2008 Kwa Mujibu wa Shetani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2008 Kwa Mujibu wa Shetani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shetani, Jan 5, 2008.

 1. S

  Shetani Member

  #1
  Jan 5, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1.mgogoro mkubwa CCM,vigogo kadhaa kufukuzwa unachama.
  2.Kabwe Zito kupauka kisiasa,madeni na fadhila za matajiri wa Ccm kumzonga, kuoa bint Mgumia his 'baby's mama'
  3.mbowe kuachia ngazi degree moja, kukamatwa kwa biashara ya unga na kuiba documenti kuhusiana na deni lake la NSSF
  4.balali kufukuzwa kazi, kufariki dunia
  5.mrema kufariki dunia,msiba wa kitaifa
  7.wezi kuendelea kupeta serikalini
  8.JF kuendelea kutokuwa na jipya,kuchokwa,kuwa taasisi rasmi ya Chadema ikiongozwa na Kitila Mtumbo,
  9.shamba la mfano la Chadema nje ya Dar kunawiri, waandishi wa habari kupelekwa kuliona,Mnyika kupandishwa cheo Chadema
  10.biashara ya magazeti kuwa ngumu zaidi,magazeti kadhaa maarufu kufungwa
  11.makanisa ya utapeli kuongezeka Dar,Mwanakijiji kuchanganyikiwa na kuanzisha lake
  12.chama kipya cha mrengo wa kushoto kuanzishwa Bongo kujumuisha Isa shivji, Makwaia Kuhenga,Joseph Butiku,Madaraka Nyerere,Jenerali Ulimwengu,Zito Kabwe
  13.slaa kubainika kumweka kimada Sekretari wa Makao Makuu ya Chadema
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  I think ur right for over 90%....
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Jan 5, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  TUNASHUKURU KWA MAONI HAYA , KAMA UNAONA HAUNA JIPYA HATA HILI ULILOTOA WEWE JIPYA NA NI MCHANGO KWAHIYO HATUKOSI KUWA NA JIPYA KWA SABABU HILI NI JUKWAA HURU KULA MTU ANA UHURU WA KUSEMA CHOCHOTE ANACHOTAKA ILA ALITUKANE , ASIDHALILISHE WALA KUTUMIA LUGHA YOYOTE CHAFU AMBAYO INAWEZA KULETA MAUZI AU KUHARIBIA JAMII HUSIKA MOOD YA KUENDELEA NA KILA KILICHOKUWA JUKWAANI .


  SHETANI USIKATE TAMAA KWA KUWA UNAONA KUNA POST KIDOGO LABDA UNASHINDWA KUKOPY NA KWENDA KUPEST KATIKA MAILING LIST YAKO AU KWA JAMAA ZAKO WENGINE .

  WAKATI MWINGINE JITAIDI KUANDIKA YAKO AU TTUNGA YAKO LETA JUKWAANI AU WEKA KATIKA MAILING LIST YAKO

  HALAFU PIA SIO LAZIMA KILA KITU UPATE JAMBO FORUM UNAJUA HII NI AFRIKA MASHARIKI KUNA UGANDA , KENYA , BURUNDI , RWANDA WOTE HAWA WANAFORUM ZAO NA VIJIWE VYAO UNAWEZA KUTOA HUKU UNALETA HUKU MAISHA YANAENDA

  USITEGEMEE TU CCM NA CHADEMA -- TANZANIA SIO YA CCM WALA CHADEMA PEKEE KUNA MENGI YA KUONGELEA NA KUJADILI

  MWISHO WA SIKU WEWE JIULIZE FANI YAKO JE WEWE NI MWALIMU ? KUNA JUKWAA LA ELIMU , WEWE NI MCHUMI KUNA JUKWAA LA UCHUMI , WEWE NI MWANDISHI KUNA JUKWA LA HOJA NZITO JE WEWE NI MWANAMTANDAO KAMA MIMI KUNA FUNGU LAKO LA SAYANSI NA TEKILOLOIA

  SIO LAZIMA SIASA
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  shetani bwana umenifanya nikate mbavu kinoma.

  wewe kweli shetani unaona tusioyaona
   
 5. green29

  green29 JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Then ndoto ikaendeleaje shetani?
   
 6. S

  Shetani Member

  #6
  Jan 5, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndoto iliisha kwasababu uliiba mchele ndani kwenu ukaenda kujipikilisha kwenye vikopo vya TanBond.

