Brooklyn
JF-Expert Member
- Mar 17, 2009
- 1,459
- 284
Zikiwa zimebaki takribani wiki mbili kufikia tarehe 04 December, 2009 ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) litakuwa likichezesha draw ya kupanga makundi ya timu zitakazo shiriki mashindano ya Kombe la Dunia huko Afrika ya Kusini hapo June mwaka kesho.
Draw hiyo itakayofanyika katika Jiji la Cape Town, inatarajiwa kuvuta hisia za wapenzi wengi wa mpira wa miguu dunia nzima. Timu 32 ambazo zimefudhu kupata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia ni;
Kutoka Africa: Algeria, Cameroon, Ivory Cost, South Africa, Ghana na Nigeria
Kutoka Ulaya: Denmark, France, Greece, Netherlands, Slovenia, Serbia, Switzerland, England, Italy, German, Portugal, Slovakia na Spain
Kutoka Asia: Austraria, Korea DPR, Japan na Korea Republic (KOR)
North, Central America & Caribbean: Honduras, USA, na Mexico
Oceania: New Zealand
South America: Brazil, Argentina, Chille, Uruguay na Paraguay.
1. Hebu wadau wa soka tubashiri nani atapangwa na nani katika makundi.
2. Nini nafasi ya Afrika katika kuhakikisha kombe linabaki Afrika kwa mara ya kwanza,
3. Nchi gani yenye nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa dunia kwa mtizamo wako??