufikia asilimia saba, kutoka asilimia 6.2 ya robo ya tatu.

Kuhusu akiba ya fedha za kigeni ambayo Tanzania inayo hadi hivi sasa, Prof Ndulu alisema kuwa nchi ina dola za Marekani 3.8 bilioni ambazo zinaweza kununua huduma kwa nchi nzima kwa miezi sita mfululizo.

Alisema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa kupita nchi yeyote ya Afrika Mashariki.

Source: Mwananchi Jumapili
 
Kwanza nawapa pole sana ndugu watanzania wenzangu.Ni wazi kuwa hatuna wa kumlilia kwa sasa!

Ugumu wa maisha haukuanza leo, miaka mitano iliyopita maisha yalikuwa karibu au sawa na haya tuliyo nayo leo. Tatizo letu watanzania ni kupenda vitu vya mteremko kwa ghrama ya jasho dogo au ikiwezekana bila ya jasho kabisa.

Kilio hakisaidii kitu, fanyeni kazi kwa bidii, zaidi kuweni wabunifu kwa hata kile kidogo mnachokipata ili kujiongezea kipato.Japo hamtaweza kununua magari nina imani hamtokufa njaa.

Kilio mtalia sana ila yapasa mjue kuwa hakuna mtu wa kuwasikiliza kamwe.

Yabidi tujifunge mikanda kisha tujipange upya!

Tulipo liliia wembe tukapewa, kwa vile umetukata basi akili zetu zifanye kazi na tutafakari mustakabari wetu na Taifa letu hapo kesho.

Pilau na khanga za kipindi kile haya ndo madhara yake!
 
Ugumu wa maisha, wananchi tutaamua

Thursday, 03 March 2011 12:17

NDUGU Mhariri, awali ya yote napenda nikushukuru kwa kupata nafasi hii kutoa dukuduku langu ambalo naamini kupitia gazeti lako sauti yangu itawafikia walengwa.Hakika maisha yamekuwa magumu sana ukilinganisha na miaka 2005 kurudi nyumba, Watanzania tumekuwa wazungumzaji sana wa kuilaumu Serikali kitu ambacho kamwe hakitatusaidia.

Watazania tufike mahala tufanye maamuzi yenye tija kwa maisha yetu kwani tukizidi kunung'unika bila kuchukua hatua hakuna kitakachobadilika.

Kitu cha msingi ni kuamia nini kifanyike ili kubadilisha hali iliyopo sasa, ukiangalia hali ya maisha kiukweli inatisha kwani chakula kimepanda bei mara dufu, huduma za umeme zimepanda na hasa hili la mgawo ndio limeleta athari kubwa katika maisha.

Binafsi sijui Rais wetu na Serikali yake wanafikiria nini kuhusu mambo haya, inawezekana viongozi wetu hawana mpango wa kutusaidia ila kutuumiza, la msingi ni Watanzania wenyewe kuwa na msimamo kwani tunawaona baadhi ya wabunge wanaongea sana bungeni lakini utekelezaji katika majimbo yao sifuri.

Imefika kipindi wananchi wanafanya mijadala ya wazi kwenye redio , televisheni na hata kwenye vyombo vya usafiri kama daladala, lengo likiwa ni kuonesha hali halisi wakifikiria labda viongozi wetu hawajui kwamba maisha ni magumu.

Tunahisi viongozi wanasikia lakini hatuoni mabadiliko yoyote, wananchi tumechoka na itafika siku tutachukua hatua, naitahadharisha Serikali iwe makini kwa sababu yaweza kuwa ni nzuri ama mbaya.
source:DAR LEO.
Mwanaharakati,
Esther Mashoto,
Dar es Salaam


USHAURI WANGU:
CHADEMA WATUSAIDIE WANAUME NA WANAWAKE WOTE WA TANZANIA.
Naunga mkono hoja 100%
 
Ugumu wa maisha, wananchi tutaamua Thursday, 03 March 2011 12:17 NDUGU Mhariri, awali ya yote napenda nikushukuru kwa kupata nafasi hii kutoa dukuduku langu ambalo naamini kupitia gazeti lako sauti yangu itawafikia walengwa.Hakika maisha yamekuwa magumu sana ukilinganisha na miaka 2005 kurudi nyumba, Watanzania tumekuwa wazungumzaji sana wa kuilaumu Serikali kitu ambacho kamwe hakitatusaidia.

