2011, mwaka wa kisiasa: Dk. Slaa azidi kung’ara kisiasa;Lipumba, Maalim waporomoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2011, mwaka wa kisiasa: Dk. Slaa azidi kung’ara kisiasa;Lipumba, Maalim waporomoka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 29, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]
  Mwandishi Wetu - Raia Mwema
  [​IMG]


  Dr Wilbroad Slaa
  Dk. Slaa azidi kung’ara kisiasa
  Lipumba, Maalim waporomoka
  Nape abeba zigo la kuitetea CCM


  KWA takriban miezi yote 12 ya mwaka unaokwisha mwishoni mwa wiki hii wa 2011, umekuwa ukitawaliwa na mivutano ya hoja ambazo msingi wake ni siasa, tathmini ya Raia Mwema, inathibitisha.
  Dalili za mwaka 2011 kuanza safari yake kwa kutawaliwa na siasa ilianza kujitokeza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
  Ni katika uchaguzi huo ambao Jakaya Kikwete, mgombea kutoka CCM alitangazwa mshindi wa kiti cha urais, akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa na Mgombea wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
  Hapakuwa na hali ya pande zote kukubaliana na matokeo hayo ambayo hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hakuna fursa ya kuhoji mahakamani.
  Wabunge wa CHADEMA walionyesha dhahiri dalili za kuendelea kwa mvutano wa kisiasa mwaka 2011, baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge, ambako Rais Jakaya Kikwete siku chache baada ya kuapishwa, alikwenda kuzindua Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hotuba maalumu.
  Lakini dalili za mwaka 2011 kutawaliwa na mivutano ya hoja ambazo msingi wake ni siasa, hazikuwekwa bayana na CHADEMA pekee, bali hata Rais Jakaya Kikwete binafsi.
  Kikwete, katika hotuba yake ya salamu za mwaka mpya wa 2011, alizotoa kabla ya kumalizika kwa mwaka 2010, aliweka bayana nia ya Serikali kuanzisha mchakato wa Katiba mpya, akieleza kuwa, inatarajiwa kukamilika Aprili, mwaka 2014, wakati Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utakapotimiza miaka 50.
  Kwa hiyo, matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na ahadi ya Rais Kikwete kuanzisha mchakato wa Katiba mpya, zilikuwa ishara za kujitosheleza kwamba mwaka huu unaokwisha wa 2011 utatawaliwa na mivutano ya hoja za kisiasa.
  Ndiyo ilivyokuwa mara baada ya safari ya mwaka 2011 kuanza, masuala ya kupinga baadhi ya uamuzi wa Serikali kwa njia ya maandamano yalishikiwa ‘bango’ na CHADEMA, huku wanasiasa wengine na baadhi ya viongozi serikalini wakionyesha kutofurahia hali hiyo.
  Maandamano ya Arusha yaliyosababisha polisi kutumia nguvu kubwa na kusababisha vifo, yalizidisha mivutano ya kisiasa zaidi nchini, huku Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, akizidi kung’ara kwa umaarufu wa kisiasa katika mwaka 2011, pengine kuliko wanasiasa wengine kutoka CHADEMA.
  Dk. Slaa ameokana kiongozi wa kitaifa, ambaye kwa baadhi ya watu wanaamini kuanguka kwake kisiasa kunaweza kuwa ni ishara ya kupoteza umaarufu wa CHADEMA.
  Viongozi wengine ndani ya CHADEMA katika mwaka wa 2011 wamejitambulisha kwa namna tofauti kutokana na matendo yao. Mbunge Tundu Lissu, amejitambulisha kama mpigania haki mwenye msimamo mkali lakini aliyemakini katika kuelewa masuala ya kitaifa na kimataifa, hususan sheria, upeo ambao unaonekana kuwa tofauti na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye anaelekea kupenda kutambulika mbele ya jamii ni mpigania haki lakini, akiwa na ukomo wa uelewa katika baadhi ya masuala ya kijamii.
  Freeman Mbowe ameendelea kufanya siasa zake kwa njia ya umakini zaidi akikwepa kufanya makosa yanayoweza kuwapa nafasi wanasiasa wengine ndani ya CHADEMA kujenga hoja za kumuondoa kwenye nafasi ya uenyekiti.
  Kabwe Zitto, anaonekana kukomaa zaidi katika michezo ya kisiasa, taratibu akiondoka katika siasa za harakati bila maarifa ya kutosha na kwa baadhi ya wana-CHADEMA, anatajwa kuweza kumudu kukiongoza chama hicho kama Mwenyekiti.
  Ndani ya CUF, Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba, anatajwa kupoteza umaarufu wake na ushawishi si tu ndani ya CUF bali hata nje ya chama hicho, huku visiwani Zanzibar, CUF pia ikitajwa kupoteza mvuto wake wa kisiasa wa awali, kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
  Maalim Seif naye anaanza kupoteza mvuto huku wanasiasa wengine wakongwe kama yeye, akiwamo Hamad Rashid Mohamed, wakionekana ni chaguo sahihi la kurithi mikoba yake ya Katibu Mkuu, ingawa Hamad Rashid naye anaandamwa katika CUF na wanaomuunga mkono Maalim Seif.
  Katika CCM, hali ya sintofahamu imeendelea. Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete akionekana kucheza siasa za kukinyoosha chama chake katika hali ya kuogopa vivuli vya baadhi ya wanasiasa.
  Kikwete anatajwa kuwatanguliza zaidi wanasiasa, akiwamo mwanasiasa anayezidi kupata umaarufu nchini na ndani ya CCM, Nape Nnauye, ingawa naye amekuwa na maadui ndani ya CCM.
  Mwaka huu wa 2011 unakwisha huku CCM ikiwa katika kitendawili cha namna ya kihitimisha mchakato wa kujivua gamba, ambao ulitangazwa rasmi Februari 2011. Sekretariati ya CCM, baadhi ya wajumbe wake wanaonekana kuishiwa mbinu za kufanya siasa zenye ufanisi zaidi kwa chama hicho.
  Nje ya vyama vya siasa, mjadala wa Katiba mpya umewaunganisha Watanzania wa makundi karibu yote, bila kusahau mjadala wa posho mpya kwa wabunge kutoka Sh 70,000 hadi 200,000 ambao umepingwa na Watanzania wengi, huku Rais Jakaya Kikwete akigoma kuidhinisha ongezeko hilo na kumuweka katika hali mbaya kiuongozi, Spika wa Bunge, Anne Makinda.
  Kwa vyovyote vile mwaka ujao wa 2012, utaendeleza baadhi ya viporo vya kisiasa vya mwaka 2011, ambavyo ni pamoja na Katiba mpya, lakini suala la msukosuko wa uchumi linatarajiwa kuchukua nafasi yake katika mwaka 2012, huku wimbi la kupinga vitisho vya kuruhusu ushoga kwa nchi masikini ili kupata misaada ya wafadhili likitarajiwa kuendelea.
   
Loading...