  We shy hayo maandishi ya herufi kubwa ni kinyume na ustaarabu wa kwenye intaneti,badilika.
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Unajua watu wanachukulia masihara haya yaliyotajwa na Shetani, lakini kuna ukweli mkubwa katika utabiri wake!
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hahahaha,

  Nilipoona Mchungaji kachangia mada ya shetani nilikumbwa na shauku ya kutaka kujua anachangia nini.

  Nikafikiri atamkemea kwa jina la Yesu.

  Kufungua mada, kumbe anamuunga mkono!

  Vituko vya JF, Mchungaji na Shetani waungana!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jan 5, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unaafiki kuwa rafiki yako Mwanakijiji mwaka huu atachanganyikiwa akili na kurudi bongo kuanzisha kanisa lake?
   
 10. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  tehe tehe the, sasa hapo sijui mwenye nguvu ni nani hadi sasa?
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hahahahaha mwe,
  natabiri kuwa mwaka 2008 wachungaji wengi watadhihirika wazi kuwa wako idara moja na shetani.
  we shetani ushindwe kwa majina yoote ya Mungu na hakika uende kuzimu na mautabiri yako ya nuksi yashindwe.
  hatutaki afe mtu mwaka huu na pia hatutaki migogoro ya kisiasa nchini kwetu na hakika ukemewe wewe
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Pundit,

  Shetani anaweza kuwa anakera sana na hata kusumbua umma. Lakini kupuuzia ayasemayo (yawe bora au pumba) ni upungufu wa hekima!
   
 13. B

  Binti Maria Senior Member

  #13
  Jan 5, 2008
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shetani anaudhi na kuchekesha at the same time, lakini hata mimi hilo la chama cha mrengo wa kushoto nimelisikia japokuwa wajumbe wake sijawasikia!
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  duh jamani nimecheka mpaka basi.

  shetani na wenziwe wananichekesha kinoma.


  mkjj pole sana kama upo njoo uone maono ya shetani
   
 15. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nyani Ngabu,

  Hata katika urafiki wangu na Mwanakijiji, kuna mambo tunatofautiana na hatukubaliani. kanisa atakaloanzisha ni kanisa la Kujenga Taifa!

  Kwani hilo kanisa ni lazima liwe kama la Kakobe, Lwakatare au Mwakasege? Kama ni kuchanganyikiwa, mbona ni wengi tuliochanganyikiwa? hakuna binaadamu aliye timilifu (perfect)! kila mmoja wetu ana mapungufu yake na mazuri yake. Kutofautiana mtazamo, maoni au hoja au namna ya kufikiri na utendaji ni haki yetu.
   
 16. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Binti Maria,

  Ndio maana nimesema kuna mengine aliyoyasema Shetani ni ya msingi na si kupuuzia. Inawezekana kabisa alitaka kututajia nyeti tano lakini kazifanya kumi ukiongeza upupu ndo maana watu wamchukulia kimasihara!

  Hili la chama cha mlengo wa kushoto, hata mimi nimelihisi na nitakuwa wa kwanza humu ndani kukimbilia uanachama na kumuacha Mnyika solemba na Chadema yake :)
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jan 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hilo la kuanzisha Kanisa nadhani halikko mbali sana na ukweli hasa ukizingatia kuwa uchungaji nilisomea Makumira... tatizo ni Kitabu gani tutatumia, na ujumbe wake utakuwa ni nini...

  Lazima liwe Kanisa tofauti sana na makanisa mengine.. na hivyo waumini kama Shetani wanaruhusiwa as long as wanaamini katika jina la kanisa hilo... sasa sijui kama mambo ya kukemea mapepo yataruhusiwa.. ?

  Ila utabiri wa Shetani unaweza kuwa kweli kwenye mambo mengi.. maana huwezi kujua maana kwenye Ayubu tunaambiwa kuwa SHetani alijipitisha pitisha mbele za Mungu na kumsikia Mungu akimsifia Ayubu.. so you never know what our Shetwan might have heard...
   
 18. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Huyo anayejiita Shetani,anaweza kuwa SIO Shetani kama jina lake lilivyo!!,Pitieni Maandishi yake kwenye mistari,kuna message Nzito kaileta hapo!!!.Itunzeni Thread hii.
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
   
 20. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mnajua hata Malcom X aliitwa "Shetani" jela kabla ya kuwa maarufu?


  Shetani wa leo anaweza kuwa mwanamapinduzi wa kesho.

  OK, Shetani usivimbe kichwa sana sasa.
   
Loading...