2005-vigezo vilivyotumiwa na chadema kuchagua wabunge wa viti maalum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2005-vigezo vilivyotumiwa na chadema kuchagua wabunge wa viti maalum

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwikimbi, Sep 2, 2008.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mnamo 2005, chadema walitumia vigezo vifuatavyo kuchagua wabunge wake wa viti maalum, nilipewa hint hizi na mmoja wa wakurugenzi wa chadema, hii inaondoa dhana kuwa hakukuwepo na ukabila

  1.0, wakati chadema inakaribia uchaguzi mkuu na ikiwa imeamua kuweka mgombea wa urais, ilikuwa haina pesa hivyo ikaamua ku-raise funds kwa njia mbalimbali mojawapo ikiwa ni pamoja na kukopa, mh. ndesamburo alikubali kuikopesha chadema zaidi ya 100m, aliweka sharti mojawapo kuwa ni lazima nafasi za ubunge wa viti maalum kiti kimoja kiende kwenye familia yake, bahati ikamdondokea mheshimiwa lucy owenye

  2.0, mheshimiwa grace kiwelu, alikuwa mbunge wa viti maalum kwenye bunge lililopita, inasemekana alifanya kazi sana ya kukitangaza chama, ikafika mahali ikamgharimu hata maisha yake ya ndoa, kwa kupewa talaka na mumewe,mkutano wa chadema likaagiza kuwa kwa sadaka aliyoitoa katika chadema, endapo zitatokea nafasi hata tatu za ubunge apewe moja, na kwa kuwa maagizo ya mkutano mkuu ndo ya juu kabisa na hutengulina mkutano mkuu nasi haikuwezekana kumwacha mama grace kiwelu

  3. mama ana komu, yeye anaitwa maulida , ni mzanzibar aliyeolewa uchagani miaka mingi ilyopita, yeye ndo mwanzilishi wa chadema mkoani kilimanjaro, huyu mama alijitolea kwa hali na mali, kuna wakati alikuwa naishi moshi peke yake akipambana na mrema wakati huo mrema akiwa ccm na jogoo wa kilimanjaro, licha ya yote yeye ndiye alikuwa mgombe mwenza wa freema mbowe baada ya aliyekuwa mgombea mweza kufariki RIP. ingekuwa vigumu mno kumwacha kwa kuwa tu alikuwa ameolewa uchagani na kusahau michango yote aliyotoa akiwa chadema.

  mheshimiwa halima mdee ni mwanasheria liyebobea, yeye ni mpare na wala siyo mchaga yeye alipambana na aakaonekana the best

  pamoja na yote, wote hapo juu walishindanishwa kwa haki, na wakshinda kwa vigezo vilivyokubalika na wanachadema wote.

  nawakilisha
  mwikimbi-raia wa tanganyika asiye na itikadi yeyte anyafungwa na utaifa wake
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Good source ya haya ni wapi? au na mwenzetu ni kiongozi mwandamizi nini?
   
 3. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu mwikimbi,
  Kama haya sio mawazo yako binafsi au mawazo binafsi ya huyo mkurugenzi aliyekupa hint basi hao Chadema wa tatizo kubwa zaidi ya ukabila (my opinion). Maana haya malezo ya kwanini kila mbunge kupewa huo ubunge yanapingana na hili hitimisho lake.

  Maana kama hilo hitimisho ni kweli basi haya maelezo mengine hayana haja ni kwamba walishinda kwa vigezo vilivyowekwa na chadema, otherwise kunakuwa na mchanganyo wa mambo. Kwa mfano

  Hapa tiyari ilijulikana kiti kimoja kitaenda kwenye huo ukoo, kwahiyo wale wagombea wote ambao hawakuwa wanatoka kwenye huo ukoo tiyari walikosa nafasi moja kati ya zilizokuwepo. Kama huo ukoo ukimpitisha mtu mmoja ndo aje kugombea hiyo nafasi (sijui walikuwa wangapi kutoka ukoo huo wanagombea)si basi lazima atapata ubunge hata kama hana sifa za kuwakilisha maslah ya chama pamoja na taifa?

  Na je kama mtu anapewa uwezo wa kuchagua nani awe mbunge kwa hela anazochangia akija R.A leo na billion 3 sharti awe mgombea wa kiti cha urais au ubunge kwa tiketi yao watakataa?

