kasyabone tall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2009
- 254
- 59
Tumekua tukiambiwa na kutadhaarishwa kila siku juu ya kuchanganya dini na siasa. Lakini mwaka huu 2010 ambao ni mwaka wa uchaguzi kwa nchi yetu inaonekana wazi maswala ya dini kutawala uchaguzi kiasi cha kutisha. Tunaweza kuona kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamechoshwa na wasanii kuendelea kutawala kwa kutumia njia za kisani, huku wengine wakidhani wanapigwa vita wao. Hii imeleta patashika nguo kuchanika kwa wananchi hasa mpaka pale ujumbe wa simu unapotumika kueneza kuwa viongozi wa dini fulani wanataka muumini wao aendelee kutawala. Wengine wakija na hoja dhaifu kuwa kuna mgombea kawekwa na wakatoloki. Pia kuna ushaidi wa wazi kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kumekuwa na upendeleo wa wazi kwa baadhi ya watu wa dini fulani hasa katika uteuzi wa viongozi mbalimbali. Hapa mimi ninashindwa kupata jibu kama matokeo ya uchaguzi ya mwaka huu yataonjesha uwiano wa waumini wa dini hizi mbili au bado yataonyesha umoja na mshikamano wa taifa letu.
Hapa wengi wamekuwa waoga kusema ukweli juu ya mambo yanayoendelea kuhusu udini lakini wamekuwa wepesi wa kujidai kukemea udini ambao wao ndio wafadhili wakubwa wa udini katika taifa lisilo hata na misingi ya udini. Wamekua wakitumia dini kama mtaji kwa mazoea na pale dini ikiwa mwiba kwao wanakimbilia kukemea udini. Tukijiuliza mbona hawakusema lolote pale viongozi wa kidini hao hao waliposema Bosi ni chaguo Mungu.
Hapa lazima tukubali kuwa lazima wavune walichopanda, ukipanda uaribifu utavuna uaribifu. Ni vigumu kwa mwaka huu kudhibiti watu wasichague mtu kwa hisia za kidini wakati wametawaliwa na hisia za kidini. Kuna watu wa dini fulani wanaona wanatengwa ndani ya nchi yao na wengine wanahisi wanapendelewa.
Ni lazima tukubali pia kuwa misingi ya taifa letu imeyumba na kuyumbishwa na viongozi tunaowategea kulinda misingi hio.
Pia kuna suala la ufamilia ambao pia unaendelezwa kwa kasi bila kutathimini madhara yake kwa jamii ya watanzania, pale baba, mama na watoto wanapopiga kampeni ya kuingia ikulu. Hapa pia pana swali muhimu la kujiuliza kuwa sisi tunatawaliwa na familia na si mtu mmoja kama ilivyokuwa kwa Nyerere. Urais kufanywa kuwa jambo la kifamilia na watu kukaa kimya hii inatisha.
Kugusia tu kidogo, uchaguzi wa mwaka huu watanzania wanatarajia mabadiliko, kwani kila dalili zinaonesha kuwa kunamabadiliko yatatokea. Ukiangalia kama ilivyo kuwa kwa kikwete 2005 dalili zilionesha atashinda KWA KISHINDO NDIVYO ILIVYOTOKEA. Mwaka huu ushahidi upo kama kura za maoni zioneshavyo Dr. Slaa lazima ashinde. Sasa kama kuna watu watatarajia kubadilisha matokeo si ajabu tukashuhudia kenya ya Tanzania.
Natamini kufika Octoba 31, 2010. Nione tanzania mpya inayotarajiwa na watu wengi.