2002 FIFA WORLD CUP: Taifa kubwa la Tanzania na rafiki yake wa karibu Uganda wakiunganisha nguvu zao wanaweza kuandaa mashindano ya AFCON 2027/2029?

Habari zenu waungwana wa humu jamiiforums

Tanzania na Uganda zikiunganisha nguvu ya pamoja tunaweza kuandaa mashindano ya AFCON 2027, 2029 au 2031?

View attachment 1746765

Nilitamani sana kusema Tanzania na Kenya ila nimeona Waganda hatunaga nao mivutano sana ukilinganisha na Kenya.

Uganda imetupa dili la bomba la mafuta (East African Crude Oil Pipeline - EACOP) kutoka Hoima mpaka Tanga na sisi tuliwasaidia kwa kumuondoa dikteta Idd Amin dada, hivyo itoshe kusema kuna uhusiano mzuri sana wa kihistoria baina yetu sisi (Tanzania) na Uganda tofauti ukilinganisha na Kenya.

KUHUSU KOMBE LA DUNIA 2002 (KOREA KUSINI NA JAPAN)
=====
Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2002 lilikuwa Kombe la Dunia la 17 la FIFA, mahindano ya ulimwengu kwa timu za mpira wa miguu za kitaifa za wanaume zilizoandaliwa na shirikisho la kandanda duniani (FIFA).

View attachment 1746764

Ilifanyika kuanza 31 Mei 2002 hadi 30 Juni 2002 kwenye viwanja tofauti tofauti huko Korea Kusini na Japan, na mechi yake ya mwisho (fainali) iliandaliwa na Japan kwenye Uwanja wa Kimataifa huko Yokohama.

Jumla ya timu 32 zilifuzu kushiriki Kombe hili la Dunia, ambalo lilikuwa la kwanza kufanyika Asia, la kwanza kufanyika nje ya mabara ya Amerika au Ulaya, na vile vile la kwanza kuandaliwa kwa pamoja na nchi zaidi ya moja (Korea Kusini na Japan)

Je, inawezekana?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Tunajipanga kuandaa peke yetu 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220602-083922.png
    Screenshot_20220602-083922.png
    151.8 KB · Views: 9
  • Screenshot_20220602-084001.png
    Screenshot_20220602-084001.png
    144.1 KB · Views: 9
Back
Top Bottom