Watazania tufike mahala tufanye maamuzi yenye tija kwa maisha yetu kwani tukizidi kunung'unika bila kuchukua hatua hakuna kitakachobadilika.

Kitu cha msingi ni kuamia nini kifanyike ili kubadilisha hali iliyopo sasa, ukiangalia hali ya maisha kiukweli inatisha kwani chakula kimepanda bei mara dufu, huduma za umeme zimepanda na hasa hili la mgawo ndio limeleta athari kubwa katika maisha.

Binafsi sijui Rais wetu na Serikali yake wanafikiria nini kuhusu mambo haya, inawezekana viongozi wetu hawana mpango wa kutusaidia ila kutuumiza, la msingi ni Watanzania wenyewe kuwa na msimamo kwani tunawaona baadhi ya wabunge wanaongea sana bungeni lakini utekelezaji katika majimbo yao sifuri.

Imefika kipindi wananchi wanafanya mijadala ya wazi kwenye redio , televisheni na hata kwenye vyombo vya usafiri kama daladala, lengo likiwa ni kuonesha hali halisi wakifikiria labda viongozi wetu hawajui kwamba maisha ni magumu.

Tunahisi viongozi wanasikia lakini hatuoni mabadiliko yoyote, wananchi tumechoka na itafika siku tutachukua hatua, naitahadharisha Serikali iwe makini kwa sababu yaweza kuwa ni nzuri ama mbaya.

Mwanaharakati,
Esther Mashoto,
Dar es Salaam


USHAURI WANGU:
CHADEMA WATUSAIDIE WANAUME NA WANAWAKE WOTE WA TANZANIA.
Naunga mkono hoja 100%

Wakulaumiwa ni uvivu wetu wananchi, kwani tungefanya kazi kwa bidii tungekuwa na chakula cha kutosha ktk magala yetu.
 
Wanawake wa Tanzania wanatuangusha kwa kuwapigia kura hawa mafisadi na ndio wa kwanza kwa kulalamika,sasa wajifunze kutokana na shida tunazopata wasibaki kupayuka hovyo kwenye Redio UHURU kuwa Dr Slaa anahatarisha amani ya nchi.
 
sio kweli huyu mwananchi anahitaji mbolea na zana za kilimo bado atahitaji mvua maana sasa hv maeneo mengi ni makame bado kuna usafiri kusafirisha mazao kwenda sokoni gharama yake unaijua!!bado asomeshe watoto shule wanahitaji chakula na ada!hapa mimi naona kikubwa ni kwamba hawa tuliowapa mamlaka ya kutusimamia wanashindwa na badala yake wanajiangalia wao wenyewe hainiingii akilini wabunge wanakopeshana milioni 90 kila mmoja kwaajili ya magari na ukizingatia wabunge wengine wapo bungeni miaka nenda rudi so kila baada ya miaka 5 anapewa pesa za gari jipya hata kama analo lile la zamani hamuoni kama ni uchezeaji wa pesa??mie nawalaumu sana viongozi wanashindwa kusimamia maslai ya wananchi wanaangalia matumbo yao!na robo tatu ya bunge ni CCM na ndio wa kulaumiwa sababu wao ndio wanaopigia kula hayo maamuzi!
Wakulaumiwa ni uvivu wetu wananchi, kwani tungefanya kazi kwa bidii tungekuwa na chakula cha kutosha ktk magala yetu.
 
Ugumu wa maisha Tanzania wa kulaumiwa ni sisi waTz wenyewe! Viongozi karibu wote wa Afrika wapo kwa maslahi yao, familia zao na rafiki zao tu, na sio kwa maslahi ya wananchi.
If you can not fight them, then join them!
 
Ni mchanganyiko wa vitu vingi sana. Uvivu wetu, ukosefu wa usimamizi madhubuti wa mali zetu, kukosa msukumo wa kujali elimu kwa watoto wetu na kubwa kuliko yote ni UFISADI!
 
Back
Top Bottom