2002 FIFA WORLD CUP: Taifa kubwa la Tanzania na rafiki yake wa karibu Uganda wakiunganisha nguvu zao wanaweza kuandaa mashindano ya AFCON 2027/2029?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari zenu waungwana wa humu jamiiforums

Tanzania na Uganda zikiunganisha nguvu ya pamoja tunaweza kuandaa mashindano ya AFCON 2027, 2029 au 2031?

fghtvgf.jpg


Nilitamani sana kusema Tanzania na Kenya ila nimeona Waganda hatunaga nao mivutano sana ukilinganisha na Kenya.

Uganda imetupa dili la bomba la mafuta (East African Crude Oil Pipeline - EACOP) kutoka Hoima mpaka Tanga na sisi tuliwasaidia kwa kumuondoa dikteta Idd Amin dada, hivyo itoshe kusema kuna uhusiano mzuri sana wa kihistoria baina yetu sisi (Tanzania) na Uganda tofauti ukilinganisha na Kenya.

KUHUSU KOMBE LA DUNIA 2002 (KOREA KUSINI NA JAPAN)
=====
Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2002 lilikuwa Kombe la Dunia la 17 la FIFA, mahindano ya ulimwengu kwa timu za mpira wa miguu za kitaifa za wanaume zilizoandaliwa na shirikisho la kandanda duniani (FIFA).

fgtghbvfds.jpg


Ilifanyika kuanza 31 Mei 2002 hadi 30 Juni 2002 kwenye viwanja tofauti tofauti huko Korea Kusini na Japan, na mechi yake ya mwisho (fainali) iliandaliwa na Japan kwenye Uwanja wa Kimataifa huko Yokohama.

Jumla ya timu 32 zilifuzu kushiriki Kombe hili la Dunia, ambalo lilikuwa la kwanza kufanyika Asia, la kwanza kufanyika nje ya mabara ya Amerika au Ulaya, na vile vile la kwanza kuandaliwa kwa pamoja na nchi zaidi ya moja (Korea Kusini na Japan)

Je, inawezekana?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana.

Hapa jambo la kwanza ni kujikita ktk hali ya viwanja; kwa mkapa hamna shida lakini Dodoma,Arusha na Mwanza kunahitajika uboreshaji wa viwanja ktk hadhi ya kimataifa.

Hii miji ktk ku-accomodate matukio ya kimataifa inakidhi vigezo.
 
Hapa jambo la kwanza ni kujikita ktk hali ya viwanja; kwa mkapa hamna shida lakini Dodoma,Arusha na Mwanza kunahitajika uboreshaji wa viwanja ktk hadhi ya kimataifa .
Sahihi kabisa mkuu. Kuanzia 2021 mpaka 2031 ni takribani miaka 10. Huu muda hautoshi katika kufanya hayo mkuu?...
 
Tungekuwa na viwanja 5 kama Mkapa, ingekuwa rahisi kuomba collabo
Viwanja vya Arusha, Mwanza na Dodoma vikifanyiwa maboresho ndani ya miaka 10 mpaka 2031, hakika taifa kubwa la Tanzania litaweza. Kumbuka maboresho ni gharama ndogo zaidi tofauti na kujenga vipya.
 
Back
Top Bottom