  Hata kabla ya nafasi kujulikana zipo ngapi kiti kingine alikuwa ameshapewa mtu kabla ya huo uchaguzi (ushindanishwaji) na sababu ulizotoa hapo juu ni kwamba alitangaza sana chama, je iliangaliwa pia na mchango wake katika bunge lililopita au ni maslah ya chama kwanza then nchi baadae? (just being objective no criticism)

  Unapojaribu kum isolate mtu mmoja tu kwenye ukabila na kuwaacha wengine basi implication inayotokea ni kwamba hao wengine ni kweli walipewa kwa kuwa na links za ukabila......

  Information kama hizi ndo huwa zinatufanya ambao hatuna chama kuwa sceptical na wapinzani maana ikiletwa hapa kama imetoka kwa mkurugenzi sisi walalahoi tunaamini ndo msimamo wa chama huo. Kama huo ndio utetezi wao wa hoja si watakuwa hivi hivi wakireplace fisadiz? Lakini kama hizi ni personal opinion za mtu hapo shega tu maana kila mtu anaruhusiwa kuwa na mawazo yake katika isues lakini instituion inayotaka dhamana ya wananchi kuwaongoza inabidi wawe serious zaidi katika kuamua mambo.
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Sawa Mheshimiwa, tueleze vigezo vilivyotumika kuwachagua Suzan Lyimo na Lucy Owenya.
   
 5. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna ukweli mwingi katika uliyoyaandika. Zitto na Mnyika si waliwahi kuandika kwa hapa vigezo hivyo. Kuna anayekumbuka walichokisema?

  Muhonga na Halima mara baada ya kumaliza masomo yao ya chuo kikuu walijitolea makao makuu ya CHADEMA. Mhonga akiwa Afisa Maendeleo wa CHADEMA na Halima akiwa Afisa wa sheria. Suzan Lyimo yeye aliteliwa kuwakilisha Vyuo Vikuu. Aliratibu sera na utafiti kampeni za urais 2005 chini ya Profesa Baregu na Kitila Mkumbo.

  Esther Matiku yeye alijitokeza mwishoni kabisa, hivyo nasikia alikuwepo kwenye orodha chini yao pamoja na Chiku Abwao. Hivyo kama CHADEMA ingepata viti maalum vingi kama CCM hawa wote wangekuwemo.

  Hata mimi niliomba kutoka Zanzibar, jimbo la Jang'ombe. Na mimi ndiye mwanamke niliyepata kura nyingi kuliko wote wa CHADEMA Zanzibar. Mama Maulidah alinizidi tu kwa kuwa yeye alikuwa Mgombea Mwenza na aliwahi kuwa Afisa Mwandamizi wa Wanawake wa CHADEMA kwa miaka mingi.

  Asha
   
 6. K

  Koba JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Hii habari imekaa kimajungu majungu sana,sijui kama kuna ukweli wowote? lakini kwa bongo najua inawezekana kuna ukweli!
   
 7. v

  vstdar Member

  #7
  Sep 3, 2008
  Joined: Apr 8, 2008
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka sababu zako nyepesi sana..cant hold water...vp kuhusu Mhonga Ruhanywa??..vigezo gani vilitumika kwake...mtu kama ana mapenzi na chama chake unapochangia/kukopesha chama huwezi ukaanza kutoa masharti ya ndugu yako lazima apendelewe hata kama hana uwezo, haya ndo mambo anayofanya RA halafu tunashangaa si nae alikichangia chama kwenye uchaguzi...kaka nadhani cku nyingine kabla hujaja kwenye jamvi jiridhise kwanza.....
   
 8. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mbona mi nimesikia Lucy Owenya ndiye aliyetoa milioni 100 toka akaunti yake ya urithi iliyoko Marekani?

  Ukweli ni upi? Alitoa ndesa au Lucy?

  Asha
   
 9. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ndo maana niliandika kuwa nimewasilisha, kwa majadiliano, kwa kuwa tunaye jamvini hapa zito, mnyika, slaa na wengine watueleweshe zaidi

  kuhusu uanachama wangu, mimi ni mwanachama namba moja wa nchi ijulikanayo kama Tanganyika, ambayo Mungu alitupa mipaka yake ikiwa ni maziwa ya tanganyika, mto ruvuma, bahari ya hindi, dola la buganga na dola la kenya, kwa kumsahihisha mwenyezi Mungu wazee mzee Mmoja aitwaye julius nyerere akaliuza dola letu kwenye nchi moja ambayo iko bara la asia inayoitwa zanzibar
   
 10. FTP

  FTP JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2013
  Joined: Jun 6, 2013
  Messages: 515
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tijikumbushe haya
   
 11. mzaramo

  mzaramo JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2013
  Joined: Sep 4, 2006
  Messages: 6,273
  Likes Received: 4,280
  Trophy Points: 280
  unapinga na ukweli hata nafsi yako inakusuta
   
Loading...